Jinsi ya Kujisajili na Kutumia App ya Startimes ON,jinsi ya kupakua Startimes On, App ya Startimes On, Jinsi ya kujisajili na Startimes On app,Startime On App Huduma kwa Wateja.Habari mwana Startimes katibu kwneye makala hii fupi amabayo itaenda kukupa mwangaza juu ya namna gani ya kudownload, kujisajili na kuweza kutumia App ya Startimes On app iliyotolewa na kampuni ya Startimes.
Jinsi ya Kujisajili na Kutumia App ya Startimes ON
Kuhusu Startimes
Hii ni moja kati ya kampuni maarufu zaidi Afrika kwa urushaji wwa channel na matangazo ya euninga. Startimes imekua kampuni pendwa zaidi batani Afrika hasa Tanzania kulingana na urushaji wa vipindi vyenye maudhui bora zaidi. Uwepo wa channele zenye vipindi vilivyotafsiriwa kwa lugha ya kiswahili umeipa nafasi ya juu zaidi kwa watumiaji wa lidha ya kiswahili. Channel kama
- Star swahili
- Tv 3
- Mambo Tv
Pia channel za Tanzania kama TBC 1, TBC 2, SAFARI CHANNEL, STAR TV, ITV, CHANNEL TEN, WASAFI TV CLOUDS TV na nyingine nyingi kumeifanya Startimes kua chaguo nambali moja kwa watumiaji wa lugha ya kiswahili.
Startimes On App ni Nini?
Hii ni Application iliyoanzaishwa na kampuni ya Startimes kwa lengo la kutoa huduma ya challen zinazorushwa kwenye runinga kupitia simu janja za mkononi. Mtumiaji wa Startimes On App anaweza kufurahia maudhui mbali mbali kama yale ya kwenye runinga kupitia startimes hata kama hana kisimbuzi cha Startimes.
Jinsi ya Kujisajili na Kutumia Startimes On App
Unaweza kufurahia channel zirushwazo na kampuni ya Startimes bure hata kama huna kisimbuzi cha Startimes kupitia kujisajili kwenye Startimes On App.
Katika makala hii tutaenda kukupa mwongozo wa jinsi ya kujisajili na kutumia Startimes On App kupitia simu yako ya mkononi, ila kumbuka ya kua huduma hii inapatika kwa watumiaji wa simu janja pekee (Smartphone)
Jinsi ya Kudownload Startimes On App
Hatua ya kwanza kabisa ili kuweza kutumia App ya Startimes On ni kupakua na kuinstall App ya Startimes On kwenye simu yako.
App ya Startimes On inapatikana kwneye Play Store, App Store na hata kwenye mfuomo wa APK unaweza kwenda Google na kudownload APK file na kuinstall kwenye simu yako.
Jinsi ya Kujisajili kwenye Startimes On App
Ukisha download na kuinstall App ya Startimes On kwenye simu janja yako sasa hatua inayofuata ni kuweza kujisajili. Ili uweze kujisaji unahitaji vitu vikuu vitatu
- Namba ya Simu
- Neno Siri
Kisha fungua App na ufuate hatua zifuatazo
1. Ukiwa ndani ya App ya Startimes On nenda kweneye eneo la akaunti
2. App itakupa machaguo mawili amabyo ni “Sign In na Sign Up” kwakua wewe ni mtumiaji wa mara ya kwanza changua Sign Up
3. Utapewa njia 3 za kuweza kujisajili njia ya Email, Namba ya simu na facebook akaunti.
4. Chagua njia unayopenda kujisajili nayo.
5. Kisha fuata maelekezo yanayofuata ili kuweza kujisajili.
Njinsi ya Kuingia (login) kwenye Startimes On App
Baada ya kukamilisha zoezi la kujisajili sasa utaweza kulogin kwenye akaunti yako ya Startimes On App. Ili kuingia kwenye akaunti yako ya Startimes On App tafadhari unaweza kufata hatua zifuatazo
1. Chini ya App ya Startimes On kuna menu ya Ap[p nenda palipoandikwa ME na upabonyeze
2. Pakisha funguka nenda juu kabisa mahari palipo andikwa SIGN IN na upabonyeze
3. Kisha ingiza login detail zako kama ulivyoweka wakati unasajili akaunti na bonyeza sign in
4 Kisha utakua umeingia kwenye akaount yako na unaweza kufurahia channel za Startimes On App bure.
Vifurushi Vinavyopatikana Kwenye App ya Startimes ON
Startimes On App inampa mtumiaji fursa za aina tatu ambazo ni
- Kuangalia Channel za Startimes kwa kulipia vifurushi vya kwenye App
- Kutazama channel za Startimes kwa kuunganisha na kisimbuzi chake
- Kuangalia channel za bure zilizopo kwenye Startimes bila kufanya malipo yoyote yale
A) Vifurushi vya Startimes On App
Ukiwa na startimes On App unaweza kufanya malipo ya vifurushi zinavyopatikana kwa matumizi ya APP peke yake. Ili kuweza kulipia vifufushi vya startimes On kwenye APP embu fuata hatua zifuatazo;
- Fungua App ya Startimes On na ulogin kwenye akaunti yako
- Kisha nenda kwenye MENU chini ya App na bonyeza palipoandikwa ME
- Juu kabisa utaona maneno yalioandikwa ” My star Times On Plan” mbele ya maneno hayo kunaneo ” MORE” bonyeza kwenye hilo neno
- Page mpya itafunguka na kisha nenda kwneye “ALL”
- Ukisha bonyeza neno ALL utaona vifurushi vyote vya Startimes On App.
Kwenye Startimes On App kunavifurushi vya aina 4 amabavyo mtumiaji anweza kulipia kwa siku, wiki,mwezi, miezi 3 na Mwaka
Kifurushi cha Max VIP
Kifurushi hiki kinampa mtumiaji wa startimes On App kuweza kutumia channel zote za kulipia zitolewzao na Startimes isipokua channel ya Mambo Tv
- Malipo ya Siku Tsh 2,200
- Malipo ya Wiki Tsh 5,600
- Malipo ya Mwezi Tsh 12,000
- Malipo ya Miezi 3 Tsh 23,000
- malipo ya Mwaka Tsh 69,000
Kifurushi cha Poa Max
Kifurushi hiki kinakupa uwezo wa kutazama channel ya Mambo Tv
- Malipo ya Siku Tsh 1,000
- Malipo ya Wiki Tsh3,000
- Malipo ya Mwezi Tsh 6,000
- Malipo ya Miezi 3 Tsh 13,000
- malipo ya Mwaka Tsh 39,000
Kifurushi cha Cold-Blooded Boss
Hiki ni kifurushi kinachokupa wasaha wa kutazama tamthiliya ya “Cold-Blooded Boss Love Me” pekee pindi utakaponunua kifurushi utaweza kutazama Tamthiliya hii hadi itakapo malizika.
- Gharama za kifurushi hiki ni Tsh 2,000 hadi tarehe 2/08/2025
Kifurushi cha Stand-In Husband
Pia Hiki ni kifurushi kinachokupa wasaha wa kutazama tamthiliya ya “Oop, Yuo Are A Stand-In Husband” pekee pindi utakaponunua kifurushi utaweza kutazama Tamthiliya hii hadi itakapo malizika.
