Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC), Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Wizara ya Mifugo na Uvuvi anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi miamoja na tatu (103) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.
Nafasi za kazi Tume Ya Taifa Ya Mipango Ya Matumizi Ya Ardhi (NLUPC) December 2024
Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 3 ya 1984 na badae ikafanyiwa marekebisho na Sheria Na. 6 ya 2007 (Sura 116). Kuanzishwa kwa Tume kulionekana kuwa na umuhimu baada ya kubaini kuwa sera, sheria, na taasisi iliyoundwa haikuwa na ufanisi wa kutosha katika kuratibu shughuli na programu mbalimbali zinazohusiana na matunzi ya ardhi zinazofanywa na asasi mbalimbali za kisekta katika Serikali, sekta binafsi na Mashirika yasiyo ya Kiserikali.
Tume ilianzishwa ili kuwianisha na kuratibu sera na sheria zote zinazohusiana na matumizi ya ardhi, ili kukuza usimamizi bora na uboreshaji wa ubora wa ardhi kwa lengo la kuhakikisha matumizi endelevu ya ardhi, ili iweze kutoa uzalishaji bora ili kuimarisha kijamii na kiuchumi. Maendeleo ya kiuchumi na matengenezo ya ubora wa rdhi kwa tija ya muda mrefu
Nafasi za Kazi Zilizopo
- Afisa Mifumo Ya Taarifa Ya Jiografia Ii (Geographical Information
Systems)- Nafasi 1
Nafasi za Kazi Wizara Ya Ardhi, Nyumba Na Maendeleo Ya Makazi December 2024
Wizara ya Ardhi ilianzishwa kama idara ya Ardhi na baadae kubadilishwa na kuwa Wizara kamili ambayo ilibadilisha jina lake kulingana na majukumu ndani ya kipindi hicho mahususi. Jina la sasa ni Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambazo zinajumuisha idara kuu za Kisekta ambazo ni : Utawala wa Ardhi, Upimaji na Ramani, Mipango ya Makazi. Sehemu kuu za Kisekta ni Usajili wa Majina, Uthamini wa Mali na Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya. Mbali na hilo, Wizara ina idara na vitengo mbalimbali vinavyosaidia kuongeza ufanisi wa kazi kama vile; Utawala ma Usimamizi wa Rasilimali Watu, Fedha na Hesabu, Ukaguzi wa ndani, Huduma za Kisheria, Sera na Mipango, Taarifa Mawasiliano na Teknolojia (TEHAMA), Habari – Elimu na Mawasiliano na Usimamizi wa Ununuzi.
Nafasi za Kazi Zilizopo
- Mkufunzi Msaidizi Wa Ardhi (Cartographer) – Nafasi 2
- Mkufunzi Msaidizi Wa Ardhi (Land Management, Evaluation And
Registration) – Nafasi 2. - Mkufunzi Msaidizi Wa Ardhi – Geographical Information Systems (Gis) –
Nafasi 1 - Mkufunzi Msaidizi Wa Ardhi –(Graphics Arts And Printing) – Nafasi 2
- Mkufunzi Msaidizi Wa Ardhi – (Land Surveyor) – Nafasi 1
- Mkufunzi Ardhi Ii – (Land Management Evaluation) – Nafasi 4
- Mkufunzi Ardhi Ii – (Geographical Information Systems ) – Nafasi 2
- Mkufunzi Ardhi Ii – (Land Surveyor ) – Nafasi 1
- Mkufunzi Ardhi Ii – (Graphics Arts And Printing ) – Nafasi 2
- Mkufunzi Ii – (Land-Real Estate Finance And Investment ) – Nafasi 1
- Mkufunzi Ii – (Graphics And Design ) – Nafasi 1
- Mkufunzi Ii – (Environmental Management) ) – Nafasi 1
- Mkufunzi Ii – (Architect) – Nafasi 1
- Afisa Ardhi Ii (Land Officer Ii)- Nafasi 10
- Fundi Sanifu Ii – Upimaji Ardhi (Land Technician Survey Ii)- Nafasi 26
- Afisa Ramani Ii (Mapping Officer Ii) – Nafasi 8
- Afisa Usajili Msaidizi Ii ( Registration Assistant Ii) – Nafasi 8
Nafasi za Kazi Wizara Ya Mifugo Na Uvuvi December 2024
Wizara ina jukumu la kusimamia na kuendeleza mifugo kwa ujumla na rasilimali za Uvuvi kwa ajili ya kufikia Malengo ya Milenia, mkakati wa Taifa wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini, kuboresha maisha ya jamii zinazotegemea mifugo na uvuvi, usalama wa chakula bila kuathiri ustawi wa Wanyama na uhifadhi wa mazingira, kujenga na kusaidia uwezo wa kiufundi na kitaaluma kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Sekta Binafsi ili kuendeleza, kusimamia na kudhibiti uendelevu wa rasilimali za mifugo na uvuvi
Nafasi za Kazi Zilizopo
- Afisa Usimamizi Nyanda Za Malisho Ii (Range Management Officer Ii)–Nafasi 4
- Afisa Usimamizi Nyanda Za Malisho Msaidizi Daraja La Ii (Range Management
Field Officer Ii) Nafasi 4 - Mteknolojia Wa Samaki Daraja La Ii (Fish Technologist Ii) – Nafasi 7
- Muunda Boti Daraja La Ii (Boat Builder Ii) – Nafasi 1
Masharti Ya Jumla
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi yao na kuainisha vizuri kwenye dirisha la maombi uelemavu walionao kwa ajili ya utambuzi kwa Sekretarieti ya Ajira;
iv. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyithibitishwa naMwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
– Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
– Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na V
– Computer Certificate
– Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
vii. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 17th Desemba, 2024.
xiii. Muhimu: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu.anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU, OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
S.L.P. 2320 DODOMA.
xiv. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;http://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
xv. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.