TAMISEMI: FORM FIVE SELECTION 2025/2026

_________________________________________________

MATANGAZO YA AJIRA  KILA SIKU BOFYA HAPA

_________________________________________________

NOTES ZA KIDATO CHA 1 HADI 6 BOFYA HAPA

_________________________________________________

MAGROUP MAPYA YA WHATSAAP BOFYA HAPA

_________________________________________________
MATANGO YA AJIRA BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

Walioitwa Kwenye Usaili MDA’s NA LGA’s  January 2025

Filed in Nafasi Za Kazi Tanzania 2025, Usaili by on January 9, 2025 0 Comments

Walioitwa Kwenye Usaili MDA’s NA LGA’s  January 2025

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya MDAs & LGAs anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 14-01-2025 hadi 24-02-2025 hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

Walioitwa Kwenye Usaili MDA's NA LGA's Majina Ya Nyongeza January 2025

1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
2. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)
3. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
4. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka.
5. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
6. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.

7. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
8. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
9. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
10. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi
vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
11. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
12. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa iku ya usaili.

Walioitwa Kwenye Usaili MDA’s NA LGA’s January 2025

Bonyeza HAPA kupakua Tangazo Kamili

Mapendekezo ya Mhariri;

1. Orodha ya Majina Walioitwa Kazini Utumishi 2025

2. Nafasi za Kazi Kutoka Maendeleo Bank January 2025

3. Nafasi 5 za Kazi Kutoka AB InBev January 2025

4. Nafasi za Kazi 475 kutoka MDAs na LGAs January 2025

5. Nafasi za Kazi Kutoka Exim Bank January 2025

MATANGO YA AJIRA BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *