Jinsi ya kubadilisha kifurushi cha Startimes
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
BONYEZA HAPA KUJIUNGA NA TELEGRAM CHANNEL YETU
Habari ya wakati huu mpenzi wa Habarika24, Karibu tena katika makal hii ambayo itaenda kukupa maelekezo juu ya njisi ya kubadilisha kifurushi cha Startimes. Kama wewe ni mteja wa kisimbuzi cha Startimes na ungependa kubadili kifurushi unachotumia kwa sasa na kwenda kwenye kifurushi kipya basi makala hii itakua na umuhimu mkubwa sana kwako, kwani hapa tutakuwekea hatua na njia zote za kufuata ili uweze kubadili kifurushi cha akaunti yako ya Startimes.
Kuhusu Startimes
Ilianzishwa mwaka 1988, StarTimes Group ni kampuni ya vyombo vya habari vya kimataifa ya China yenye makao yake makuu mjini Beijing. Baada ya miaka mingi ya maendeleo, StarTimes imekuwa Kiunganishi kikuu cha Mfumo, Mtoa Huduma za Teknolojia, Opereta wa Mtandao, na Mtoa Maudhui katika tasnia ya utangazaji ya televisheni Afrika.
Tangu mwaka 2008 StarTimes ilipoanza kufanya kazi katika soko la Afrika, kampuni hiyo imekuwa ikijitahidi kutimiza dhamira yake kuu: “Kuhakikisha kwamba kila familia ya Kiafrika inaweza kupata, kumudu, kutazama na kushiriki uzuri wa TV ya kidijitali”.
Leo, kama waendeshaji wa Televisheni ya kidijitali inayoongoza barani Afrika, StarTimes ina watumiaji milioni 13 wa DVB na watumiaji milioni 27 wa OTT, na inashughulikia idadi ya watu wote wa bara kwa mtandao mkubwa wa usambazaji. Imeanzisha tanzu katika nchi zaidi ya 30 za Afrika.
StarTimes sasa ndiyo chapa pekee ambayo kwa wakati mmoja inaendesha biashara za DTT, DTH na OTT katika soko la Afrika, na kampuni pekee inayojishughulisha na biashara ya B2B na B2C kwa wakati mmoja. StarTimes inalenga kuwa kikundi cha wanahabari chenye ushawishi wa kimataifa.
StarTimes inasaidia kuhakikisha kuwa bara la Afrika na maendeleo ya vyombo vya habari yanapiga hatua hadi ngazi ya juu katika utangazaji wa televisheni ya kidijitali. StarTimes ni mshirika mkuu wa Afrika katika juhudi zake za kuhama kutoka mfumo wa analogi kwenda dijitali.
Teknolojia na Bidhaa
StarTimes imeanzisha mfumo mkubwa wa mtandao ambao unaweza kutoa huduma kwa makumi ya mamilioni ya watumiaji. Pamoja na majukwaa 4 makubwa ya upokezaji wa mawimbi, jukwaa la satelaiti ya mawimbi, jukwaa la Televisheni ya satelaiti ya Direct-to-Home (DTH), jukwaa la Televisheni ya kidijitali (DTT) na jukwaa la Juu-juu (OTT), StarTimes imefanya ishara yake inapatikana katika bara zima la Afrika, bara la Ulaya na sehemu ya bara la Asia.
Televisheni ya satelaiti ya utangazaji wa moja kwa moja, pia inajulikana kama DTH, inasambaza vipindi vya televisheni kwa kutumia mawimbi yanayotumwa kutoka kwa vituo vya redio vya anga (k.m. setilaiti za DVB). Katika mifumo ya DTH, mawimbi hutumwa kutoka kwa satelaiti ya utangazaji wa moja kwa moja kwenye urefu wa wimbi na ni dijitali kabisa. Utumaji na chaneli zingine hazijasimbwa kwa njia fiche na kwa hivyo ni bure-kwa-hewa au kutazama bila malipo, wakati chaneli zingine nyingi hupitishwa kwa usimbaji fiche (televisheni ya kulipia), inayohitaji usajili.
DTT ni utekelezaji wa teknolojia ya kidijitali. DTT hutoa chaneli zaidi na ubora bora wa picha na sauti, kwa kutumia matangazo ya angani kwa antena ya kawaida (au angani) badala ya sahani ya satelaiti au unganisho la kebo. DTT hupitishwa kwa masafa ya redio kupitia mawimbi ya hewa, ambayo yanafanana na televisheni ya kawaida ya analogi isipokuwa tofauti moja ya msingi, matumizi ya visambazaji visambazaji vingi ili kuruhusu upokeaji wa chaneli nyingi kwenye masafa moja ya masafa.
Ili kutimiza mahitaji yanayoongezeka ya video za mtandaoni, StarTimes inaanzisha huduma yake ya kutiririsha video, StarTimes ON, katika soko la Afrika. Kabla ya Kombe la Dunia la Urusi 2018, StarTimes ilizindua rasmi huduma ya kutiririsha video, baada ya kuwawezesha watumiaji wa Kiafrika kutazama mechi zote 64 za Kombe la Dunia katika HD kwenye StarTimes ON. Sasa StarTimes ON imekusanya watumiaji milioni 27 sokoni, na kuwa mojawapo ya majukwaa matatu makubwa ya usambazaji wa video za kampuni hiyo.
Vifaa vya terminal vya StarTimes vimeundwa mahususi kwa ajili ya soko la Afrika na vinashughulikia matukio tofauti ya utumaji maombi, ambayo ni pamoja na kisikoda cha DTH, avkodare ya DTT, Kisimbuaji Combo, Kisimbuaji cha DVB+OTT, Seti ya TV ya Dijitali, Projector TV na mfumo wa Solar Power, n.k.
Startimes ndio kampuni pendwa zaidi nchini Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla, hii inatokana na vipindi bora vya television vinavyorushwa na baadhi ya chaneli zilizopo kwenye visimbuzi vyake. King’amuzi cha Startimes kinapendwa hasa na watu wa jinsia ya kike kutokana na kuwepo kwa vipindi bomba vya tamthiliya vinavyo rushwa na chanel kama vile star swahili, star swahili plus na Novela E.
Jinsi ya kubadilisha kifurushi cha Startimes
Vifurushi vya Startimes
Kabla hatujaenda kuangalia mwongozo wa jinsi ya kubadilisha kifurushi cha startimes basi kwa ufupi embu tuangazie kwanza aina ya vifurushi vinavyopatikana katika king’amuzi cha startime kwa decoda zote.
Vifurushi vya startimes vimegawanyika katika makundi mawili kundi la kwanza ni watumiaji wa kisimbuzi cha antena na kundi la pili ni watumiaji wa kisimbuzi cha Dishi
a) Vifurushi vya Startimes Kwa Kisimbuzi cha Antena
- Nyota
- Mambo
- Uhuru
b) Vifurushi vya Startimes Kwa Kisimbuzi cha Dishi
- Nyota Tsh 11,500
- Smart Tsh 23,000
- super Tsh 38,000
- Chinese Tsh 50,000
Hivyo basi baada ya kuvitambua vifurushi vinavyopatikana katika king’amuzi cha startimes sasa tunaweza anza jifunza jinsi ya kubadilisha kifurushi cha startimes, lakini kama bado hutambui bei na idadi ya chaneli kwa kila kifurushi hapo juu basi usiwe na hofu kwani ipo makala ambayo inatoa maelezo ya kutosha kuhusu vifurushi vya startimes, bei zake na idadi ya chaneli kwenye kila kifurushi. Ili kusoma makala hiyo kabla ya kujua jinsi gani ya kubadlisha Kifurushi cha startimes BONYEZA HAPA
Jinsi ya kubadilisha kifurushi cha Startimes
Ili mtumiaji wa king’amuzi cha startimes aweze kubadilisha kifurushi cha kisimbuzi chake lazima afuate baadhi ya hatua kwa njia tofauti tofauti.Hapa chini tumekuwekea njia mbali mbali za kufuata ili uweze kubadilisha kifurushi cha king’amuzi chako cha startimes;
1. Jia ya Mtandaoni
Unaweza kubadilisha kifurushi chako cha startimes kwa kutembelea wavuti ya startimes ON. Ili kuingia katika tovuti ya Startimes On irtakubidi uwe na kiffa kitakachoweza kukupeleke kwenye mtandao wa internet kisha kwenye ukrasa wa google utatafuta Startimes One na itakupeleka kwenye ukrasa wa startimes On au unaweza kutumia linki hii hapa kwneda moja kwa moja kwenye ukrasa wa startimes one – http://m.startimestv.com/browser/
– Ukrasa wa startimes on utafunguka kisha utabonyeza palipoandikwa Recharge na itakupeleka kwenye ukrasa wa kujaza taarifa za namba ya kadi ya king’amuzi chako, mara baada ya kuzaja namba ya king,amuzi chako akaunti yako itafunguka ikiwa na taarifa zote ikiwemo aina ya kifurushi unachokitumia kwa wakati huo.
Ili kubadilisha bonyeza kwenye Kifurushi sha sasa na ikafungua orodha ya vifurushi vingine kisha bonyeza kifurushi unacho kiitaji ili kubadili na utakua umefanikisha kubadili kifurushi chako.
2. Njia ya Huduma Kwa Wateja
Pia kubadilisha kirufushi chako cha startimes unaweza kutumia njia ya kupiga simu moja kwa moja startimes kupitia namba zao za huduma kwa mteja. Kuwa siliana na startimes huduma kwa mteja tafadhari piga simu kupitia namba hizi hapa chini;
- 758828234
- 764700800
Mara baada ya kupiga simu mtoa huduma wa startimes atapokea simu yako na kukuuliza namba za kisimbuzi chako hakikisha unaifahamu amba ya kadi ya kisimbuzi chako, Kisha utampa maelekezo ya hitaji la kubadili kifurushi cha kisimbuzi chako na yeye atakupa maelekezo yote ya kufuata ili kubadili.
3. Njia ya Startimes ON App
Kama unatumia simu janja unaweza kubadili kifurushi cha startimes kwa kutumia aplikeseni ya Startimes On. Unachotakiwa ni kuinstall application ya startimes on kwenye simu yako na kisha kujisajili kwa kuig=ngiza namba ya kadi ya kisimbuzi chako na utakua umejisajili.
Ndani ya application ya Startimes On sasa unaweza kubadili kifurushi chako kirahisi zaidi.
4. Njia ya SSD Code
Hapa utatumia simu yako kwa kupiga code maalumu za Startimes ambazo ni *150*63#, mara baada ya kupiga code hizo utafungua ujumbe kama huu hapa chini na utatakiwa kufanya chaguzi kulingana mahitaji yako.
Karibu StarTimes
Chagua:
- Kiswahili <
- English
( Tunachagua kiswahili,una bofya OK )
- Kujua salio
- Kulipia kwa vocha
- Sajili dekoda yako mpya
- Q and A ( Swali na Jibu )
- Chagua kifurushi <
Utachagua namba 5 chagua kifurushi na itafungua ukrasa mwingine tafadhari fuata maelekezo kwa usahihi zaidi hadi pale utakapofanikisha kubadilisha kifurushi cha king’amuzi chako cha startimes.
Hitimisho
Sisi kama Habarika24 tuanakushauri wewe mteja wa startimes kama unataka kubadili aina ya kifurushi chako ni vyema sana kutumia njia ya kupiga simu moja kwa moja kwa huduma kwa wateja kwani njia hiyo itakupa majibu ya haraka zaidi na hata kama utakua na changamoto nyingin unaweza wauliza na kupatiwa ufumbuzi.
Mapendekezo Ya Mhariri;
1. Jinsi ya kubadilisha kifurushi cha Azam TV
2. Jinsi ya Kusajiri Kampuni Tanzania
3. JINSI ya Kupata TIN Number Online
4. jinsi ya Kujisajili na Huduma za NBC Mobile Banking
5. Jinsi ya Kutoa Pesa Kwenye Akaunti ya NBC Bank
6. TIRA MIS Uthibitishaji wa Uhai wa Bima Ya Gari
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku