Walioitwa Kazini Banki Kuu ya Tanzania February 2025
Naibu Gavana Utawala na Udhibiti wa Ndani wa Benki Kuu ya Tanzania anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili wa kuandika/mchujo (Aptitude Test) unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 15-02-2025 hadi 24-03-2025.
Wasailiwa watakaofuzu usaili huu na kwenda katika hatua zinazofuata watatakiwa kushiriki katika usaili wa vitendo au/na mahojiano kwa tarehe iliyoanishwa au kama watakavyotaarifiwa kwa wakati husika. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wa kuandika/mchujo (Aptitude Test) wanapaswa kuzingatia maelekezo
yafuatayo:-
1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
2. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
3. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji/shehia anakotoka msailiwa.
4. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na vyeti vingine (kutegemeana na nafasi aliyoomba).
5. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
6. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
7. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
8. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTVET au NECTA)
9. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
10. Wasailiwa wa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
11. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.
12. MUHIMU: Wasailiwa watakao shindwa kuwasilisha nyaraka zilizokamilika kama zilivyoainishwa katika kipengele na. 2, 3, 4, 8 na 10 hawataruhusiwa kuendelea na usaili.
Bonyeza HAPA Kudowbload PDF File
Mapendekeo Ya Mhariri;
1. CV ya Miloud Hamdi Kocha Mpya wa Yanga
2. WAFUNGAJI Bora Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania 2024/2025
3. Wafungaji Bora Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2024/2025