Ratiba Ya Hatua ya Mtoano Ligi ya Mabingwa Ulaya 2024/2025
Ligi ya Mabingwa Ulaya 2024/2025 imefikia hatua ya mtoano, ambapo timu bora zaidi barani Ulaya zinachuana kuwania taji la kifahari. Msimu huu unashuhudia mabadiliko makubwa katika muundo wa mashindano, huku hatua ya makundi ikibadilishwa na kuwa ligi moja yenye timu 36. Timu hizi zinacheza mechi nane dhidi ya wapinzani tofauti, nne nyumbani na nne ugenini. Baada ya hatua hii, timu nane za juu zinafuzu moja kwa moja kwa hatua ya 16 bora, huku timu zilizoshika nafasi ya 9 hadi 24 zikicheza mtoano ili kuingia hatua ya 16 bora.
Timu zilizofuzu Hatua ya Mtoano Ligi ya Mabingwa Ulaya
Baada ya kumalizika kwa hatua ya ligi timu zilizomaliza kwenye msimamo wa namba 9 hadi 24 zimeingia hatua ya mtoano ili kutafuta timu 8 zitakazoweza kuungana na zile zilizofizu moja kwa moja kwenye hatua ya 16 bora. Hapa chini ni timu zilizoingia kwneye hatua ya mtoano ligi ya mabingwa ulaya.
- Lille
- Aston Villa
- Atalanta
- Bayern Munich
- Real Madrid
- AC Milan
- Juventus
- Manchester City
- PSV
- Benfica
- Monaco
- Feyenoord
- Brest
- Sporting
- Celtic
- Club Brugge
Ratiba ya Hatua ya Mtoano
Hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2024/2025 inaanza mwezi Februari 2025 na itaendelea hadi Mei 2025, ikihitimishwa na fainali itakayofanyika tarehe 31 Mei 2025 katika Uwanja wa Soka wa Munich, Ujerumani.
February 1o
- Brest vs PSG
- Juventus vs PSV
- Manchester City vs Real Madrid
- Sporting vs Borussia Dortmund
February 12
- Celtic vs Bayern Munich – 23:00
- Club Brugge vs Atalanta – 23:00
- Feyenoord vs AC Milan – 23:00
- Monaco vs Benfica – 23:00
February 18
- AC Milan vs Feyenoord – 20:45
- Atalanta vs Club Brugge – 20:45
- Bayern Munich vs Celtic – 23:00
- Benfica vs Monaco – 23:00
February 19
- Borussia Dortmund vs Sporting – 20:45
- PSG vs Brest – 23:00
- PSV vs Juventus – 23:00
- Real Madrid vs Manchester City – 23:00
Mzunguko wa Mtoano wa Awali
Mechi za mtoano wa awali zitafanyika tarehe 11/12 na 18/19 Februari 2025. Timu zilizoshika nafasi ya 9 hadi 24 katika hatua ya ligi zitachuana ili kupata nafasi ya kuingia hatua ya 16 bora. Ratiba kamili ya mechi hizi itatangazwa baada ya droo inayotarajiwa kufanyika tarehe 31 Januari 2025.
Hatua ya 16 Bora
Hatua ya 16 bora itaanza tarehe 4/5 na 11/12 Machi 2025. Timu nane zilizoshika nafasi za juu katika hatua ya ligi zitakutana na washindi wa mtoano wa awali. Droo ya kupanga mechi hizi itafanyika tarehe 21 Februari 2025.
Robo Fainali
Robo fainali zitachezwa tarehe 8/9 na 15/16 Aprili 2025. Timu nane zitakazofuzu kutoka hatua ya 16 bora zitachuana katika mechi za nyumbani na ugenini ili kupata nafasi ya kuingia nusu fainali. Droo ya kupanga mechi hizi pia itafanyika tarehe 21 Februari 2025.
Nusu Fainali
Nusu fainali zitafanyika tarehe 29/30 Aprili na 6/7 Mei 2025. Washindi wa robo fainali watakutana katika mechi mbili, nyumbani na ugenini, ili kuamua ni timu zipi zitakazofuzu kwa fainali.
Fainali
Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2024/2025 itafanyika tarehe 31 Mei 2025 katika Uwanja wa Soka wa Munich, Ujerumani. Huu utakuwa ni msimu wa kwanza kwa uwanja huu wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 67,000 kuandaa fainali ya Ligi ya Mabingwa tangu mwaka 2012.
Hitimisho
Msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya 2024/2025 unatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na mabadiliko ya muundo wa mashindano na ubora wa timu zinazoshiriki. Mashabiki wa soka kote ulimwenguni wanatarajia mechi za kusisimua katika hatua ya mtoano, huku kila timu ikipania kutwaa taji hili la heshima.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Msimamo Wa Ligi Kuu ya NBC 2024/2025 Tanzania Bara
2. Msimamo wa NBC Championship Tanzania 2024/2025
3. Ratiba ya Mechi Za Leo Ligi Mbalimbali