VIINGILIO Mechi ya Yanga vs MC Alger 18 January 2025
Habari mwanamichezo wa Kisiwa24 karibu katika makal hii fupi itakayoenda kukuonyesha kuhusu viingilio harisi vya mchezo wa marudiano wa raoundi ya 6 kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika 2025.
Kama wewe ni shabiki wa klabu ya Yanga na mpenda soka basi naamini utakua kusubilia kwa hamu mchezo huu wa Yanga vs MC Alger siku ya jumamosi 18/01/2025, Hivyo kama utahitaji kuutazama mtanange huu live kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam hauna budi kuweza kufahamu bei ya tiketi ya mechi hii ya Yanga vs MC Alger klabu bingwa Afrika mchezo wa roundi ya 6 hatua ya makundi kufudhu kwenda robo fainali.
VIINGILIO Mechi ya Yanga vs MC Alger 18 January 2025
Hapa chini ni mchanganuo wa bei ya tiketi ya mchezo wa Yanga vs MC Alger 18/01/2025.Viingilio katika mchezo huu vimeweza kugawanywa katika makundi maku manne ambayo ni;
1. Mzunguko (Orange) – Tsh 5,000
2. VIP C – 10,000
3. VIP B – Tsh 20,000
4. VIP A – Tsh 30,000
Hapa chini ni picha kuonyesha bei ya Tiketi mechi ya Yanga vs MC Alger 18/01/2025
Umuhimu wa Mchezo Huu kwa Yanga SC
Mchezo huu ni muhimu sana kwa klabu ya Yanga kwani ushindi wake katika mchezo huu utampa nafasi ya kuweza kusonga hadi nafasi ya 2 na kuweza kufuvu kwenda katika hatu inayofuata ya robo fainali ya michuano ya hii ya klabu bingwa Afrika kwa msimu wa 2025.
Hadi sasa kwenye kundi A klabu ya Yanga iko katika nafasi ya 3 ikiwa na jumla ya pointi 7 nyuma ya MC Alger iliyoko katika nafasi ya 2 ikiwa na pointi 8. Yanga haiitaji sare katika mchezo huu inahitaji pointi 3 ili kuweza kusonga hatua inayofuata.
Matumaini ya Mashabiki wa Yanga
Mashabi wa klabu ya Yanga wanamatumaini makubwa ya timu yoa kuweza kushinda katika mchezo huu na kuweza kusonga mbele kwenye hatua inayofuata ya robo fainali. Mchezo huu utafanyika siku ya jumamosi majira ya saa 10:00 jioni katika uwanja wa Benjamini Mkapa ulioko jijini Dar es Salaam.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho Afrika 2025
2. Timu Zilizofuzu Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2025
3. Ratiba ya Mechi Za Leo Ligi Mbalimbali
4. Msimamo Wa Ligi Kuu ya NBC 2024/2025 Tanzania Bara
5. Msimamo wa Ligi Kuu Uingereza EPL 2024/2025