CV ya Elie Mpanzu Mchezaji Mpya wa Simba SC
CV ya Elie Mpanzu, Habari mwana Habarika24, karibu kwenye makala hii fupi itakayoenda kuangazia CV ya Elie Mpanzu mchezaji aliyesajiliwa na klabu ya wekundu wa msimbazi hivi karibuni kama winga wa kulia ili kuimalisha kikosi cha Simba SC kwenye msimu huu wa ligi kuu ya NBC Premier Leuge 2024/2025.
Simba SC klabu imefanya usajili wa winga wa kulia mwenyeji wa nchi ya Congo Elie Mpanzu ikiwa ni miongoni mwa mikakati yake ya kuendelea kukitengeneza kikosi chake ili kujiakikishia ushindi kutoka kwa mabingwa watetezi wa kombe la ligi kuu ya NBC Yanga Africans.
Simba SC ni miongoni mwa klabu kubwa katika ulimwengu wa soka nchini Tanzania, Afrika Mashariki na Kati na Afrika kwa ujumla wake, Hivi karibuni imemtambulisha mchezji mwenye uraia wa Dr Congo kama mchezaji wake katika nafasi ya winga wa kulia akitokea katika klabu ya AS Vita ya mjini Kinshasa.
Usajili wa Mkongo Elie Mpanzu katika klabu ya Simba umekuja ikiwa ni miongoni mwa mipango ya klabu ya mwekundu wa msimbazi katika kukijenga na kukiimalisha kikosi chake kwenye msimu huu mpya wa ligi kuu ya NBC baada ya kupoteza ubigwa wa ligi hiyo msimu nuliopita dhidi ya wapinzani wao klabu ya Yanga.
CV ya Elie Mpanzu

Hapa tutaenda kuangazia kwa ufupi zidi kuhusu CV ya Elie Mpanzu kama mchezaji mpya wa klabu ya Simba.
CV ya Elie Mpanzu | |
Jina | Elie Mpanzu Kibisawala |
Taifa | Kongo DR |
Tarehe ya kuzaliwa | 1, Januari 2002 |
Umri | Miaka 22 |
Nchi Aliyozaliwa | Kongo DR |
Mahali Alipozaliwa | Kinshasa |
Nafasi Uwanjani | Winga wa Kulia |
Urefu | 165 Cm |
Uzito | 65 Kg |
Mguu Uwanjani | Kulia |
Klabu Aliyotoka | AS Vita |
Klabu ya Sasa | Simba CS |
Elie Mpanzu na Katika Ulimwengu wa Soka
Elie Mpanzu ni raia wa nchi ya Kongo DR, Safari yake kama winga wa kulia katika soka ilianza kutoa matumaini na kumfanya mchezaji bora katika nchi ya Kongo pale alipojiunga na klabu ya AS Vita na kuwa mchezaji hatari anapokua uwanjani.
Umaarufu wake akiwa na klabu ya AS Vita aliyo jiunga nayo mnamo mwaka 2022 ndio iliuliofungua milango ya mafanikio katika keria yake ya soka hadi kufikia kutazamwa na baadh ya klabu kubwa balani Afrika ikiwemo klabu ya Simba Sc. Na kutokana na uwezo wake mwaka 2024 Elia Mpanzu alifanikiwa kujiunga na klabu ya wekundu wa msimbazi Simba ya Tanzania
Simba Na Usajili wa Elie Mpanzu
Klabu ya Simba inayoshiriki ligi kuu ya NBC msimu huu mpya wa 2024 na michuano ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF, imefanya usajiri wa winga huyo kutokea AS Vita ya Kongo ikiwa ni moja ya mikakati yake ya kuboresha kikosi chake ili kuhakikisha ushidi wa ligi mbali mbali.Simba inategemea kupata huduma ya winga huyo ambaye ilimsajili kwa dola 200,000.
Elie Mpasu anajiunga na klabu ya Simba ya Tanzania kama winga akienda kuungana na wachezaji wengine waliosajiliwa na klabu hiyo ambao wakicheza nafasi sawa na ya Elia Mpanzu kama vile Joshua Mutale, Edwin Balua, Ladack Chasambi, na Salehe Karabaka.
Uwezo wa Elie Mpanzu Akiwa Uwanjani
Elie Mpnzu ni mchezaji mwenye uwezo wa juu sana kwa nafasi anayoichezea hasa winga ya kulia, ukiachilia mbali urefu wake wa kimo cha 165 Cm bado amekua msumbufu sana katika eneo la ushambuliaji na mchezaji mwenye kuleta matokeo chanya awapo uwanjani na hii ndio sababu kuu ya klabu kubwa kama Simba kuweza kumsajili
Simba SC na washabiki zake wategemee makubwa kutoka kwa mchezaji huyu kwani madhara yake akiwa uwanjani ni mkubwa sana.
Hitimisho
Simba SC haikufanya makosa kwenye usajili wa nyota huyu anayehudumu katika nafasi ya winga akiwa uwanjani, kama sehemu ya klabu ya Simba katika kutengeneza kikosi chake msimu huu wa ligi kuu ya NBC 2024 basi Ele Mpanzu ni miongoni mwa sajili sahihi kabisa.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Ratiba ya Mechi Za Leo Ligi Mbali Mbali Duniani Jumapili