Viingilio Mechi Ya Yanga Vs Al Hilal Sudan Jumanne 26 Novemba 2024, Habari mwana michezo wa Habarika24, karibu katika makala hii fupi ya kimichezo itakayoenda kukuhabarisha juu ya bei ya tiketi ya mechi ya Yanga Vs Al Hilal Sudani itakayo chezwa siku ya jumanne 26 Novemba 2024 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuanzia majira ya saa 16:00 za jioni.
Yanga itaingia uwanja katika mchezo wake wa kwanza kwenye hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika kwa kuikaribisha Al Hilal Sudani tarehe 26 Novemba 2024.
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Kufuatia mchezo huo wa kimataifa wa klabu bingwa Afrika klabu ya Yanga nimetangaza viingilio vya mchezo huo huku ikitarajiwa mashabiki wengi wa klabu hiyo kuweza kununua tiketi zao mapema kwenda kuipa nguvu timu yao.

Viingilio Mechi Ya Yanga Vs Al Hilal Sudan
Viingilio vya mchezo huu vimegawanywa katika makundi manne kulingan na hadhi ya nafasi;
- Mzunguko (Machungwa): Tsh 3,000
- VIP C: Tsh 10,000
- VIP B: Tsh 20,000
- VIP A: Tsh 30,000
Viingilio vimekua rafiki na nafuu ili kuwawezesha mashabiki wa klabu ya Yanga na wapenzi wote wa mpira wa soka kuweza kumudu kununua tiketi na kushuhudia mchezo huo live.
Vituo Vya Kununua Tiketi Mechi ya Yanga Vs Al Hilal 26/11/2024
Baada ya kutangazwa viingilio rasmi vya mchezo wa Yanga dhidi ya Al Hilal Sudani pia vituo vitakavyotumika kununulia tikeki kwa ajili ya mchezo huo vimetangazwa na huduma ya ununuzi tiketi unaendelea.
Hapa chini ni ordha ya vituo vya kukunua tiketi mechi ya Yanga Vs Al Hilal 26 novemba 2024
- Young Africans – Jangwani
- Vunja Bei – Dar es Salaam Shops
- T-Money Ltd – Kigamboni
- Gitano Samwel – Mbagala Zakhem
- Khalfan Mohamed – Ilala
- Lampard Electronics
- Gwambina Lounge – Gwambina
- Karoshy Pamba – Dar Live (Zakhem)
- Antonio Service – Sinza, Kivukoni
- Tumpe Kamwela – Kigamboni
- Sovereign – Kinondoni Makaburini
- View Blue Skyline – Mikocheni
- Mkaluka Traders – Machinga Complex
- New Tech General Traders – Ubungo
- Sabana Business – Mbagala Maji Matitu
- Juma Burrah – Kivukoni
- Juma Burrah – Msimbazi
- Alphan Hinga – Ubungo
- Mtemba Service Co. – Temeke
- Jackson Kimambo – Ubungo
- Shirima Shop – Leaders
Jezi Mpya Za Yanga Kimataifa 2024/2025 (Jezi Za Yanga CAF 2024/2025)
Baada ya kutangaza viingilio vya mchezo wa Yanga dhidi ya Al Hilal Sudan Klabu ya Yanga pia imezindua jezi zake mpya ikakazozitumia kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika. Ambapo jezi hizo zime gawanywa katika makundi matatu
- Home Kit
- Away Kit
- Third Kit
Hapa chini ni picha za wachezaji wa klabu ya Yanga wakiwa wamevalia jezi mpya z klabu hiyo ya Yanga kwa michuano ya CAF Champions League mumsimu wa 2024/2025
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Ratiba ya Simba SC Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025
2. Jezi Mpya Za Simba SC Kimataifa Msimu Wa 2024/2025
3. Ratiba Ya Mechi Zote Za Yanga Ligi Kuu Ya Nbc Msimu Wa 2024/2025
4. Ratiba Ya Ligi Kuu England 2024/2025 (EPL Fixtures 2024/2025)