Jinsi ya kuangalia Namba ya Simu Mitandao Yote, Mwongozo wa kutazama namba ya simu mitandao ya Airtel, Vodacom, TTCL, Tigo & Halotel, Habari karibu tena kwenye makala hii fupi itakayoenda kukupa mwongozo wa code ya kuangalia namba ya simu kwa mitandao ya Airtel, Vodacom, TTCL, Tigo na Halotel.
Kama wewe ni mtumiaji wa simu na bado hufahamu namba yako ya simu basi makala hii itakupa mwongozo wa jinsi ya kuweza kuangalia namba yako ya simu ya mtandao unao tumia.
Muundo wa Namba ya Simu Tanzania
Namba ya simu Tanzania ina muundo uliogawika katika sehemu kuu 3 ambazo ni
1. Code ya Nchi (Huundwa na tarakimu 3)
2. Tarakimu za Mtandao wa simu (Huundwa kwa tarakimu 2)
3. Namba za Mtumiaji (Huwa na tarakimu 7)
Ili kuwza kupata maelezo ya kina kuhusu muundo wa namba za simu za Tanzania tafadhali unaweza tembelea “Orodha ya Code Za Mitandao ya Simu Tanzania”
Jinsi ya kuangalia Namba ya Simu Mitandao Yote
Ili kuweza kutazama namba ya SIM Kadi yako unaweza tumia njia hizi hapa chini. Kuna njia kuu 2 hii ni kutokana na aina ya SIM Kadi aliyonayo mtumiaji
1.Laini za Simu za Zamani
Kwa watumiaji wa laini za zamani namba ya simu ya SIM Kadi ilikua ikiandikwa nyuma ya SIM Kadi husika. Kama SIM Kadi iko ndani ya simu ili kuweza kujua namba yako ya simu utahitajika kuzima simu kisha kutoa laini (SIM Kadi) na nyuma ya laini ya simu utaona namba yako ya simu.
2. Laini Mpya za Simu
Kwa laini mpya mabolesho yameweza kufanyika na namba ya simu imekua ni fiche kutoka kwenye laini. Ilikuweza kupata namba ya simu kwenye laini za kisasa mtumiaji wa simu itampasa kupitia mchakato wa kupiga code maalumu.
Hapa tutaenda kukuonyesha hatua kwa hatu njinsi ya kuangalia namba ya simu kwa laini za kisasa kwenye mitandao yote ya simu kama vile Aurtel,Halotel, Tigo/Yas, Vodacom, TTCL na Zantel.
- Jinsi ya kujua namba ya simu ttcl
- Jinsi ya kujua namba ya simu tigo
- Jinsi ya kujua namba ya simu halotel
- Jinsi ya kujua namba ya simu airtel
1. Chukua simu yako na kisha pia *106#
2. Kutoka kwenye maelezo chagua 1 (Angalia Usajili)
3. Kisha ujumbe utakuja kwenye skrini ya simu yako ukiwa na namba yako ya simu na majina yako kamaulivyosajili laini yako.