Nafasi Mpya Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Wangingombe Novemba 2024
DEREVA DARAJA II NAFASI 5
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne na Leseni hai Daraja la C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
MAJUKUMU YA KAZI YA DEREVA DARAJA II
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari (log book)
- Kufanya usafi wa gari.
NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi ya Mshahara wa Serikali – TGS B
MWANDAZI DARAJA LA II NAFASI 2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV na kufuzu Mafunzo si chini ya mwaka mmoja katika fani ya Food and Bevereges kutoka kwenye vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
MAJUKUMU YA KAZI YA MWANDAZI DARAJA II
- Kuandaa sehemu ya kulia chakula.
- Kupamba meza ya kulia chakula
- Kupanga vifaa vya kulia chakula na vinywaji mezani
- Kuandaa vinywaji
- Kuondoa vyombo baada ya kula chakula
NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi ya Mshahara wa Serikali – TGS.B MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI WA NAFASI ZA KAZI
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma
Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E- mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;
Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards);
“Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Watakao kidhi Sifa zinazotakiwa ndio pekee watakaoitwa katika Usahili.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 28/11/2024