Jinsi ya Kuweka Pesa Kwenye Kadi ya Mwendokasi Kwa HaloPesa, Habari mwana habarika24 karibu katika makala hii fupi itakayokupa mwongozo wa kuweza kuongeza pesa/salio kwenye kadi yako ya malipo ya usafiri wa mwendo kasi kwa kutumi mtandao wa Halotel (HaloPesa)
Fahamu Kuhusu Wakala Wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART)
Wakala Wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) ni taasisi ya serikali iliyoundwa kwa mujibu wa Tangazo la serikali No. 120 la tarehe 25 Mei 2007 chini ya sheria No. 30 ya Wakala za Serikali ya mwaka 1997 na marekebisho yake. Jukumu kuu la DART ni kuanzisha na kuendesha mfumo wa Usafiri wa Mabasi Yaendayo katika mkoa wa Dar es Salaam.
DART imeamua kurahisisha shuguli ya kufanya malipo kwa abiria wanaotumia usafiri wa mabasi ya mwendokasi kwa kupunguza foreni ya kukata tiketi kwa kuanzisha kadi janja ambayo itakua ikitumika katika kufanya malipo ya usafiri wa mabasi ya mwendo kasi.
Kuhusu Kadi ya Mabasi ya mwendokasi
Kadi ya mwendokasi ni kadi inayotumika kufanya malipo ya usafiri wa mabasi ya mwendokasi pale abiria anapotaka kusafiri kwa kutumia mabasi hayo. kama unahitaji maelezo zaidi kuhusu kadi ya mwendokazi kama vile upatikanaji wake na jinsi inavyofanya kati tafadhari bonyeza HAPA.

Jinsi ya Kuweka Pesa Kwenye Kadi ya Mwendokasi Kwa HaloPesa
Ili kuweza kuongeza salio/pesa katika kadi yako ya mwendokasi baada ya salio kuisha kupitia mtandao wa simu wa Halotel (HaloPesa) unatakiwa kufuata hatua hizi hapa chini;
- Ingia kwenye ,menu ya HaloPesa kwa kupiga Piga *150*88#
- Kisha Chagua 4 – Lipa bili
- Kisha Chagua 5 – Malipo ya Serikali
- Ingiza kumbukumbu namba (Namab ya kadi ya Mwendokasi)
- Ingiza Kiasi unachotaka kukiweka kwenye kadi yako
- Ingiza Pin ya HaloPesa
- Bonyeza 1 ili kuthibitisha
- Utapokea ujumbe utakaokujulisha malipo ya muamala yanafanyiwa kazi.
Hizo hapo ndio hatua za kufuata ili kuweza kuongeza pesa kwenye kadi yako ya Mwendokasi kwa kutumia mtandao wa simu wa Halotel.
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa unamaswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku