Mechi ya Yanga Vs Kagera Suger leo 01/02/2025 Saa Ngapi?
Kama ni miongoni mwa watu wanaojiuliza kuhusu juu ya saa ngapi mechi ya Yanga na Kagera Sugar itacheza wakati gani siku ya Jumamosi, basi hapa katika kurasa hii utaenda kukupa mwongozo kamili wa mchezo huu wa kiporo ligi kuu ya NBC 2024/2025.
Baada ya kusimama kwa ligi kuu ya NBC weekend hii itarejea tena kwa kuanza na mechi za viporo vya mzunguko wa kwanza. Siku ya Jumamosi ya tarehe 02/02/2025 klabu ya Yanga watakua wenyeji dhidi ya Kagera Sugar mchezo utakaofanyika katika viunga vya mwenge jijini Dar es Salaam katika uwanja wa KMC Complex majira ya saa 10:00 za jioni.
Kipengele | Maelezo |
---|---|
Timu Zinazocheza | Yanga vs Kagera Sugar |
Tarehe | 02 February 2025 |
Muda | Saa 10: 00 jioni |
Uwanja | Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam |
Mashindano | NBC Premier League |
Matangazo | @azamtvsports |
Tathimi ya Mchezo
Klabu ya Yanga inaingia uwanjani siku ya jumamosi ikiwa imetolewa kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika, nguvu na jitihada za wachezaji wa klabu hiyo zinaelekezwa katika michezo ya ligi kuu ya NBC huku akiitaji kutete ubingwa wake. Hadi sasa Yanga ipo kwenye nafasi ya 2 ikiwa na jumla ya pointi 39 pointi moja nyuma ya klabu ya wekundu wa msimbazi Simba SC.
Mchezo uliopita uliofanyika
kwenye mchezo wa kwanza uliofanyikia Agost 29, 2025, mkoani Kangera Yanga iliibuka na ushindi wa goli 2 kwa sifuri, mchezo huu wa leo ni mchezo wa kutamatisha mechi ya mzunguko wa kwanza kabla ya kuanza kwa mzunguko wa 2 wa ligi kuu ya NBC Tanzania bara kwa msimu wa 2024/2025.
Kwa maelezo zaidi kuhusu mechi hii, unaweza kutembelea Azam TV Sports kwa matangazo ya moja kwa moja na uchambuzi wa kitaalamu.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Vituo Vya Kununua Tiketi Mechi ya Yanga Vs Kagera Suger 01/02/2025
2. Viingilio Mechi ya Yanga vs Kagera Suger 01 February 2025
3. Tabora Utd vs Simba Sc Leo 2/02/2025 Saa Ngapi?
5. Tazama Hapa Makundi ya AFCON 2025