Ubalozi unapenda kuwaarifu Watanzania kuhusu uwepo wa fursa za ufadhili wa masomo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili (Master’s Degree) kwa mwaka wa masomo 2026/2027 katika Chuo Kikuu cha Princeton, New Jersey na Chuo Kikuu cha Williams (Williams College), Massachusetts.
CHUO KIKUU CHA PRINCETON
Chuo Kikuu cha Princeton kimetangaza kutoa ufadhili wa masomo ya Shahada ya Uzamili katika fani zifuatazo:
- Master in Public Policy (MPP) na
Master in Public Affairs (MPA)
Vigezo vya Ufadhili:
- MPP – Ni programu ya mwaka mmoja (1) kwa waombaji wenye uzoefu wa kazi wa zaidi ya miaka saba (7+) (mid-career applicants).
- MPA – Ni programu ya miaka miwili (2) kwa waombaji wenye uzoefu wa kazi wa kati ya miaka miwili (2) hadi minne (4) (early career applicants).
Taarifa zaidi kuhusu fursa hizi zinapatikana kupitia tovuti: https://spia.princeton.edu/graduate-admissions
Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 15 Desemba 2025
CHUO KIKUU CHA WILLIAMS (Williams College)
Chuo Kikuu cha Williams (Williams College) kimetangaza nafasi za ufadhili wa masomo kwa mwaka wa masomo 2026/2027 katika fani ya Master of Arts in Policy Economics (MA in Policy Economics).
Vigezo vya Ufadhili:
Ufadhili huu ni kwa waombaji wenye uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu (3) katika masuala yanayohusiana na sera za umma.
Taarifa zaidi kuhusu fursa hii zinapatikana kupitia tovuti: www.cde.williams.edu
Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 01 Desemba 2025
Bonyeza Hapa Kudownload PDF ya Tangazo
