Huyu Hapa Kocha Mpya Wa Manchester United Mrithi Wa Ten Hag, Jumatatu ya tarehe 28 mashabiki na wapenzi wa soka duniani kote walishuhudia klabu kubwa duniani Man Utd ikimfukuza kocha wake mkuu Eric Ten Hag kufuatia matokeo mabovu ya mfururizo kwa takribani mechi 8.
Matokeo yaliochangia kufukuzwa kwake ni mechi yake na West Ham Utd uyliofanyika siku ya jumapili ya tarehe 27 mwezi 10 kufuatia kichapo cha goli 2 kwa 1.
Kocha Mpya Wa Manchester United

Mrith wa Ten Hag kwa Muda Mfupi
Baada ya kufukuzwa kwake uongozi wa klabu ulimteua aliyekua kocha msaidizi wa Ten Hag Ruud van Nistelrooy kukiongoza kikosi hicho cha mashetani wekundu kwa muda.
Ten Hag anaondoka klabuni hapo akiacha Man utd katika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi kuu ya uingeleza huku ikiwa na pointi 11 na kucheza michezo 9 huku ikiwa na GD ya -3
Nani Kurithi mikoba ya Ten Hag Man Utd?
Kumekua na fufunu za makocha wengi kusakwa na matajiri wa united wakihitaji saini zao ili kukinoa kikosi hicho cha mashetani wekundu.
Miongoni mwa makocha wanaosakwa na wamiliki wa klabu ya Manchester United ni pamoja na hawa walioko kwenye picha hapa chini.
Hao ndio makocha watano wanao waniwa ili kuweza kuchukua nafasi ya Eric Ten Hag ndani ya kikosi cha Man Utd
Embu Tupitie Wasifu wao Kwa Ufupi
Mmoja kati ya hawa hapa ndio anaetajwa kuchukua mikoba ya Eric Ten Hag katika klabu ya Man Utd ingwa kwa sasa R . Van Nistelrooy ndiye anaye hudumu kama kocha wa mpito apo awali alikua kocha msaidizi wa Ten Hag.
1. R. van Nistelrooy
Umri – Miaka 48
Kama kocha ameweza kushiriki michezo 148, ameshinda michezo 76, amedroo michezo 33 na kupoteza michezo 39.
2. Xavi
Umri – Miaka 44
Kama kocha ameweza kushiriki michezo 239, ameshinda michezo 157, amedroo michezo 36 na kupoteza michezo 46.
3. R. Amorim
Umri – Miaka 39
Kama kocha ameweza kushiriki michezo 244, ameshinda michezo 174, amedroo michezo 34 na kupoteza michezo 36.
4. G. Southgate
Umri – Miaka 54
Kama kocha ameweza kushiriki michezo 287, ameshinda michezo 138, amedroo michezo 64 na kupoteza michezo 85.
5. T. Frank
Umri – Miaka 51
Kama kocha ameweza kushiriki michezo 424, ameshinda michezo 191, amedroo michezo 97 na kupoteza michezo 136.
Hitimisho
Embu tuambie wewe kama shabiki wa Manchester Utd na shabiki wa soka la uingereza unadhani kutoka kwenye orodha hiyo hapo juu ni nani ataechukua mikoba ya Ten Hag pale Old Trafford ili kukinoa kikosi cha mashetani wekundu? Acha komenti yako hapo chini kupitia kisanduku cha maoni.