Nafasi 6 za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa March 2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa amepokea kibali cha Ajira mpya kwa Ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu – Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024. Hivyo, watanzania wote wenye sifa na uwezo wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kujaza nafasi zifuatazo:
MSAIDIZI WA MAENDELEO YA JAMII DARAJA LA II – NAFASI 06
KAZI NA MAJUKUMU
i) Kuratibu shughuli zote za Maendeleo ya Jamii kwa kuzingatia Jinsia.
ii) Kuraghabisha jamii kuanzia ngazi ya familia katika kubuni, kupanga, kutekeleza, kusimamia na kutathimini mipango na au mradi yao ya maendeleo.
iii) Kuhamasisha kuondokana na mila/desturi potofu na kuwa na mtazamo wa kupenda mabadiliko.
iv) Kutoa taarifa za utekelezaji wa kazi zake kila mwezi.
v) Kuelimisha jamii juu ya kutekeleza masuala ya kijinsia.
vi) Kuhamasisha jamii kutumia teknolojia sahihi na rahisi.
vii) Kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kutoa taarifa za matukio mbalimbali kama vifo, milipuko ya magonjwa, masoko, uzalishaji mali, vyakula, ajira na unyanyasaji wa kijinsia.
viii) Kuhamasisha jamii kujiunga na Elimu ya Watu Wazima.
ix) Kuelimisha jamii kuhusu masuala ya Watoto.
x) Kukusanya, kuchambua na kuweka takwimu zinazozingatia jinsia zitakazowezesha jamii kupanga mipango yao.
xi) Atafanya kazi nyingine za fani yake kama atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na Cheti cha kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo; Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS B
Bonyeza HAPA kupakua Tangazo Kamili
Kwa matangazo ya Ajira Mpya kila Siku Bonyeza HAPA