Jinsi ya Kuweka na Kutoa Call Forwarding Kwenye Simu Yako
Katika ulimwengu wa sasa wa mawasiliano, kuhakikisha hupotezi simu muhimu ni jambo la msingi. Mojawapo ya njia bora za kufanikisha hili ni kupitia huduma ya Call Forwarding. Katika makala hii, tutachambua kwa kina jinsi ya kuweka na kutoa Call Forwarding kwenye simu yako, faida zake, na tahadhari unazopaswa kuchukua.
Makala hii itaenda kuangazia njia za uwekaji/uwezeshaji wa huduma ya Call Forwarding kwenye simu yako kwa kutumia njia ya Setting na matumizi ya Code
Call Forwarding ni Nini?
Call Forwarding, au Uelekezaji wa Simu, ni huduma inayokuwezesha kuelekeza simu zinazoingia kwenye namba yako kwenda kwenye namba nyingine. Hii inamaanisha, unapokuwa huwezi kupokea simu kwa sababu yoyote ile, unaweza kuhakikisha simu hizo zinaelekezwa kwa namba nyingine ili zisikupite.
Aina za Call Forwarding
Kuna aina kuu nne za Call Forwarding:
- Call Forwarding Unconditional (CFU): Hii inaelekeza simu zote zinazoingia moja kwa moja kwenda kwenye namba nyingine bila kujaribu kupiga simu yako kwanza.
- Call Forwarding Busy (CFB): Simu zinaelekezwa kwenda kwenye namba nyingine pale tu unapokuwa kwenye simu nyingine au namba yako imejaa.
- Call Forwarding No Reply (CFNR): Simu zinaelekezwa ikiwa haujajibu baada ya muda fulani uliowekwa.
- Call Forwarding Not Reachable (CFNRc): Simu zinaelekezwa pale tu simu yako inapokuwa haipatikani, kwa mfano, ikiwa imezimwa au haina mtandao.
Jinsi ya Kuweka Call Forwarding
Kama unahitaji kutumia huduma ya call Forwarding jua kunanjia mbalimbali za kuweza kuwezesha huduma ya Call Forwarding kwenye simu yako, Hapa chini ni baadhi ya njia za kuwezesha huduma ya Call Forwading kwenye simu yako.
1. Kwenye Simu za Android
- Fungua Programu ya Simu: Bonyeza ikoni ya simu kwenye kifaa chako.
- Fungua Mipangilio: Bonyeza alama ya nukta tatu au menyu kisha chagua “Mipangilio” au “Settings”.
- Chagua “Call Forwarding”: Katika menyu ya mipangilio ya simu, tafuta na uchague “Call Forwarding”.
- Chagua Aina ya Call Forwarding: Chagua aina ya uelekezaji unayotaka (kwa mfano, “Always forward”, “Forward when busy”, nk.).
- Ingiza Namba ya Kuelekeza: Ingiza namba ya simu unayotaka kuelekeza simu zako.
- Hifadhi Mabadiliko: Bonyeza “Enable” au “Turn on” ili kuhifadhi mabadiliko.
2. Kwenye Simu za iPhone
- Fungua Mipangilio (Settings): Bonyeza ikoni ya “Settings” kwenye skrini kuu.
- Chagua “Phone”: Shuka chini na uchague “Phone”.
- Chagua “Call Forwarding”: Bonyeza “Call Forwarding”.
- Washa Call Forwarding: Geuza kitufe cha Call Forwarding kiwe kijani.
- Ingiza Namba ya Kuelekeza: Bonyeza “Forward To” kisha ingiza namba ya simu unayotaka kuelekeza simu zako.
- Rudi kwenye Mipangilio: Baada ya kumaliza, rudi nyuma ili kuhifadhi mabadiliko.
3. Kutumia Msimbo wa USSD
Unaweza pia kutumia misimbo ya USSD kuweka Call Forwarding:
- Kuelekeza Simu Zote: Piga
**21*<namba ya kuelekeza>#
kisha bonyeza kitufe cha kupiga simu. - Kuelekeza Simu Wakati wa Kujishughulisha: Piga
**67*<namba ya kuelekeza>#
. - Kuelekeza Simu Wakati wa Kutopokea: Piga
**61*<namba ya kuelekeza>#
. - Kuelekeza Simu Wakati wa Kutopatikana: Piga
**62*<namba ya kuelekeza>#
.
Kumbuka kubadilisha <namba ya kuelekeza>
na namba halisi unayotaka kuelekeza simu zako.
Jinsi ya Kutoa Call Forwarding
Ili kuzima Call Forwarding, unaweza kutumia misimbo ifuatayo:
- Kuzima Uelekezaji Wote: Piga
##002#
kisha bonyeza kitufe cha kupiga simu. - Kuzima Uelekezaji wa Simu Zote: Piga
##21#
. - Kuzima Uelekezaji Wakati wa Kujishughulisha: Piga
##67#
. - Kuzima Uelekezaji Wakati wa Kutopokea: Piga
##61#
. - Kuzima Uelekezaji Wakati wa Kutopatikana: Piga
##62#
.
Baada ya kupiga msimbo husika, utapokea uthibitisho kwamba uelekezaji umeondolewa.
Faida za Kutumia Call Forwarding
- Kupatikana Wakati Wote: Hakikisha hupotezi simu muhimu hata kama huwezi kupokea kwenye namba yako ya kawaida.
- Kuboresha Huduma kwa Wateja: Biashara zinaweza kuelekeza simu kwa watoa huduma wengine ili kuhakikisha wateja wanahudumiwa haraka.
- Kudhibiti Simu Zinazoingia: Unaweza kuelekeza simu kwenda kwenye namba nyingine wakati haupo ofisini au unahitaji muda wa kupumzika.
Mpendekezo ya Mhariri;
1 Jinsi ya Kukopa Salio Airtel
2. Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2025
3. Jinsi ya kubadilisha kifurushi cha Azam TV