Nafasi nyingi za kazi za Mtendaji wa kijiji katika halmashauri za wilaya mbalimbali nchini Tanzania mara nyingi huitaji mwombaji aliyeweza kuhitimu angalau elimu ya kidato cha nne (form iv) au kidato cha sita (form six) aliyehitimu astashahada/cheti katika moja ya fani zifuatazo:
- Utawala
- sheria
- Elimu ya jamii
- usimamizi wa fedha
- maendeleo ya jamii na sayansi ya sanaa
kutoka chuo cha serikali za mitaa hombolo au chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.
Kama wewe ni miongoni mwa wenye sifa hizo hapo juu basi unaweza kutuma maombi pindi ajira hizo za mtendaji wa kijiji na mitaa zinapotangwazwa kupitia Halmashauri husika au kwa kutumia tovuti ya Ajira Portal. Lakini kabla hujatuma maombi yako basi ni muhimu kufahamu zaidi juu ya muundo wa uandishi wa barua ya maombi ya kazi kwa kada hiyi ya mtendaji wa kijiji na Mtaa.
Kwa kuliona hilo na kujali mahitaji ya wafuasi wetu basi ndio maana sisi Habarika24 tumeamua kukuonyesha mfano/muundo wa barua ya kuamba kazi ya mtendaji wa kijiji na mtaa.

Muundo wa Barua ya Maombi ya Kazi Mtendaji wa Kijiji na Mtaa
Barua ya kuomba kazi ndio waraka ambao mara nyingi husomwa kabla ya waraka mwingine wowote unaoambatanishwa katika kuomba kazi. Ni vyema barua hii ikaandaliwa kwa umakini, na kwa kufuata alama za kiuandishi huku ikijaribu kugusa kwa ufupi mambo yaliyoonekana kwenye wasifu binafsi.
Kuandika barua ya maombi ya kazi ni hatua muhimu sana katika mchakato wa kuomba kazi ya mtendaji wa kijiji na mtaa. Barua yako inapaswa kuwa ya kipekee, rasmi, na yenye maelezo ya kina kuhusu sifa na uzoefu wako.
Hatua za Uandishi wa Barua
Hapa chini ni muundo wa barua rasmi ya kuomba kazi katika ngazi ya Mtendaji wa Kijiji na Mtaa
1. Taarifa za Muombaji ( Anuani ya Mwandishi)
Anza barua yako kwa kuandika jina lako kamili, anuani, namba ya simu, na barua pepe. Hii itafuatiwa na tarehe ambayo unaandika barua hiyo.
2. Taarifa za Mpokeaji (Anuani ya Mwandikiwa)
Hapa hukaliwa na anuani ya mwandishi.Andika jina kamili la anayepokea barua, cheo chake, na anuani ya ofisi husika.
3. Utangulizi
Katika aya ya kwanza, taja nafasi unayoomba na jinsi ulivyogundua nafasi hiyo. Eleza kwa kifupi kwanini unafikiri wewe ni mgombea bora.
4. Sifa na Uzoefu
Toa maelezo ya kina kuhusu elimu yako, uzoefu wa kazi, na sifa nyinginezo zinazokufanya uwe mgombea bora kwa nafasi hiyo. Eleza jinsi sifa zako zinavyolingana na mahitaji ya nafasi unayoomba.
5. Hitimisho
Hitimisha barua yako kwa kueleza shukrani kwa kuzingatia ombi lako na taja kwamba uko tayari kwa mahojiano wakati wowote utakaohitajika. Weka sahihi na jina lako
Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Mtendaji wa Kijiji na Mtaa
Juma Saidi Kibwagizo
Simu; 07872377141
Dar es Salaam, Tanzania
12/06/2005
Mtendaji Mkuu wa Wilaya,
Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha,
S.L.P 30153,
Kibaha.
YAH: MAOMBI YA KAZI YA MTENDAJI WA KIJIJI/MTAA
Ndugu,
Nachukua fursa hii kuomba nafasi ya kazi ya Mtendaji wa Kijiji/Mtaa iliyotangazwa kupitia tangazo lenu la tarehe 10/06/2005 kupitia tovuti ya Ajira portal.
Nina shahada ya elimu kutoka chuo kikuu cha Dodoma niliyohitimu mwaka 2000. Nina uzoefu wa miaka 3 katika masuala ya utawala na uongozi wa jamii. Nimewahi kufanya kazi kama afisa rasilimali watu.
Ninaamini nina sifa zote zinazohitajika kwa nafasi hii, ikiwa ni pamoja na:
– Uwezo wa kuongoza na kusimamia shughuli za maendeleo ya jamii
– Ujuzi wa kutumia kompyuta na teknolojia ya habari
– Uwezo wa kufanya kazi chini ya masharti magumu
– Uwezo wa kufanya kazi bila usimamizi wa karibu
– Uzoefu katika usimamizi wa fedha na rasilimali
Ninaahidi kutumia ujuzi na uzoefu wangu kusaidia maendeleo ya jamii na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Nimeambatanisha nyaraka zifuatazo:
1. Wasifu (CV)
2. Nakala za vyeti vya elimu
3. Nakala za vyeti vya mafunzo
4. Barua za mapendekezo
5. Picha ya hivi karibuni
Nasubiri majibu yenu.
Wako mtiifu,
…………………….
Juma Saidi Kibwagizo
Simu: 07872377141
Barua pepe: [email protected]
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Ratiba ya treni za SGR Dar es Salaam na Morogoro
2. Soma Nauli za treni ya mwendokasi SGR
3. JINSI ya Kutumia Kadi Ya GUSA AzamPesa
4. Jinsi Ya Kufanya Biashara Mtandaoni
5. Jinsi Ya Kuhakiki Bima Ya Gari Lako Haraka Zaidi
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa unamaswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku