Nafasi za Kazi Hospitali ya Taifa ya Mirembe

Filed in Ajira by on March 22, 2026 0 Comments

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe anawatangazia uwepo wa nafasi za kazi kwa Ajira ya Mkataba wa Kujitolea.

Nafasi hizo zinahusu kada zifuatazo;

  • Maafisa Wauguzi Wasaidizi (ANO), nafasi kumi na nne (14).
  • Wasaidizi wa Afya (MATT) nafasi kumi (10).
  • Dereva, nafasi moja (1) na Afisa Habari nafasi moja (1).

Watanzania wenye sifa ya kuomba, na kujaza nafasi hizi, wanaombwa kuleta maombi ya:

✅AFISA MUUGUZI MSAIDIZI
Mwombaji awe na stashahada ya Uuuguzi kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, vyeti vya Uuguzi na Ukunga na leseni hai.

✅MSAIDIZI WA AFYA
Mwombaji awe na cheti kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali,

✅DEREVA
Mwombaji awe na cheti kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na leseni hai.

✅AFISA HABARI
Mwombaji awe na stashahada au shahada kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali

SIFA ZA JUMLA

  • Awe na umri usiozidi miaka 35 (Thelathini na tano).
  • Awe amefaulu kidato cha Nne / Sita.
  • Awe na kitambulisho cha Uraia na
  • Awe na wadhamini wawili wanaotambulika na Serikali ya Kijiji/ Mtaa anapoishi.

MASHARTI YA JUMLA
Waombaji wote waambatishe nakala ya cheti cha kidato cha Nne / Sita, cheti cha taaluma, cheti cha kuzaliwa, maelezo binafsi (curriculum Vitae).

Waombaji watakaowasilisha “Result Slip”, “Statement of Result”, “Provisional Result” au “Transcript” HAWATAKUBALIWA.

Maombi yote yatumwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe,
S.L.P 910.
DODOMA
Au kupitia barua pepe: barua@mirembe.or.tz

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 08 Aprili, 2026, Saa 9:30 Alasiri.

JE, WEWE NI MIONGONI MWA  WATAFUTA KAZI?


Basi Unaweza Kujiunga na Watanzania Wenzako ili Kupata Matangazo ya Ajira Mpya Kila Siku Kutoka Serikalini na Kampuni Mbalimbali kwa Kugusa HAPA TU


Sambaza Kwa Ndugu na Marafiki ili nao Pia Waweze kupate Nafasi hizi Kila Siku.


JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM YETU HAPA.

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *