CAF Orodha Ya Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking),Vilabu Bora Afrika 2024/2025 CAF Ranking – CAF Ranking of African Clubs 2024, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetangaza orodha mpya ya vilabu bora Afrika kwa msimu wa 2024/2025, ikionyesha mabadiliko makubwa katika mandhari ya soka barani Afrika. Orodha hii inazingatia utendaji wa vilabu katika mashindano ya kimataifa na ya ndani, hususan Champions League ya Afrika na Confederation Cup.
Al Ahly SC kutoka Misri inaendelea kudumisha nafasi yake kama klabu bora zaidi Afrika, ikifuatiwa kwa karibu na Esperance Tunis.
Orodha Ya Vilabu Bora Afrika 2024
Nafasi | Jina La Klabu | Ponti |
1 | Al Ahly | 82 |
2 | Esperance Tunis | 61 |
3 | Waydad AC | 60 |
4 | Mamelodi Sundowns | 54 |
5 | Zamalek | 43 |
6 | RS Berkane | 42 |
7 | Simba SC | 39 |
8 | Petro de Luanda | 39 |
9 | TP Mazembe | 38 |
10 | CR Belouizdad | 37 |
11 | USM Alger | 36 |
12 | Raja CA | 35 |
13 | Young Africans S.C. | 31 |
14 | ASEC Mimosas | 30 |
15 | Pyramids FC | 29 |
16 | AL Hilal | 25 |
17 | JS Kabylie | 22 |
18 | Rivers United | 18 |
18 | Horoya AC | 18 |
20 | Étoile du Sahel | 16 |
20 | Orlando Pirates | 16 |
22 | Dreams FC | 15 |
24 | Future FC – | 12 |
24 | Marumo Gallants | 12 |
25 | Coton Sports | 11.3 |
27 | FC Nouadhibou | 10.5 |
28 | Abu Salim | 10 |
28 | Stade Malien | 10 |
28 | Kaizer Chief | 10 |

Umuhimu wa Vilabu Bora Afrika
Vilabu bora vya mpira wa miguu barani Afrika vimekua na umuhimu mkubwa katika maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu na jamii kwa ujumla. Hapa chini ni baadhi ya faida za kuwa na virabu bora barani Afrika
- Huvutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchi
- Huongeza mapato ya serikali kupitia kodi
- Huunganisha watu wa jamii tofauti
- Hukuza vipaji vya vijana na kuwapa nafasi ya kujipatia riziki
- Huimarisha hadhi ya nchi kimataifa
- Huvutia wachezaji bora kutoka nchi mbalimbali
Nafasi ya Simba na Yanga kwenye Orodha Ya Vilabu Bora Afrika 2024
Vilabu vya Tanzania vya Simba na Young Africans (Yanga) vimeendelea kuimarisha nafasi yao katika ramani ya soka barani Afrika. Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni, vilabu hivi viwili vikubwa vya Tanzania vimekuwa vikishiriki kwa ufanisi katika mashindano ya kimataifa, hususan Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika.
- Simba iko nafasi ya 7
- Yanga iko nafasi ya 13
Hitimisho
Vilabu hivi vimekuwa mstari wa mbele katika kuboresha viwango vya soka Afrika. Uwekezaji wao katika miundombinu, maendeleo ya vijana, na teknolojia ya kisasa umechangia pakubwa katika mafanikio yao. Kadri soka ya Afrika inavyoendelea kukua, vilabu hivi vitaendelea kuwa mfano wa kuigwa kwa vilabu vingine barani.