Umuhimu Wa Kuangalia Deni la Gari
Kama wewe ni mliki wa gari au dereva wa gari basi tambua ya kua kunafaida nyingi sana za kutazama deni la gari yako kupitia mfumo wa TMS Traffic Check. Hapa chini ni miongoni mwa faida za wewe kama mliki wa gari kuangaria deni la gari yako mara kwa mara:
Inasaidia Kuepusha Usumbufu Usio wa lazima Usumbufu
- Ukiwa na tabia ya kutizama kama gari lako linadeni itakupa wakati mzuri wa kuweza kushugurikia kabla hata mambo hayajawa mabaya zaidi kwa kufikishwa mbele ya sheria.
Itakuongezea Nidhamu katika Matumizi ya Gari Yako
- Uangalizi wa deni la gari itakupa wasaa wa kua makini katika matumizi ya gari lako barabarani na kuepusha kupigwa faini kutokana na uvunjifu wa sheria za barabarani
Inasaidaia katiak Kufuatilia Malipo Ya Gari Lako
- Kuwa na tabia ya kuchunguza deni la gari lako itakupa urahisi wa kujua kama malipo ya deni yanafika kwa usahihi mahari husika na kuondolewa kwa deni ulilofanyia malipo

Jinsi Ya Kuangalia Deni La Gari
Baada ya kuweza kutizama ni jinsi gani ilivyokua muhimu kwa wewe kama mliki wa gari kuweza kutizama deni la gari yako basi sasa embu tuangalie jinsi ya kuweza kuanagalia deni la gari yako kwa urahisi zaidi;
Mambo ya Kua nayo Kabla ya Kuangalia Deni la Gari Yako
- Hakikisha unasimu janja au kompyuta
- hakikisha kifaa hicho kinauwezo wa kuunganishwa na intaneti
- Unga kifaa chako na internet
- Hakikisha unanamba ya usajiri wa gari lako
Hatua za Kufuata Ili Kuangalia Deni la Gari Yako
Hapa chini ni hatua za kufuata ili kuweza kutizama kama gari yako inadeni au haina kupitia mfumo wa TMS Traffic Check
1.Chukua simu yako au Kompyuta na Unganisha na Internet:
Hatua ya kwanza kabisa ni kuhakikisha kifaa chako iwe simu au kompyuta imeunganiswa vizuri na mtandao wa internet
2. Fungua Broswer Unayotumia Kwenye kifaa Chako
Kisha nenda kwenye app au application zilizopo kwenye kifaa chako na ufungue kivinjali (broswer) unayotumia kuingilia kwenye mtandao inaweza kua google chrome, Safari au hata Mozira
3. Fungua Tovuti ya TMS Tanzania Traffic Check
Kupitia broswer yako ingia na utafute TMS Tanzania Traffic Check na ikisha funguka bonyeza linki yake ili kuingia katika tovuti yake au unaweza kutumia linki hii hapa kwenda maoja kwa moja kwenye tovuti: https://tms.tpf.go.tz
4. Ingiza Namba ya Usajili wa gari:
Baada ya tovuti kufunguka sasa utaona kisanduku za kujaza na hapo utatakiwa kujaza namba ya gari iliyosajiliwa ambayo unataka kujua taarifa za deni lake
5. Bonyeza “Tafuta”:
Mara baada ya kuingiza namba ya gari unaweza sasa kubonyeza palipo andikwa “TAFUTA” ili kuruhusu mfumo kupiti taarifa za gari lako.
Baada ya mfumo kuweza kutafuta taarifa utakunyesha kwenye skrini kama gari haidaiwi mfumo utasema pia kama gari linadaiwa mfumo utaota maelezo
Tazama Video ya Jinsi ya Kuangalia Deni la Gari Kwa Uwelwa Zaidi
TMS Traffic Check huu ni mfumo wa kimtandao ulioanzishwa kwa lengo mahususi la kuwasaidia madereza na wamiliki wa magari kuweza kujua mwenendo wa faini na madeni ya magari yao kutokana na uvunjifu wa sheria za barabarani
Kwa maelezo Zaidi Wasiliana na;
TPF ICT
P.o.Box 961
Dodoma, Tanzania
Phone: 0262323585
Email: [email protected]
Hitimisho
Wewe kama mliki wa gari basi hakikisha unatembela mfumo huu wa TSM Traffic Check ili kuweka mazingira salama ya gari lako kwa kushugurikia matatizo kabla ya mamlaka kuweza kukufikia, TSM Traffic Check ni mchumo uliotengenezwa kwa ufanisi kwa utizamaji wa deni la gali lako hauchukui hata dakika ndani ya mfumo.
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa unamaswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku