Je umewahi kusikia juu ya Bakhresa Group?Unajua ni nani mwanzilishi wa kampuni hii maarufu zaii nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla?, Basi katika makala hii tutaenda kuangazia juu ya hitoria kwa ufupi ya Saidi Salim Bakhresa mwanzilishi na mmliki wa kampuni ya Bakhresa Group.
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Historia ya Said Salim Bakhresa Mmliki wa Bakhresa Group
Ili kumjua zaidi Said Salim Bakhresa embu amabatana nasi hadi mwisho wa makala hii.
Said Salim Bakhresa ni moja ya wafanya biashara maarufu zaidi nchini Tanzania alizaliwa mnamo mwaka 1949 katika visiwa vya Zanziber. Said Salim Bakhresa ndiye mwanzililishi wa kampuni kubwa zaidi nchini Tanzania ya Bakhresa Group, kampuni ambayo inatoa huduma nyingi sana kwa watanzania na Wa Afrika.
Pia Said Salim Bakhresa ndio mmiliki wa timu ya mpira wa miguu ya Azam FC chini ya Bakresa Group inayoshiriki michuano mbalimbali ikiwemo ligi kuu ya NBC Tanzania Bara.
Historia ya Maisha ya Said Salim Bakhresa
Said Salim Bakhresa ni mzaliwa wa Tanzania na maisha yake yalikua ya kawaida katika familia yake kitu kilicho msukuma kuwa na hamu ya kua ni moja ya wafanya biashara wakubwa zaidi.Katika hitoria ya Said Salim Bakhresa inaonyesha ya kua akiwa katakita umri wa miaka 14 ilimrazimu kuacha shule ili kuweza kusaidia majukumu mbalimbali kwenye familia yake
Akiwa na umri mdogo alijifunza uendeshaji wa biashara ndogo ndogo kama vile uuzaji wa viazi kisha alipanua biashara yake kwa kutengeneza mgahawa uliompa umaarufu kutokana na huduma bora na za kuvutia.
Hapo ndio msingi wa ubpambanaji wake na ukuaji kibiashara ulipoanzaia na kumfanya kua miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa zaidi nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla wake.
Safari yake kwenye Biashara
Unapo litaja jina la Said Salim Bakhresa basi huna budi kuzungumzia mwanzo kabisa mwa kuanza safari yake ya mafanikio ambayo leo amekua nayo. Chimbuko lake linaanza pale alipojiingiza katika biashara kwa kufungua mgahawa mdogo ambao ulipelekea hadi kufungua kiwanda kidogo cha usangaji nafaka za mahindi cka Kipawa Flour Mill na huo ndio ukawa mwanzo wa kukua kwake katika sekta ya biashara.
Kutoka kwenye kiwanda cha kusaga nafaka hadi kufikia kuanzisha kampun ya Bakhresha Group yenye mkusanyiko wa viwanga vingi ndani yake na chapa ya Azam. Viwanda vingi vya Said Salim Bakhresa chini ya mwamvuli wa Bkhresa Group vinajihusisha na bidhaa kama vile unga wa aina mbalimbali, vinywaji na Icream. Huku chapa ya Azam ikisimamia pia matangazo ya Lunga na timu ya mpira wa miguu ijulikanayo kama Azam FC.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Jinsi Ya Kurudisha Channel Zilizopotea Kwenye Kisimbizi Cha Azam
2. Njinsi ya Kuweza Kutazama Channel za Azam Tv Bure