Form Five Selections ni mchakato wa uteuzi wa wanafunzi waliomaliza mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na kufanikiwa kujiunga na Kidato cha Tano katika shule mbalimbali za sekondari nchini Tanzania. Kupitia makala hii, tunakuletea taarifa kamili, sahihi na za kina kuhusu waliochaguliwa kujiunga na Kidato Tano mwaka 2025, jinsi ya kuangalia majina ya waliochaguliwa, pamoja na hatua muhimu unazopaswa kuchukua endapo umechaguliwa.
BOFYA HAPA KUPATA MATOKEO YA UCHAGUZI MAPEMA
TAMISEMI ni Nini na Jukumu lake kwenye Uchaguzi wa Kidato Tano?
TAMISEMI ni kifupi cha Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, taasisi ya serikali inayosimamia usimamizi wa elimu ya sekondari kwa kushirikiana na NECTA na wizara ya elimu. Moja ya majukumu makuu ya TAMISEMI ni kuratibu na kutangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano kila mwaka kwa kuzingatia ufaulu, ushindani wa tahasusi, na nafasi zilizopo katika shule mbalimbali.
Lini Majina ya Waliochaguliwa Kidato Tano 2025/2026 Yatatangazwa?
Kwa kawaida, TAMISEMI hutangaza majina ya wanafunzi waliopangiwa Kidato cha Tano miezi michache baada ya matokeo ya Kidato cha Nne kutangazwa. Kwa mwaka huu wa 2025, tunatarajia majina ya Form Five kuanza kutangazwa mwezi wa Mei au mapema Juni 2025. Ni muhimu kufuatilia tovuti rasmi ya TAMISEMI mara kwa mara.
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Kidato Tano 2025/2026
BOFYA HAPA KUPATA MATOKEO YA UCHAGUZI MAPEMA
Hapa chini ni hatua kwa hatua jinsi ya kuangalia majina ya waliochaguliwa Kidato Tano kupitia tovuti ya TAMISEMI:
Fungua tovuti ya TAMISEMI: Nenda kwenye https://selform.tamisemi.go.tz
Bonyeza sehemu ya “CHOOSE SELECTION VERSION” kutoka kwenye orodha chagua mwaka 2025”
Chagua Mkoa na kisha Wilaya yako
Tafuta shule yako ya sekondari ya uliohitimu
Angalia jina lako kwenye orodha ya waliochaguliwa
Pia, unaweza kutumia namba yako ya mtihani (CSEE Index Number) kutafuta kwa haraka.
ARUSHA | DAR ES SALAAM | DODOMA |
GEITA | IRINGA | KAGERA |
KATAVI | KIGOMA | KILIMANJARO |
LINDI | MANYARA | MARA |
MBEYA | MOROGORO | MTWARA |
MWANZA | NJOMBE | PWANI |
RUKWA | RUVUMA | SHINYANGA |
SIMIYU | SINGIDA | SONGWE |
TABORA | TANGA |
BOFYA HAPA KUPATA MATOKEO YA UCHAGUZI MAPEMA
Kitu cha Kufanya Baada ya Kuchaguliwa Kidato Tano
Iwapo umechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, ni muhimu kuchukua hatua zifuatazo mapema:
Pakua barua ya wito (Joining Instructions) kutoka tovuti ya TAMISEMI au ya shule husika.
Fanya maandalizi ya vifaa vya shule, ada na mahitaji mengine ya msingi.
Hakikisha unawasili shuleni kwa tarehe iliyoainishwa kwenye barua ya wito.
Kwa wale waliokosa nafasi, kuna nafasi ya kuomba kupitia awamu ya pili (second selection) au kujiunga na vyuo vya kati (VETA, NACTE, nk).
Orodha ya Shule Maarufu za Kidato cha Tano Tanzania
Kwa wanafunzi waliopata alama za juu, mara nyingi hupangiwa kwenye shule zifuatazo:
Ilboru Secondary School – Arusha
Mzumbe Secondary – Morogoro
Tabora Boys – Tabora
Kibaha Secondary – Pwani
Kilakala Girls – Morogoro
Mwanza Secondary – Mwanza
Shule hizi hutoa tahasusi mbalimbali kama PCM, PCB, EGM, HGL, CBG, HGE, na nyinginezo kulingana na matokeo ya mwanafunzi.
Tahasusi Zinazopendwa Zaidi Kidato cha Tano
Wanafunzi wengi hupendelea tahasusi zifuatazo:
PCM (Physics, Chemistry, Mathematics) – Kwa wanaotaka kuwa wahandisi
PCB (Physics, Chemistry, Biology) – Kwa wanaotaka kuwa madaktari
EGM (Economics, Geography, Mathematics) – Kwa wanaotaka masomo ya biashara
HGL (History, Geography, Language) – Kwa wanaotaka kuwa wanataaluma wa jamii
Chagua tahasusi kulingana na uwezo wako, matokeo yako, na ndoto zako za baadaye.
Uhamisho au Mabadiliko ya Shule Kidato cha Tano
Iwapo mwanafunzi hataridhika na shule aliyopangiwa, anaweza kuomba uhamisho wa shule kwa njia rasmi, mara tu baada ya kuripoti shuleni alikopangiwa awali. Hata hivyo, mchakato huu unategemea nafasi katika shule unayotaka kuhamia na sababu za msingi.