CAF Yabadilisha Refa Mechi ya Stellenbosch vs Simba
Kuelekea mchezo wa nusu fainali kombe la shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup Semi Final) duru ya pili kati ya Stellenbosch vs Simba Sc Shirikisho la mpira wa miguu barani Africa CAF limeamua kufanya mabadiliko ya ghafla ya refa aliyekua amepangiwa hapo awali kuchezesha mchezo huo siku ya Jumapili 27 April 2025.
Apo awali refa aliyekua amepangwa kuchezesha mchezo huo alikua ni Amin Omar kutokea nchini Misri,Mabadiliko yaliyifanywa na CAF sasa mchezo huo utachezeshwa na refa Mohamed Maarouf Eid Mansour kutokea huko huko nchini Misri.
Hadi sasa bado haijafahamika sababu za kimsingi za CAF kufanya mabadiliko hayo ni ipi.Ikumbukwe kua kocha Amin Omar ndiye kocha aliyechezesha mchezo kati ya Simba Sc dhidi ya Oroya na katika mchezo huo wa hatua ya makundi Simba akiwa ungenini alipoteza kwa kufungwa goli 1-0 katika ligi ya mabingwa Afrika msimu wa 2023/2024.