Yanga vs MC Alger Leo 18 January 2025
Habari mwana michezo wa Kisiwa24 Blog karibu katika kurasa hii itakayoenda kukupa uchambuzi wa kina juu ya mchezo wa Yanga dhidi ya MC Alger kwenye ligi ya mabingwa roundi ya 6 katika hatua ya makundi kusaka tiketi ya kuweza kufuzu hatua ya robo fainali.
Siku na Muda wa Mchezo
Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa siku ya jumamosi ya taree 18/01/2025 katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya 10:00 jioni. Huu ni mchezo wa marudiano baina ya timu zote 2 baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa 07 December 2024 na Yanga iliweza kupoteza mchezo huo akiwa ugenini kwa kupokea kichapo cha goli 2 kwa sifuri.
Umuhimu wa Mchezo Huu
Mchezo huu ni muhimu kwa timu zote mbili kwani ndio mchezo wa maamuzi ya timu ipi kati ya hizi mbili itaenda kuungana na Al Hilal katika kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali.
Kutokana na msimamo wa kundi A Tayari timu moja imesha fuzu hatua ya robo fainali (Al Hilal) timu ya pili itakayoungana na Al Hilal kutoka kundi A itategemea mcheo wa Yanga na MC Alger. MC Alger iko katika nafasi ya pili katika msimamo wa kundi A ikiwa na pointi 8, ili kufudhu hatua ianayofuata inahitaji sare tu katika mchezo huu.
Yanga SC yenyewe iko katika nafasi ya 3 katika msimamo wa kundi A ligi ya mabingwa Afrika ikiwa na pointi 7 pointi moja nyuma ya MC Alger ili Yanga iweze kusonga mbele kwenye hatua ya Robo fainali inahitaji ushindi wa mchezo huu wa pointi 3 ili ifikishe pointi 10.
Matarajio ya Mashabiki
Mashabi walio wengi wa soka nchini Tanzania hasa wale wa Yanga wanaimani kubwa juu ya klabu ya Yanga inayocheza mchezo huu katika uwanja wake wa nyumbani kuibuka na ushindi ili kuweza kujihakikishia kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika kwa msimu wa 2024/2025. Kwa upande mwingine MC Alger wanatumani kuhakikisha wanapata japo sare katika mchezo huu kama sio kushinda ili kujipa nafasi ya kusonga mbele.
Tathimini ya Mchezo
Mchezo huu yutakua wa upinzani mkubwa kani kila timu inahitaji matokeo chanya katika mechi hii. Mashabiki wa soka wasubilie kuona burudani nzuri katika mchezo huu na kuona wachezaji wakionyesha vipaji vyao na uwezo wao ndani ya uwanja katika dakika zotez 90 za mchezo.
Mapendekezo ya Mhariri
1. Vituo Vya Kununua Tiketi Mechi ya Yanga vs MC Alger 18/01/2025
2. KIKOSI Yanga Vs MC Alger Leo 18 January 2025
3. Yanga vs MC Alger Leo 18 January 2025 Ni Saa ngapi?
4. CV Ya Jonathan Ikangalombo Mchezaji Mpya wa Yanga
5. Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho Afrika 2025