Jinsi ya Kujisajili na Kutumia AzamTV MAX App, AzamTV Max, Jisajili na AzamTV Max, AzamTV Max Huduma kwa wateja, Habari, karibu katika makala hii itakayoenda kukuangazia juu ya App ya Azam Max kutoka kampuni ya Azam Tv..
Kama wewe ni miongoni mwa familia ya Azam Tv na unatumia simu janja au unatamani kujiunga na familia ya Azam Tv na hauna kisimbuzi chochote kile cha Azam Tv basi unaweza kutumia App ya AzamTV Max ili kufurahia vipindi vya televisheni vinavyorushwa na Azam Tv.
Jinsi ya Kujisajili na Kutumia AzamTV MAX App
Azam Tv ni moja miongoni mwa kampuni kubwa na pendwa zaidi kwa utoaji wa huduma ya urushaji wa channel za tv na kupitia AzamTV Max App maarumu iliyotendenezwa na Azam Tv watumiaji na wapenzi wa Azam Tv wamekua huru kutizama channel zirushwazo na Azam Tv wakati na maharo popote pale bira wasa wasasi wala usumbufu wa aina yoyote ile.
Jinsi ya Kudownload AzamTV Max
Ili kuweza kufurahia channel zirushwazo na App ya AzamTV Max basi ni lazima uweze kuidownload na kuinstall kwenye simu janja yako.
App ya Azam Max inapatikana Play Store, App Store pia unaweza kwenda google na kudownload AzamTV Max APK kwa njia zote hizo unaweza kua na uwanja wa kudownload na kuweza kuinstall App ya AzamTv Max.
Jinsi ya Kujisajili kwenye Azam Max
Mara baada ya kupakua na kuinstall App ya AzamTv Max sasa hatua inayofuata ni kujisajili kwenye App ili uanza kugurahia maudhui ya vipindi vinavyorushwa na channel za Azam Tv
Ili kujisajili kwa mtumiaji wa mara ya kwanza fuata hatua hizi hapa chini
1. Nenda kwenye simu yako na ufungue App ya AzamTV Max
2. Kisha itakutaka ujaze tarifa fuata maelekezo
3. Ingiza namba ya kisimbuzi chako ili kuunganisha kisimbuzi chako na App yako
4. Kumbuka wakati wa kujisajili utahitaji namba ya simu au email
5. Tengeneza neno siri ambalo utalikumbuka kwa urahisi
6. Hifadhi neno siri na namba ya simu au email uliyotumia kujisajili kwani vitatumika kama login details hapo baadae
7. Ingia kwenye App na ufurahie maudhui ya channel za Azam TV kupitia AzamTV Max
Njinsi ya Kuingia (login) kwenye Azam Max
Baada ya kupakua na kujisajili kwenye AzamTv Max sasa utahitaji kuweza kulogin kwenye App yako ya AzamTv Max, hapa chini ni hatua za kulogin kwenye AzamTV Max
1. Ili kuweza kulogin kwenye App ya AzamTV Max ingia kwenye simu yako na usungue App
2. Kisha itakupa chaguzi za kuweza kutumia kuingia kwenye akaunti yako ya AzamTV MAX,
- Unaweza kulogin kwa kutumia email yako
- au unaweza kuingia kwa kutumia namba yako ya simu ulioitumia wakati wa kujisajili
3. Kisha utaweka neno siri na utabonyeza INGIA
4. Utakua umesha ingia kwenye akaunti yako ya AzamTV MAX.
Vifurushi vya Azam Max
Vifurushi vya AzamTV MAX vimegaweanywa katika makundi makuu mawili amabayo ni vifurushi vya WIKI na vifurushi vya MWEZI
-Vifurushi vya WIki
- Kifurushi cha Silver – Kina channel 94 malipo yake ni shilingi 11000, Kifurushi hiki ni kwa matumizi ya App haikifanyi kazi kwenye kisimbuzi.
- Kifurushi cha Bronze – Kina channel 76 malipo yake ni shilingi 5000, Kifurushi hiki ni kwa matumizi ya App haikifanyi kazi kwenye kisimbuzi.
– Vifurushi vya Mwezi
- Kifurushi cha Gold – Kina channel 99 malipo yake ni shilingi 25000, Kifurushi hiki ni kwa matumizi ya App haikifanyi kazi kwenye kisimbuzi.
