Chuo cha Ualimu King’ori
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Chuo cha Ualimu King’ori ni miongoni mwa taasisi maarufu za kielimu nchini Tanzania. Chuo hiki kinatoa mafunzo bora kwa walimu wanaotaka kuendeleza taaluma yao na kutoa elimu ya hali ya juu kwa wanafunzi. Kituo hiki kina mazingira mazuri ya kujifunza na miundombinu inayofaa kwa wanafunzi.
Chuo hiki kinatoa kozi mbalimbali zinazohusisha masomo ya msingi na ya juu, ambazo moja kwa moja zinalenga kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Wanapohitimu, wanafunzi wanakuwa na uwezo mkubwa wa kufundisha katika shule za msingi na sekondari.
Chuo cha Ualimu King’ori kinajulikana kwa kua na mazingira bora kwa kujifunzia yanayopelekea wanafunzi kupata ufahamu mzuri wa mbinu za ufundishaji kitu ambacho huwasaidia kuwa walimu bora na kuleta mabadiliko kwenye elimu ya Tanzania pale wanapohitimu kozi zao.
Sifa kuu za Chuo cha Ualimu cha King’ori
- Chuo hiki kinatoa mafunzo bora kwa walimu
- Programu zingine hutoa masomo ya msingi na ya juu
- Mazingira na miundombinu ni ya kuvutia kwa wanafunzi
Historia Ya Chuo ya Chuo Cha Ualimu cha King’ori
Chuo cha Ualimu King’ori kilianzishwa mwaka 2008 na kupata usajili wake mwaka 2015 kikiwa na lengo la kutoa mafunzo ya ualimu kwa vijana. Chuo cha ualimu King’ori kinapatikana katika mkoa wa Arusha.
Chuo cha ualimu King’ori kinatoa kozi za uiwalimu katika ngazi mbali mbali za elimu kama vile
- Ualimu wa awali,
- Ualimu wa msingi, na
- Ualimu wa sekondari.

Kozi zitolewazo na Chuo cha Ualimu cha King’ori
Chuo cha Ualimu King’ori kinatoa kozi mbalimbali za mafunzo katika ngazi ya cheti na Diploma ya elimu. Kozi zote zitolewazo na chuo cha ualimu cha King’ori zinazingatia elimu bora na ujuzi wa kufundisha.
Kozi za Cheti Zinazotolewa na Chuo Cha Ualimu Cha King’ori
Hapa tutaangazia kozi za ngazi ya cheti zinazotolewa na chuo cha ualimu King’ori, katika ngazi ya cheti chuo kinatoa mafunzo ya kozi moja tu ambayo ni
- Cheti cha Ufundi katika Elimu ya Msingi (In Service) katika ngazi ya NTA Level 5
Kozi za Cheti Zinazotolewa na Chuo Cha Ualimu Cha King’ori
Katika ngazi ya diploma chuo cha ualimu cha King’ori kinatoa mafunzo katika kozi mbili ambazo ni;
- Diploma ya Kawaida katika Elimu ya Msingi (In Service) katika ngazi ya NTA Level 6
- Diploma ya Kawaida katika Elimu ya Msingi (Pre Service) katika ngazi ya NTA Level 6
Programu Kuu za Mafunzo katika Chu cha ualimu cha King’ori
- Shahada ya Ualimu: Hii ni programu ya miaka mitatu. Inawawezesha wahitimu kuwa walimu wa shule za msingi na sekondari.
- Mafunzo ya Kitaaluma: Haya ni mafunzo ya muda mfupi yanayolenga kuongeza ujuzi wa walimu waliopo kazini.
- Mafunzo ya Ujuzi wa Maisha: Programu hii inakazia ujuzi wa maisha kwa wanafunzi. Husaidia katika maendeleo yao kwa ujumla.
Chuo kinatumia mbinu mbalimbali za kufundisha. Mbinu hizi ni kama vile:
- Darasani: Masomo yanahusisha mafunzo ya kawaida ya darasani.
- Vitendo: Wanafunzi wanapata nafasi ya kufanya mazoezi na kufundisha katika shule za karibu.
- Mikutano: Wanafunzi wanakutana na walimu na wataalamu kwa majadiliano na semina.
Programu hizi zimeundwa ili kukidhi mahitaji ya soko la kazi. Chuo kinahakikisha kuwa wahitimu wanakuwa tayari kwa changamoto za ufundishaji.
Sifa za Kujiunga na Chuo cha Ualimu cha King’ori
Ili kujiunga na kozi katika chuo cha ualimu cha King’ori mwanafunzi natakiwa awe amekidhi baadhi ya vigezo,hapa tuanaenda kuonyesha sifa za kujiunga na kozi za cheti na diploma;
Kozi ya Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE)
- Mwombaji anatakiwa awe na alama za ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu au GPA isiyopungua 1.6.
Kozi za Diploma
- Wanafunzi wanapaswa kuwa na alama za ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu katika masomo ya sekondari ya juu (A-level)
- Awe na alama tano za ufaulu katika masomo ya sekondari ya chini (O-level) ikiwemo Kiingereza na Hisabati.
Jinsi ya Kutuma maombi ya Kujiunga na Chuo cha Ualimu cha King’ori
Ili mwanafunzi aweze kujiunga na chuo cha ualimu cha King’ori laziama apitie baadhi ya hatua kama vile;
- Kujaza form ya maombi ya usajiri – form hupatikana kwenye tovuti ya chuo au kwa kufika katika ofisi za chuo
- Kujaz fomu ya usajiri – baada ya kupata fomu mwanafunzi atapaswa kuijaza kulingana na kozi anayotarajia kuisona
- Kulipia ada ya usajiri – hii hulipwa kwa kupityia banki
- Kurudisha fomu ya usajiri – baada ya kujaza na kulipa ada ya usajiri mwanafunzi anapawa kurejesha fomu ya usajiri katika ofisi za chuo ili kuanza mchakato wa usahili
Ada Ya Kozi katika Chuo cha Ualimu Cha King’ori
Ada ya chuo inaweza kulipwa kwa awamu kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali hapa chini. Hii ni kurahisisha malipo kwa wazazi au walezi wanaopata tabu kulipa ada zote za chuo kwa mkupuo.
Hata hivyo, wale ambao wanaweza kulipa kwa mkupuo au mara mbili wanaruhusiwa kufanya hivyo bila kuzingatia usambazaji huu.
Malipo ya Ada ya Chuo kwa Mwaka
Muda | Hostel | Kutwa |
Semester I | 650,000/= Tsh | 400,000/=Tsh |
Semister Ii | 650,000/=Tsh | 400,000/=Tsh |
Jumla | 1,300,000/=Tsh | 800,000/=Tsh |
Malipo ya Ada ya Chuo kwa Awamu
Semester I | Semester Ii | |||
Payment | Month | Amount | Month | Amount |
1st Installment | Jul – Sept | 200,000/=Tsh | Jan-March | 200,000/=Tsh |
2nd Installment | Oct – Dec | 200,000/=Tsh | April -May | 200,000/=Tsh |
Total | 400,000/= | 400,000/= |
Wanafunzi wa hosteli
Semester I | Semester Ii | |||
Payment | Month | Amount | Month | Amount |
1st Installment | Jul – Sept | 325,000/=Tsh | Jan-March | 325,000/=Tsh |
2nd Installment | Oct – Dec | 325,000/=Tsh | April -May | 325,000/=Tsh |
Total | 650,000/=Tsh | 650,000/=Tsh |
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na uongozi wa chuo cha ualimu cha King’ori kwa mawasiliano yafuatayo;
Phone: (+255) 754 255 888
Whatsapp: (+255) 754 255 888
Email: [email protected]
Head Office: 1 Arusha DC, Sekei, Arusha,Tanzania,
P.O.Box 708, Arusha
Hitimisho
Chuo cha Ualimu King’ori kimejengwa katika mazingira tulivu na ya asili.Chuo kinapatikana katika mkoa wa Arusha, karibu na milima na mandhari ya kuvutia. Hii inatoa fursa kwa wanafunzi kujifunza katika mazingira yanayosisimua. Miundombinu ya chuo iko vizuri kama vile, Majengo (Kuna madarasa, maktaba, na maabara), Nishati (Chuo kina umeme wa uhakika) na Maji lakini pia Chuo kina maeneo ya kupumzika na michezo ambayo yanasaidia wanafunzi kupumzika na kufanya mazoezi.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Ardhi Morogoro
2. Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Ardhi Tabora
3. Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha ADEM Bagamoyo
4. Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Utalii Arusha
5. Chuo cha Ualimu cha Waama Lutheran
6. Chuo cha Ualimu cha Moravian Mbeya
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku