Jinsi Ya Kuangalia Salio La NSSF Kwa Njia ya Simu (NSSF Balance Check), Habari za Wakati huu, tunapenda kukukaribisha tena katika mkala hii amaboy utaenda kujifunza kwa ufupi zaidi jinsi ya kuangalia salio la NSSF kwa njia ya Simu.
Kama wewe ni mmoja miongoni mwa wale wanaohitaji kutumia mtandao was imu ya mkononi kuweza kutazama salio lako la NSSF tambua kua kunanjia rahisi sana utakayoweza kuitumia kupitia mitandao ya simu kama vile mtandao wa Vodacom, Airtel, Halotel na Tigo.
Ili kutumia njia hii tafadhari hakikisha unasimu yenye mtandao mmoja kati ya hiyo hapo tulioitaja hapo juu kisha fuata hatua zifuatazo;
Jinsi Ya Kuangalia Salio La NSSF Kwa Njia ya Simu (NSSF Balance Check)
Kunanjia mbali mbali za kuangalia salio la akaunti yako ya NSSF. Hapa habarika24 tutaenda kuangalia njia moja baada ya nyingine na jinsi zinavyotumika katika kuangalia salio la akaunti yako ya NSSF.
Kuangalia Salio la Akaunti ya NSSF Kwa Njia Ya SMS
Hapa tutaenda kuangalia jinsi ya kuangalia salio la akaunti ya NSSF yako kwa kutuma jumbe mfupi yani SMS. Fuata hatua hizi hapa chini
- Fungua sehemu ya kuandikia meseji
- Kisha Andika ujumbe wenye neno “NSSF Balance” kisha ufwatiwe na namba yako ya NSSF, kwa mfano ujumbe unatakiwa usomeke hivi “ NSSF Balance 5378298127”
- Baada ya kukamilisha kuandika uhumbe sasa tuma ujumbe huo Kwenda namba 15200
- Mara baada ya ujumbe wako kufanikiwa kutuma, utapokea mesji yenyekuonyesha salio la akaunti yako ya NSSF.
Kupata Statement ya Akaunti ya NSSF Kwa Njia Ya SMS
Hapa tutaenda kuangalia jinsi ya kupata statement ya akaunti yako ya NSSF kwa njia ya ujumbe mfumpi wa maandishi SMS. Fuata hatua hizi hapa chini ili kuweza kupata taarifa za statement ya akaunti yako ya NSSF kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS)
- Hatua ya kwanza ni kufungu uwanja wa kutumia sms kwenye simu yako
- Tuma ujumbe wenye neno “NSSF Statement” ukifuatiwa na namba yako ya uanachama wa NSSF. Mfano: NSSF Statement 123456789.
- Tuma ujumbe huo kwenda namba 15200
- Baada ya kufanikiwa kutuma ujumbe huo utapokea mesiji yenye taarifa za akaunti yako ya NSSF

Kuangalia Salio La NSSF Kwa Njia ya WhatsApp
Licha ya kuangalia salio la akaunti yako ya NSSF kupitia ujumbe wa simu lakini pia unaweza tumia njia ya WhatsApp kuweza kutazama salio lako, embu fuata hatua hizi hapa chini kutazama salio lako kupia njia ya WatsApp;
- Kwanza kabisa itakupasa kuhifadhi namba hii kweye simu yako 0756 140 140
- Kisha fungua akaounti ya WhatsApp na utume ujumbe wenye neno “hello” au “Habari”
- Kisha fuata maelekezo utakayopewa ili kuweza kuangalia salio la akaunti yako ya NSSF au taarifa za akaunti yako
Kuangalia Salio la NSSF kwa Programu ya Simu Janja
Pia unaweza kutazama taarifa au salio la akaunti yako kwa kutumia applikasioni kwenye simu janja, unachotakiwa kufanya ni kufuata hatua hizi hapa chini;
- Nenda kwenye play store ya simu yako na upakue na kuhifadhi program ya NSSF Taarifa
- Kisha ingia kwenye program kwa kujaza taarifa zako za kimsingi za Nssf
- Kisha utaweza kua na uwezo wa kuangalia salio la akaunti yako, mwenendo wa michango yako na hata taarifa nyingine muhimu
Mambo Muhimu ya Kuzingatia
Kumbuka si mara zote unapotumia njia ya simu taarifa zinaweza kuwa sahihi kwa asilimia mia moja la asha taarifa unazozipokea kwa njia ya simu juu ya salio lako mara nyingi upisha kidogo sana na taarifa za msingi, hii ni kutokana na kuhuwishwa au kurekebishwa kwa taarifa za akaunti yako kuchelewa wakati wewe ndio unatazama taarifa za akaunti yako
Hivyo basi licha ya njia hii kua rahisi zaidi juu yaw ewe mtumiaji kupa taarifa za akounti yako kwa haraka zaidi lakini pia tunashauli utumie njia nyingi ya kimsingi itakayokuwezesha kupata taarifa zilizo sahihi kabisa kuhusu akaunti yako, unaweza kutembelea moja kwa moja kwenye ofisi za NSSF zilizo Jirani nawe ukiwa na nambali ya akaunti yako.
Mawasiliano Zaidi na NSSF
Kama utahitaji mawasiliano zaidi na NSSF basi unaweza kufanya mawasiliano na watu wa huduma kwa wateja kwa tumia mawasiliano hayo hapo chini;
- National Social Security Fund
- P.O.Box 1322, Benjamin Mkapa Pension Towers, Azikiwe St, Dar Es Salaam,Tanzania
- [email protected]
- 0 (75) 6140140 | 0800116773
- (255) (22) 2200037
>>Namna ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Kwa Mtu Mzima
>>Jinsi ya Kuandika Barua ya Kuomba Kazi ya Ualimu TAMISEMI 2024
>>Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mtendaji wa Kijiji na Mtaa