- Gharama za kifurushi hiki ni Tsh 2,000 hadi tarehe 2/08/2025
B) Kuangalia Channel za Startimes On App kwa Kulink Kisimbuzi chako
Wateja ambao tayari wanavisimbuzi vya Startimes wanaweza kufurahia vifueushi walivyovilipia kwenye visimbuzi vyao kupitia App ya Startimes On wakati wowote. Ili kuweza kuunganisha kisimbuzi chako na App ya Startimes On tafadhari fuata hatua zifuatazo;
1. Ingia kwenye App ya Startimes On kisha login kwenye akaunti yako
2. Nenda upande wa MENU ya App chini na ubonyeze palipo andikwwa ME
3. Kisha tafuta na ubonyeze palipoandikwa Startimes Decoder Service
4. Kisha bonyeza palipoandikwa Click Here To Link Your Decoder
5. Ingiza namba za kisimbuzi chako na kisha ubonyeze linki
6. Hadi hapo utakua umeunganisha kisimbuzi chako na App yako ya Startimes On na utaweza kufurahia channel za kifurushi kilicholipiwa kwenye kisimbuzi chako kupitia Strimes On App.
C) Kutazma channel Bure kwenye Startimes On App
Fursa ya mwisho ni uwezo wa mtumiaji wa App ya Startimes On kuweza kutizama baadhi ya channel bure kabisa bila kulipia gharama za aina yoyoyte.
Ilio kuweza kutazama channel za startimes bute kabisa kupitia Startimes On App fuata hatua zifuatazo
1. Fungua App ya startimes kwenye simu janja yako, hii haiitaji hata kua na akaunti kwenye Startimes On App
2. Nenda chini ya App utaona menu, kisha bonyeza neno ” LIVE TV”
3. Hapa orodha ya channel zote za tv zitaonyeshwa za kulipia na zile za bure
4. Ili kutizama channe za bure tafuta channel zilizoandikwa “TRIAL”
5. Channel zote zenye neno trial unaweza kutazma bure kabisa bita kulipia chochote ukiwa na Startimes On App.
6. Furahia maudhui ya bure ya tv ukiwa na startimes On App.
Jinsi ya Kufanya Malipo ya Vifurushi vya Startimes ON App
jinsi ya kulipia vifurushi vya Startimes On App unaweza kutumioa njia mbili amabzo ni
- Kupitia mitandao ya Simu
- Kupitia eWallet kwa mteja mwenye akaunti ya Startimes On
Ili kufanya malipo ndani ya App ya Startimes fuata hatua zifuatazo
Malipo kwa Njia ya Mitandao ya Simu
App ya Startimes On inaruhusu malipo kwa njia ya mitandao ya simu ya M-pesa na Tigo Pesa (Mix by Yas)
- Ingia kwenye app ya startimes On kisha nenda kwenye menu na ubonyeze neno ME
- Juu kabisa ya App bonyeza palipoandikwa MORE ili kufungua vifurushi vyote
- Chagua kifurushi unachokitaka na kibonyeze
- Kisha chagua muda wa malipo unaotaka kulipia mfano Siku, Wiki, Mwezi, Miezi 3 au Mwaka
- Kisha shuka chini na uchague njia ya malipo kwa mtandao wa simu kama ni M-Pesa au Tigo Pesa (MIX By Yas)
- Baada ya kuchagua mtandao wa kufanya malipo shuka chini na ubonyeza palipoandikwa BUY
- Page mpya itafunguka na utaingiza namba ya simu ya mtandao uliouchagua. Kumbuka namba ya simu utakayoiingiza iwe na kiwango cha fedha zaidi kidogo na kile nunachotaka kulipia ili kuruhusu makato ya uhamisho wa fedha (transaction fee)
- Kisha bonyeza neno NEXT na susbili
- Ujumbe utakumwa kwenye simu yako na kamiliasha malipo
- Hadi hapo utakua uimefanya malipo ya kifurushi chako cha Starimes On Ap na unaweza kufurahia channel zipatikanazo nadi ya App ya Starimes On.
