Wachezaji wanaolipwa pesa nyingi Tanzania 2025, Katika dunia ya michezo Tanzania, vipaji vinaendelea kuvuma na kuvutia dau kubwa la mishahara. Mwaka 2025 umeleta sura mpya kwa wachezaji wanaolipwa fedha nyingi zaidi, huku soka likibaki kuwa mchezo unaolipa zaidi, lakini pia michezo kama netiboli na riadha ikianza kuchangia listi hii.
Kama unashahuku ya kutaka kujia ni wachezaji gani na wanatoka klabu gani wanalipwa pesa ndefu zaidi kwenye ligi kuu ya NBC basi makala hii itakupa kila kitu unachotamani kukifahamu kwa msimu wa 2025.
Ligi kuu ya NBC imekua ni miongoni mwa ligi bora zaidi Afrika mashariki na Afrika kwa ujumnla wake kwani kwenye ubora wa viwango vya CAF ligi ya Tanzania (NBC Premier League) inashika nafasi ya 5 kwa ubora barani Afrika.
Hii ni kutokana na uwekezaji unaofanywa katika klabu zinazoshiriki katika ligi hiyo. Mfano kwa klabu kama Yanga, Simba na Azam wamewekeza pesa nyingi sana katika vilabu vyao na hivyo kuwavutia wachezaji wengi wazuri wa kimataifa kwa kuwalipa vizuri. Wamekua wakitoa mishahara mizuri kwa wachezaji hivyo kufanya wachezaji wenye uwezo mkubwa kutamani kucheza katika ligi hii.
Kwa mujibu wa chanzo chetu hii ni orodha ya Wachezaji 10 wanaolipwa Mishahara mikubwa Ligi Kuu ya NBC.
Wachezaji wanaolipwa pesa nyingi Tanzania 2025
1. Stephane Aziz Ki (Yanga SC) – TSh 32 Milioni
2. Feisal Salum (Azam FC) – TSh 27 Milioni
3. Clatous Chama (Yanga SC) – TSh 25 Milioni
4. Fabrice Ngoma (Simba SC) – TSh 24 Milioni
5. Pacôme Zouzoua (Yanga SC) – TSh 22 Milioni
6. Alassane Diao (Azam FC) – TSh 20 Milioni
7. Leonel Ateba (Simba SC) – TSh 20 Milioni
8. Ayoub Lakred (Simba SC) – TSh 19 Milioni
9. Prince Dube (Yanga SC) – TSh 19 Milioni
10. Mohamed Hussein (Simba SC) – TSh 18 Milioni
Orodha ya Wachezaji Wengine Wanaolipwa Mishahara Mizuri zaidi Tanzania
Ukiachilia mbali wachezaji wa nne tuliowaweka kwenye orodha hapo juu pia katika ligi ya NBC kuna wachezaji wengine wengi tu wanaolipwa pesa nyingi zaidi kama mishahara yao kutokana na vipaji vyao vya uchezaji.
Hapa chini ni orodha ya wachezaji wengine wanaolipwa pesa nyingi zaidi katika klabu zao
- Luis Miquisone
- Pacome Zouzoua
- Saidoo Ntibanzokiza
- Henock Inonga
- Fabrice Ngoma
- Djigui Diarra
- Ayoub Lakred
- Kibu Denis
- Maxi Mzengeli
Ukiangalia vizuri kutoka kwenye orodha hiyo hapo juu utaona kua vilabu kama Simba SC, Yanga SC na Azam FC ndio vinavyo ongoza kwa kulipa mishahara mizuri zaidi kwa wachezaji wake huku ligi kuu ya NBC ikiwa na ushiriki wa timu 16.
Soma Pia;