Mkuu wa Jeshi la Polisi anawatangazia vijana walioomba ajira ya Jeshi la Polisi kupitia mfumo wa Ajira (TANZANIA POLICE FORCE – RECRUITMENT PORTAL) kuwa usaili utafanyika kuanzia tarehe 28/4/2025 saa 07:00 Asubuhi hadi tarehe 11/5/2025 kote nchini.
Vituo vya Usaili kwa Wasailiwa wa ajira za Jeshi la Polisi vimetengwa kulindana na ngazi za elimu na kufuata maeneo wa waombaji wa Ajira hizo za Polisi kwa mwaka wa ajira wa 2025.
Vituo Vya Usaili Ajira za Jeshi la Polisi 2025
Hapa chini ni vituo vya usaili kwa waombaji walioitwa kwenye usaili jeshi la polisi kwa mwaka 2025. Soma kwa makini kwani vituo vya usaili vimetengwa kulingana na Elimu ya wasailiwa pamoja na maeneo waliotuma maombi.
1. Wasailiwa wenye elimu ya Shahada, Stashahada na Astashahada
- kwa Upande wa Tanzania bara: wasailiwa wenye elimu ya Shahada, Stashahada na Astashahada usaili utafanyika jijini Dar es Salaam katika uwanja wa gwaride uliopo Kambi ya Polisi (Police Barracks) barabara ya Kilwa nyuma ya kituo cha Polisi Kilwa
Road. - Kwa upande wa Zanzibar: Wasailiwa wa Zanzibar wenye elimu ya Shahada, Stashahada, Astashahada usaili utafanyika Zanzibar
- Wasaili waliopo mikoa ya Unguja-usaili utafanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani)
- Wasaili walioko Mikoa ya Pemba – usaili utafanyika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba (Chakechake).
Soma Pia; Mambo Muhimu ya Kuzingatia Kwenye Usaili Ajira za Polisi
2. Wasailiwa wenye elimu ya kidato cha Nne na cha Sita
- kwa Upande wa Tanzania bara: usaili utafanyika kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa waliyoichagua wakati wa kutuma maombi.
- Kwa upande wa Zanzibar: Wasailiwa wa Zanzibar wenye elimu ya Kidato cha sita na Nne usaili utafanyika Zanzibar
- Wasaili waliopo mikoa ya Unguja-usaili utafanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani)
- Wasaili walioko Mikoa ya Pemba – usaili utafanyika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba (Chakechake).
BOFYA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA MAJINA WALIOITWA KWENYE USAILI AJIRA ZA JESHI LA POLISI 2025