Malipo kwa Njia ya Akaunti ya eWallet
Njia ya 2 ya Kufanya malipo ya kifurushi chako ndani ya Startimes On ni kutumia akaunti ya eWallet, njia hii ni kwa wateja amabao wamrfungua akaunti ndani ya app ya Startimes On
Ili kununua kifurushi ukipendacho kupitia akaunti ya eWallet itakupasa kwanza kuweka pesa kwenye eWallet yako kupitia mitandao ya simu kama vile
- Tigo-Pesa
- M-Pesa
- Airtel Money
- EzyPesa
- HalPesa
Ili kuongeza pesa kwneye akaunti yako ya eWallet kwa kutumia mitandao ya simu nenda kwenye neno RECHARGE kisha bonyeza mtandao unaotaka kufanya malipo ya eWallet yako kisha maelekezo ya kufuata yatatokea kwenye skrini ya simu yako ili kukamilisha uhamisho wa pesa kwenda kwenye akaunti yako ya eWallet ya Startimes On App
Baada ya kuhamisha fedha kwenye akaunti yako ya eWallet sasa unaweza kulipia kifurushi ukitakacho cha Startimes On App na kuanza kufurahia channel zilizopo kwenye App ya Startimes On.
NB;
Kumbuka njia ya malipo ya mtandao unayoitumia lazi simu iwe hweani ili kuweza kupokea ujumbe wa kukamilisha mailipo nje ya hapo hauta fanikiwa kuweza kufanya malipo ya kifurushi chako ndani ya startimes On App.
Faida na Hasara za Kutumuia Startimes On APP
Kwa watumiaji wa App ya Stimes On kunafaida na hasara zake embu katika kategoria hii embu tuangazie faida na hasara za kutumia App ya Startimes On.
Faida za Kutumia App ya Startimes On
1. Kutazama channel bure bila kulipia gharama ya aina yoyote ile
2. Kufuruahia channel za startimes mahari popote na wakati wowote
3. Urahisi wa kulipia vifurushi kwa njia ya mtandao na eWallet
4. Huna haja ya kufungua akaunti kwenye app ya Startimes ON
5. Unaweza kufurahia kifurushi cha kisimbuzi chako kupitia app ya startimes On kwa kuunganisha kisimbuzi chako na App yako
Hasara za Kutumia Startimes On App
Licha ya kuwepo kwa faida nyingi za kutumia Startimes On App lakini pia hakuna kitu kisichokua na hasara, zifuataoz ni hasara za kutuma App ya Startimes On
- Matumizi ya fedha za ziada kwa tumia bando – licha ya kuunganisha kisimbuzi chako na app ya startimes On au kununua kifurushi ndani ya startimes On App bado itakubidi uwe na internet data ili kuweza kutachama channel ndani ya App ya Startimes
- Matumizi mabaya ya muda, kwakua startimes on app iko ndani ya simu yako unaweza kujikuta mda wote unatazama vipindi vya vinavyoppatikana ndani ya statimes TV hata wakati wa kufanya kazi nyingine
- Matumizi ya Chaji ya Simu- App ya startimes inapokua on kwa mda mrefu pia huongeza matumiz ya chaji ya simu yako.
Startimes ON App Huduma kwa wateja
Kama unachangamoto kwenye utumizi wa app ya startimes On usiwe na shaka unaweza kuwasiliana nao kwa mawasiliano tuliyoyaweka hapa chini mawasiliano haya yanapatikana 24/7
Namba ya Simu
- 0764 700 800
- 0677 700 800
Hitimisho;
Startimes On App ni moja ya app bora zaidi kuwahi kutokea kwenye ulimwengu wa kampuni za urushaji wa matangazo ya channel za television nchini Tanzania, huduma zake ni nafuu zaidi naunaweza kulipa kuanzia kifurushi cha siku, wiki, mwezi, miezi 3 au hata mwaka pia unaweza kuunga decoder yako na App yako cha zidi ni kua App imedhibikiwa katika matuymizi ya data kwani unaweza kutumia kiwango cha chini cha mb hadi Mb 100 kwa lisaa.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Jinsi Ya Kulipia Vifurushi Vya King’amuzi Cha Startimes
2. Jinsi ya kubadilisha kifurushi cha Startimes