Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Utalii Arusha
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Utalii Arusha, Habari ya wakati huu mwana Habarika24, karibu tena katika makala hii fupi ambayo kwa kina iatemda kukupa maelezo ya kutosha kuhusu Ada, Fomu, kozi na sifa za kujiunga na chuo cha utalii Arusha.
Kama wewe ni miongoni mwa wanaohitaji kujiunga na chuo cha utalii kampasi ya Arusha basi jua makala hii ni ya muhimu sana kwa upande wako kwani itaenda kukupa maelezo ya kutosha ya wewe kuweza kujiunga na chuo hiki.Kampasi hii ya chuo cha utalii Arusha ni moja miongoni mwa kampasi zilizoanzishwa na chuo cha taifa cha utalii (NCT). Chuo hiki kinatoa kozi katika ngazi ya cheti na Diploma.
Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Utalii Arusha
Kuhusu Chuo Cha Utalii Arusha
Chuo cha Taifa cha Utalii – Kampasi ya Arusha kilianzishwa mwaka 1993 na taasisi ya madhara ya Seidel Foundation ya Munich Ujerumani na Halmashauri ya Manispaa ya Arusha kwa lengo la kutoa ujuzi stahiki wa ufundi stadi kwa wanafunzi ambao wangependa kutafuta taaluma katika tasnia ya hoteli. Chuo kimechukuliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii tarehe 4 Julai 2008 kama sehemu ya Chuo chake cha Taifa cha Utalii.
Chuo cha utalii Arusha kiko katika ukanda wa kaskazini ambapo mahitaji ya huduma za utalii ni ya juu sana ambayo yaliongeza mahitaji ya wafanyikazi waliohitimu. Hivi sasa, chuo kinatoa kozi za ukarimu katika ngazi ya cheti. Miundombinu iliyopo ina uwezo wa kuchukua hadi wanafunzi 150 kila mwaka.
Kozi Zitolewazo na Chuo cha Utalii Arusha
Hapa tuanenda kuangazia kuangazia kozi zinazotolewa na chuo cha utalii kampasi ya Arusha kwa level za NTA level 4 na NTA level 5
- Uendeshaji wa Utalii kwa ngazi ya Cheti (NTA Level 4)
- Uendeshaji wa Utalii kwa ngazi ya Diploma (NTA Level 5)
- Ukarimu kwa ngazi ya Cheti (NTA Level 4)
- Ukarimu kwa ngazi ya Diploma (NTA Level 5)
Ada za Chuo cha Utalii Arusha katika Kozi Mbali Mbali
Hapa tunaenda kuangalia ada zinazotozwa kwa kozi zinazotolewa na chuo cha utalii Arusha katika kozi ya cheti(NTA level 4) na kozi ya cheti (NTA level 5)
Ada ya Kozi ya Uendeshaji Utalii Cheti (NTA Level 4) Katika Chuo cha Utalii Arusha
- Ada ya Masomo ni Tsh 1,200,000 kwa mwaka
Ada ya Kozi ya Ukarimu Cheti (NTA Level 5) katika Chuo cha Utalii Arusha
- Ada ya Masomo – TZS 1,200,000 kwa mwaka
Ada ya Kozi ya Uendeshaji Utalii Diploma (NTA Level 5) Katika Chuo Cha Utalii Arusha
- Ada ya Masomo – TZS 1,500,000 kwa mwaka
Ada ya Kozi ya Ukarimu Diploma (NTA Level 5) Katika Chuo Cha Utalii Arusha
- Ada ya Masomo – TZS 1,500,000 kwa mwaka
Fomu ya Kujiunga Na Chuo Cha Utalii Kampasi ya Arusha
ili kujiunga na chuo cha utalii kampasi ya Arusha unahitajika kujaza fomu ya maombi na fomu ya maombi ya kujiunga na chuo cha utalii Arusha kunania mbili za kupata fomu hiyo ambazo ni;
1. Unaweza kupata fomu ya kujiunga na chuo cha utalii kupitia tovuti ya chuo – nct.ac.tz- Arusha
2. Njia ya pili ni kwenda moja kwa moja kwenye ofisi za chuo cha utalii kampasi ya Arusha.
Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Utalii Arusha
Ili kujiunga na chuo cha utalii Arusha lazima mwanafunzi anatakiwa awe na sifa na vigezo maalumu kulingana na ngazi ya kozi unayotaka kusoma.
Sifa za Kujiunga na Kozi za Cheti (NTA Level 4)
Ili kujiunga na kozi za cheti kwa NTA level 4 basi mwanafunzi anapaswa kua na sifa zifuatazo;
- Wanafunzi awe amehitimu kidato cha Nne (CSEE) na ufaulu wa alama D nne na kuendelea
- Au awe na cheti cha VETA katika fani husika
Sifa za kujiunga na Kozi za Diploma (NTA Level 5)
Kwa wanafunzi wanaotarajia kuikunga na kozi za diploma kwa level ya NTA level 5 lazima awe na sifa na vigezo vifuatavyo;
- Awe amehitimu kidato cha Sita (ACSEE) na ufaulu wa alama E mbili na kuendelea.
- Au awe na cheti cha NTA Level 4 katika fani husika.
Hitimisho
Chuo cha utalii Arusha ni miongoni mwa kampasi za za chuo cha utalii Tanzania (NCT) na nichuo bora kwa utoaji wa kozi za utalii kama vile uendeshaji wa utalii na ukarimu kwa ngazi ya cheti na diploma level za NTA level 4 na level 5.
Hkikisha kama unahitaji kujiunga na moja ya kozi zitolewazo na chuo hiki uwe unasifa na vigezo vya kozi husika.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Utalii Dar es Salaam
2. Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Utalii Temeke
3. Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Utalii Mwanza
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku