Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita (NECTA) ni moja kati ya matokeo muhimu katika safari ya elimu ya kila mwanafunzi nchini Tanzania. Matokeo haya huchangia kwa kiasi kikubwa mwenendo wa wanafunzi nchini kwasababu ndio hutumika kama kigezo cha kujiunga na elimu ya ngazi ya juu kama vile elimu ya shahada na astashahaada. Pia Matokeo ya NECTA kidato cha sita hutumia na baadhi ya makampuni na tasisi katika kuajiri wafanyakazi wa nafasi mbalimbali.
Wakati wanafunzi, wazazi, walezi, na walimu wote wanasubiri kwa hamu kubwa zoezi la kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha sita na Baraza la mitihani Tanzania (NECTA) ni muhimu kuwa na taarifa sahihi na za kuaminika kuhusu jinsi ya kuangalia matokeo ya mtihani wa Kidato cha Sita 2024. Mwongozo huu wa kina umetayarishwa kwa lengo la kuwapa wanafunzi, wazazi, walezi, na walimu taarifa zote muhimu ili kuhakikisha wanapata matokeo yao kwa urahisi na bila usumbufu.
Mwongozo huu utaelezea kwa undani njia mbalimbali ambazo wanafunzi wanaweza kutumia kuangalia matokeo yao, ikiwa ni pamoja na kuangalia kupitia mtandao, ujumbe mfupi wa simu (SMS), au moja kwa moja shuleni. Aidha, mwongozo huu utawapa vidokezo muhimu vya kuzingatia kabla na baada ya kuangalia matokeo, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kujiandaa na nini cha kufanya baada ya kupokea matokeo.
Jinsi Ya Kuangalia Matokeo Ya Kidato Cha Sita 2024
Kuna njia kuu tatu tutazoenda kuziangalia katika kutazama matokeo ya kidato cha sita amabazo ni;
- Kuangalia Matokeo ya Kidato Cha Sita Mtandaoni (Online)
- Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Sita Kupitia USSD
- Kuangalia Matokeo ya NECTA Kidato cha Sita Mashuleni
Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Sita 2024 Kupitia Mtandao (Online)
Njia rahisi na inayopendelewa na wengi ni kuangalia matokeo ya Kidato cha Sita 2024 kupitia mtandao. Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) hutoa matokeo haya kwenye tovuti yao rasmi. Ili kuangalia matokeo yako, fuata hatua zifuatazo:
1. Tembelea Tovuti ya NECTA
- Kwanza kabisa kupitia kifaa chako cha internet tembelea tovuti rasmi ya NECTA: www.necta.go.tz.
2. Tafuta Menyu ya Tovuti na Bonyeza “Matokeo”
kwenye ukrasa wa mbele wa tovuti ya NECTA, tafuta nenyu kuu iliyoko juu na ubonyeze palipo andikwa “Matokeo.”
3. Chagua “Matokeo ya ACSEE”
baada ya kubonyeza matokeo itatokea ordha ya matokeo yote kulingana na ngazi ya elimu kisha chagua “Matokeo ya ACSEE” ambayo ndio matokeo ya Kidato cha Sita.
4. Changa Mwaka 2024”
Baada ya kubonyeza ACSEE yatatokea matokeo ya miaka mbali mbali na hapa utachagua mwaka 2024
5. Kisha Tafuta Shule Uliyo Malizia
Mattokeo yatafunguka kwa mgawanyo wa shule hapa utatafuta shule uliyofanyia mtihani na kuibonyeza na kisha matokeo yatafunguka.
6. Ndani Ya Matokeo Ya Shule Tafuta Jina Lako
Baada ya matokeo ya shule kufunguka sasa unaweza kutafuta jina lako na kusave natokeo yako
Jinsi Ya Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Sita 2024 Kupitia USSD
- Piga *152*00#
- Chagua namba 8. ELIMU
- Chagua namba 2. NECTA
- Chagua aina ya huduma 1. MATOKEO
Chagua aina ya Mtihani 2. ACSEE - Ingiza Namba ya Mtihani na Mwaka Mfano: S0334-0556-2019
- Chagua aina ya Malipo (Gharama kwa SMS ni Tshs 100/=)
- Baada ya kukamilisha malipo, utapokea ujumbe mfupi wenye matokeo.
Kuangalia Matokeo ya NECTA Kidato cha Sita Mashuleni
Shule nyingi nchini Tanzania hupokea matokeo ya wanafunzi wao moja kwa moja kutoka NECTA na kuyabandika kwenye ubao wa matangazo wa shule. Wanafunzi wanaweza kutembelea shule zao ili kuangalia matokeo yao kwenye ubao huu.
Aidha, walimu wakuu, walimu wa darasa, au maafisa wengine wa shule wanaweza kutoa msaada kwa wanafunzi ambao wanakabiliwa na changamoto zozote katika kuangalia matokeo yao ya mtihani wa kidato cha sita 2024. Ni muhimu kwa wanafunzi kuwasiliana na shule zao mapema ili kujua utaratibu maalum wa kuangalia matokeo shuleni.
ANGALIA HAPA Matokeo ya Kidato cha Sita 2024 (NECTA Form Six Results)
ALL CENTRES | A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M |
N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z |
All School Form Six Results 2024