Makundi ya Klabu Bingwa Africa Msimu wa 2024/2025 (Caf Champions League Groups)
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
BONYEZA HAPA KUJIUNGA NA TELEGRAM CHANNEL YETU
Makundi ya Klabu Bingwa Africa Msimu wa 2024/2025,Makundi ya Caf Champions League 2024/25, Kundi la Yanga CAF Klabu Bingwa Afrika 2024/2025 , Habari ya wakati huu mwanasoka wa Habarika24, Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika tarehe 7 ya mwezi October mwaka wa 2024 imweza kuchezesha droo ya hatua ya makundi kwa ligi ya klabu bingwa Afrika msimu wa 2024/2025 na kutangaza makundi makundi manne yenye timu nne kwa kila kundi. Hii ndio hatua muhimu sana iliyokua ikisubiliwa na wapenzi wa soka barani Afrika na Dunia kwa Ujumla.
Kwa wapenda soka wa Tanzania hasa mashabiki wa klabu za Simba na Yanga basi mmesha fahamu kua klabu zenu zimwewekwa na timu gani katika makundi hayo ya ligi ya klabu bingwa Afrika msimu wa 2024/2025.
Makundi ya Klabu Bingwa Africa Msimu wa 2024/2025
Hapa tutaenda kuangazia Makundi yote manne na timu ambazo zipo katika kila kundi
Muundo wa Makundi
Timu 16 bora zimegawanywa katika makundi manne, kila kundi likiwa na timu nne. Timu hizi zitacheza mchezo wa kwenda na kurudi dhidi ya kila timu katika kundi lao. Timu mbili bora kutoka kila kundi zitaendelea hadi hatua ya robo fainali.
Kundi A
- TP Mazembe (DR Congo)
- Yanga (Tanzania)
- Al Hilal SC (Sudan)
- MC Alger (Algeria)
Kundi B
- Mamelodi Sundowns (South Africa)
- Raja Club Athletic (Morocco)
- AS FAR (Morocco)
- AS Maniema Union (DR Congo)
Kundi C
- Al Ahly SC (Egypt)
- CR Belouizdad (Algeria)
- Orlando Pirates (South Africa)
- Stade d’Abidjan (Ivory Coast)
Kundi D
- ES Tunis (Tunisia)
- Pyramids FC (Egypt)
- GD Sagrada Esperance (Angola)
- Djoliba AC (Mali)

Matarajio ya Walio Wengi
Mashindano haya yanaahidi kuwa na mchezo wa kuvutia na wa hali ya juu. Timu za Kaskazini mwa Afrika zimeendelea kuonyesha ubora wao, lakini timu kutoka sehemu nyingine za Afrika zinaonekana kuwa na nia ya kuvunja ukabila huu.
Kwa mashabiki wa soka la Afrika, msimu huu wa Ligi ya Klabu Bingwa unakuja na ahadi ya kuona mpira wa kisasa, mikakati ya hali ya juu, na nyota chipukizi za Afrika zikipeperusha bendera za nchi zao.
Hitimisho
Tunapotazamia mechi za makundi, ni wazi kwamba kila timu itahitaji kuwa katika hali yake bora ili kufanikiwa. Historia inaonyesha kwamba hata timu zinazoonekana kuwa na nafasi ndogo zinaweza kusababisha mshtuko. Ni mashindano ya kuvutia ambayo yataendelea kuchangia katika kukuza soka la Afrika na kuleta hamasa kwa mashabiki.
Je unadhani ni timu zipi zitaibuka kidedea katika kila kundi, kwa Watanzania na mashabiki wa klabu ya Yanga Unaipa nafasi ipi kwenye kundi A? embu acha komenti yako hapo chini kwenye kijumba cha komenti.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Jinsi ya Kununua Tiketi ya Mpira Kupitia Mtandao Wa M-pesa
2. Ratiba Ya Mechi za Chelsea Zilizobaki Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) 2024/2025
3. Ratiba Ya Mechi Za Simba SC Zilizobaki Ligi Kuu Ya NBC Msimu Wa 2024/2025
4. Ratiba ya Mechi Za Leo Ligi Mbali Mbali Duniani
5. Mchezaji mwenye Magoli mengi Tanzania
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku