Cv ya Kelvin Nashon (Midfielder),Klabu ya Yanga iko kwenye mchakati wa kumsajili Kelvin Nashon kwenye usajili huu wa dirisha dogo.
Lengo la Yanga kufanya sajili ya Kelvin Nashon ni miongoni mwa mikakati yake ya kukijenga na kukiimalisha kikosi chake hasa kutokana na ubora wa vikosi vya timu pinzani ndani ya ligi kuu ya NBC na kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika.
Ikumbukwe ya kua hadi sasa kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika klabu ya Yanga imesha cheza michezo 3 na kwenye michezo hiyo 3 imeshapoteza michezo 2 na kutoa sare mchezo 1 hivyo kujikusanyia pointi 1 na iko katika nafasi ya 4 kwenye msimamo wa kundi A.
Kwenye ligi kuu ya NBC klabu ya Yanga iko kwenye nafasi ya 3 hadi sasa japo imecheza michezo 11 ikiwa na pointi 27 huku Azam ikiwa kileleni na pointi 33 ikiwa imecheza michezo 15
Usajili wa Kelvin Nashon Yanga unatija kubwa sana kwa kua Yanga bado inamapambano makubwa sana kwenye ligi ya ndani na michuano ya kimataifa Afrika.
Wasifu wa Kelvin Nashon
Jina kamili: Kelvin Nashon
Kuzaliwa: 2/08/2000
Mahari: Mwanza
Umri: miaka 24
Urefu: 1.68m
Nafasi Uwanjani: Kiungo (Midfielder)
Safari ya Kelvin Nashon kwenye Ulimwengu wa soka
Kelvin Nashon kwa sasa anachezea klabu ya Geita Gold na ni mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania
Klabu ya Yanga inataka kufanya sajili ya Kelvin Nashon kama moango wa kubolesha eneo la kiungo la klabu hiyo.