- Kifurushi cha Silver – Kina channel 94 malipo yake ni shilingi 23000, Kifurushi hiki ni kwa matumizi ya App haikifanyi kazi kwenye kisimbuzi.
- Kifurushi cha Bronze – Kina channel 76 malipo yake ni shilingi 16000, Kifurushi hiki ni kwa matumizi ya App haikifanyi kazi kwenye kisimbuzi.
- Kifurushi cha EONII – Kina channel 6 malipo yake ni shilingi 2000, Kifurushi hiki ni kwa matumizi ya App haikifanyi kazi kwenye kisimbuzi.
NB; Tafadhari kumbuka kuangalia zipata kwenye kila kifurushi kupitia ukrasa wa HOME kama zinakidhi mahitaji yako kabla ya kufanya malipo ya kifurushi hicho
Jinsi ya Kufanya Malipo ya Vifurushi vya AzamTv Max
Ili kulipia kifurushi cha AzamTV MAX tafadhari fuata hatua zifuatazo
- Ingia kwenye chaguzi za vifurushi
- bonyeza kwenye kifurushi unachotaka kufanya malipo Mfano mwezi
- Chagua aina ya kifurushi unachotaka kukifanyia malipo mfano Silver
- Bonyeza kwenye alama ya duara kisha utaona alama ya “TIKI” kwenye kiduara
- Angalia chini utaona maneno Lipia na uyabonyeze
- Kisha bonyeza palipoandikwa Thibitisha Kifueushi
- Chagua njia ya kufanya malipo- Kunanjia kuu mbili za kufanya malipo nazo ni njia ya creadit/Debit Card au malipo kwa njia ya mitandao ya simu kama vile Azam Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money na M-Pesa,
- Ukisha chagua njia ya kufanya malipo fuata maelekezo yatakayoendelea kujitokeza kwenye skrini yako ili kukamilisha malipo yako
Faida na Hasara za Kutumuia AzamTV MAX
Faida za Kutumia AzamTv Max
Kama bado hujajiunga na AzamTv MAX basi tambua unakosa vitu vingi sana kwani kutumia AzamTV Max ku nakupa nafasi ya kufurahia maudhui yanayorushwa na channel za Azam Tv hata kama hujanunua kisimbuzi cha Azam Tv
Zifuatazo ni faida za kutumia AzamTV Max App
- Kutazama channel za Azam Tv hata kama huna kisimbuzi cha Azam RV
- Gharama nafuu zaidi
- Kufurahia maudhui ya Azam Tv mahari popote
Hasara za Kutumia AzamTv Max
Hakuna kiti kisichokua na hasara, pia AzamTV MAX inahasara zake. Hapa chini ni hasara za utumiaji wa AzmTV MAX App
- Gharama za ziada – licha ya kulipia kifurushi cha AzamTv Max lakinin pia itakuhitaji huduma ya Internet ili kuweza kufungua channel zake
- Matumizi mabaya ya muda kwa kuwa na AzamTV MAX inakupa uhuru wa kutazma nchannel za Azam Tv wakati wowote na mahari popote kitu ambaccho kinaweza perekea madumizi mabovu ya muda.
Azamtv max Huduma kwa wateja
Ili kuboresha huduma zao AzamTv Max wamekusogezea huduma kwa wateja karibu nawe. Pindi unapopata changamoto ya aiana yoyote ile kwenye matumizi ya AzamTV Max basi usisite kuwasiliana nao kwa mawasiliano hayo hapo chini
Simu Namba
- 0677 996 644
Hitimisho;
AzamTv Max App inakupa uhuru wa wewe unayetamani kuweza kujiunga na familia ya Azam Tv ili kufuruahia huduma ya channel zinazorushwa kupitia Azam TV buree hata kama wewe si mteja wa kisimbuzi cha Azam Tv. Ukiwa na AzamTv MAX ni uwamuzi wako kufanya malipo ya vifurushi zinavyotolewa na Azmtv Max pekee kwa wiki au Mwezi.
Mapendekezo ya Mhariri
1. Jinsi Ya Kurudisha Channel Zilizopotea Kwenye Kisimbizi Cha Azam TV
2. Njinsi ya Kuweza Kutazama Channel za Azam Tv Bure
3. Channel Zote za Visimbuzi Vya Azam TV
4. Jinsi Ya Kulipia King’amuzi Cha Azam Tv kupita Mitandao Ya Simu
5. Bei ya Vifurushi vya Azam TV Kisimbuzi Cha Dishi Na Antena 2024