Ten Hag Atimuliwa Man Utd, Baada ya kuitumikia klabu ya Mancherster United kwa takribani miaka miwili na na miezi kadhaa hatimae kocha mkuu wa klabu hiyo Erik ten Hag amefukuzwa kazi kutokana na mfururizo wa matokeo mabovu ya timu hiyo.
Maamuzi ya klabu ya Man United kumfuta kazi Ten Hag yamekuja baada ya mechi ya jumapili dhidi ya West Ham United ambapo matokeo ya mchezo huo yalikua 2-1 kwa Man United kupoteza mchezo huo.
Kocha Ten Hag amefukuzwa kazi huku klabu hiyo ikiwa katika nafasi ya 14 katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza kwa kuawa na pointi 11 huku ikiwa imecheza michezo 9 katika ligi hiyo.
Ten Hag alianza kuitumikia klabu hiyo ya mashetani wekundu mnamo mwaka 2022 mwezi April kama kocha mkuu wa timu hiyo.
Baada ya kufutwa kazi kwa kocha mkuu wa Man utd aliyekua kocha msaidizi wa timu hiyo Ruud van Nistelrooy amepewa nafasi ya kushika ukocha mkuu wa klabu hiyo kipindi hiki ambacho timu hiyo haina kocha mkuu.

Ten Hag Atimuliwa Man Utd
Safari ya Ten Hag Ndani ya Manchester Utd
Kama tulivyosema kocha Ten Hag alijiunga na klabu ya Man Utd mnamo mwezi April 2022 na hii ndio likua safari yake kwenye ligi kuu ya uingereza
- Amecheza michezo 85
- Ameshida michezo 44
- Ametoa Droo Michezo 15
- Amefungwa Michezo 27