Aina Za Majeshi Tanzania
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Aina Za Majeshi Tanzania, Majeshi ya Tanzania, Habari mwana Habarika24, karibu katika makala hii amabyo itaenda kuangazia aina za majeshi ya Tanzania. Kama ulikua na shahuku ya kutaka kujua kuna aina ngapi za majeshi nchini Tanzania basi katika makala hii fupi unaenda kufayafahamu kwa idadi na majina yake.
Aina za Majeshi Tanzania
kwa ujumla kuna aina kuu nne za majeshi nchini Tanzania ambayo ni
- – Jeshi la Polisi la Tanzania
- – Jeshi la Wanamaji
- – Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
- – Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
Aina hizo kuu nne za majeshi ya majeshi yanayopatika Tanzania kila jeshi linamajukumu yake na uongozi wake.
Aina za Majeshi Tanzania na Kazi zake
1. Jeshi la Polisi Tanzania
Hili ndio jeshi linalowajibika na kulinda raia na mali zao, Kazi kuu katika taifa ni kuhakikisha kubaini, kuzuia na kudhibiti uhalifu ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jeshi la Polisi la Tanzania lilianzishwa rasmi 25 August 1919 kwa tangazo la Serikaliya Kiingereza lililotoka Gazeti la Serikali No.Vol.1 No.21-2583 kwa wakati huo likaitwa Jeshi la Polisi Tanganyika
Majikumu ya Msingi ya Jeshi la Polisi Tanzania
- Majukumu ya kimsingi ya jeshi la polisi ni kuchunguza, kubaini na kuzuia aina yoyote ya uharifu
- Kuhakikisha usalama wa Raia na mali zao.
- Kudumisha amani katika jamii
2. Jeshi la Wanamaji
Jeshi la wanamaji ni kitengo maalumu cha kijeshi kinachshugulikia ulinzani na usalama wa nchi kutokea baharini, Jeshi hili linajumlisha askari, manowari na meli za kuasaidia manowari, mabandari ya pekee na vituo vingine. Jeshi hili lilianzishwa mnamo mwaka 1970
Majukumu ya Jeshi la Wanamaji
Majukumu ya msingi ya jeshi la wanamaji ni pamoja na
- Kuhakikisha usalama wa Bahari
- Kulinda nchi kutoka kwa wavamizi wa baharini
- Kuhakikisha amani na utulivu kwa watumiaji wa bahari
- Kulinda mipaka ya nchi kutokea baharini
- Kuhakikisha doria na oparesheni za baharini
3. Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
JKT ilianzishwa mwaka 1958 wakati wa ziara ya viongozi wa Taifa nchini Ghana, ambapo Baba wa Taifa Mwl. Nyerere na Mhe. Rashid Kawawa (Simba wa Vita) walikwenda kuhudhuria sherehe za kuadhimisha mwaka mmoja wa uhuru wa nchi hiyo.
Mjuku ya Jeshi la Kujenga Taifa
Malezi ya Vijana
- Vijana kufundishwa moyo wa kupendana bila kujali tofauti za itikadi, dini, kabila na kipato.
- Kupenda kazi za mikono.
- Kuthamini na kuendeleza mila, desturi na kudumisha utamaduni wa Taifa.
- Kuwa raia wema, wanaojiamini, wanaojituma, wenye uzalendo na kuipenda nchi yao.
Ulinzi wa Taifa
- Kuwapa vijana mbinu za kijeshi wawe Jeshi la akiba, kuwaandaa vijana watakaofaa kujiunga na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.
- Kuwaandaa vijana kusaidia katika majanga mbalimbali, mfano mafuriko, moto na ajali mbali mbali.
Uzalishaji Mali
- Ili kuwafanya vijana wa kitanzania waepukane na kusumba kuwa kazi za ofisini ndio njia pekee na bora inayomuwezesha mtu kuishi, JKT linahusika na uzalishaji mali kwa lengo la kuwawezesha vijana kujiajiri katika sekta mbali mbali mara baada ya kumaliza mkataba na JKT. Uzalishaji mali unaofanywa na JKT ni pamoja na:-
- Kujenga na kukarabati majengo
- Viwanda na Kilimo
- Madini na Nishati
- Utalii
- Ulinzi kwa Taasisi binafsi (Security Guard Services)
- Maduka (Super Market)
- Kuunganisha magari na mitambo
- Huduma za elimu
4. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania – JWTZ lilianzishwa mnamo mwaka 1964 likiwa na jukumu kuu la kulinda na kumalisha usalama wa mipaka ya nchi
Majukumu ya Msingi ya JWTZ
Jeshi la JWTZ linamakumu ya msingi kama vile
- kulinda mipaka ya nchi
- Kuimalisha usalama wa ndani wa nchi
- kusaidia majeshi mengine kutunza amani ya nchi
JWTZ ni jeshi kuu la nchi, lililoanzishwa mwaka 1964. Lina jukumu la kulinda mipaka ya nchi na kuimarisha usalama wa ndani. JWTZ inajumuisha vikosi vya ardhini, majini, na angani. Jeshi hili linafanya mazoezi ya kijeshi na kushiriki katika operesheni za kimataifa za amani.
Vikosi vya Majeshi ndani ya Jeshi la JWTZ
- Ardhini
- Majini
- Angani
Hitimisho
Nchini Tanzania kuna aina nyngi sana za majeshi lakini hapa tumeweza kukuwekea aina kuu nne za majeshi, majeshi haya na mengine yanashirikiana kwa pamoja kuhakikisha ulinzi na usalaama wa nchi unakuwepo kwa juhudi na gharama za aian yoyote ile.
Kwa maelezo zaidi unaweza tembelea
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Orodha ya Kambi za JKT Tanzania
2. Vigezo na Sifa za Kujiunga JKT Mujibu Wa Sheria
3. Fomu ya Kujiunga na Usalama Wa Taifa Tanzania
4. Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Usalama Wa Taifa Tanzania
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku