Yanga vs Mashuja Leo 19/12/2024, habari mwanamichezo wa Kisiwa24, karibu katika makala hii fupi itakayoenda kutoa uchambuzi mfupi wa mechi ya Yanga Dhidi ya Mashujaa kwenye ligi kuu ya NBC Tanzania bara msimu wa 2024/2025
Yanga vs Mashuja Leo 19/12/2024
Mechi ya Yanga na Mashujaa ni mechi ya matumaini mapya kwa klabu ya Yanga ambayo imetoka kushiriki michuano ya klabu bigwa Afrika kwa kucheza michezo 3, katika michezo hiyo mitatu Yanga imepoteza michezo 2 na kutoa sare mchezo mmoja.
Nafasi ya Kila Timu kwenye Ligi kuu ya NBC
Yanga SC
Kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC klabu ya yanga ipo katika nafasi ya 4 ikiwa imecheza taklibani michezo 11 na kujikusanyia pointi 27. Katika michezo 11 ambayo klabu ya Yanga imefanikiwa kuicheza kwenye ligi kuu ya NBC imeshinda michezo 9 na kupoteza michezo 2.
Mashujaa FC
Klabu ya mashujaa inakutana na Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC round ya 4 ikiwa katika nafasi ya 7 huku ikiwa imefanikiwa kucheza michezo 14, katika michezo hiyo 14, imeshinda michezo 4, imetoa sare michezo 7 na kufungwa michezo 3 hivyo kujinyakulia pointi 19.
Utabiri wa Mchezo
Kutokana na uzoefua na rekodi za nyuma mchezo huu klabu ya Yanga inanafasi kubwa ya kushinda mchezo huu. kama klabu ya Yanga itashinda mchezo huu itakua na pointi 30 hivyo kusongea hadi nafasi ya 3 mbele ya Singida Big Stars kwa utofauti wa magoli.
Ila kama mashujaa atashinda mchezo huu atasogea hadi nafasi ya sita kwa kua na pointi 22 na kuishisha klabu ya Fountain Gate ambayo inapointi 20.
Kama mchezo utamalizika kwa matokeo ya Sare basi kila timu itasalia kwenye nafasi iliyopo kwani Yanga itakia na pointi 28 na Mashujaa itakua na pointi 20.
Muda na Mahari Mchezo utakapochezwa
Mechi hii ya Yanga vs Mashujaa itachezewa jijini Dar es salaam
- Uwanja wa Benjamini Mkapa
- Muda; 6:00 jioni
Je wewe kama shabiki wa Yanga au Mashujaa nini matarajio yako kueleka mchezo huu? unaweza kuacha komenti yako hapo chini
Mapendekezo ya Mhariri:
1. CV ya Fahad Aziz Bayo Mchezaji Mpya wa Yanga Sc
2. TETESI za Usajili Yanga SC 2024/2025
3. Orodha ya Makombe Yote ya Simba SC Kwenye Ligi Kuu Tanzania
4. Msimamo wa Ligi ya NBC Championship Tanzania 2024/2025