Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Utalii Mwanza
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Utalii Mwanza, Habari ya wakati huu mwana habarika24, karibu katika makala hii fupi ambayo itaenda kukupa maelekezo juu ya ada, fomu, kozi na sifa za kujiunga na chuo cha utalii kampasi ya Mwanza.
Chuo cha utalii kampasi ya Mwanza inatoa kozi kwa ngazi ya cheti, diploma na utalii na inauwezo wa kuchukua wanafunzi takribani 500 kwa mwaka, katika makala hii tutaenda kuelezea juu ya ada za masomo na gharama zote katika kila kozi katika chuo cha utalii Mwanza.
Chuo Cha utalii Mwanza kipo katikati ya jiji la Mwanza na kina uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 wa Diploma, Cheti na uanagenzi kila mwaka. Ni maalumu katika Programu Mbili ambazo ni za kuongoza watalii Uendeshaji na Usafiri na utalii na ina vifaa vya kisasa vya mafunzo ya sanaa.
Kuanzishwa kwa kampasi ya Mwanza kuna dhamira pekee ya kuunga mkono juhudi za serikali za kuendeleza utalii katika ukanda wa Magharibi (Western Tourism Circuit) unaojumuisha mikoa ya Mwanza, Geita, Simiyu, Shinyanga, Kagera, Mara, Tabora, Katavi na Kigoma.
Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Utalii Mwanza
Kozi Zitolewazo na Chuo cha Utalii Mwanza
Hapa tuaenda kuangazia kozi zinazotolewa na chuo cha utalii kampasi ya Mwanza.Chuo cha utalii Mwanza kinatoa kozi katika ngazi ya Cheti na Diploma kwa level ya NTA level 4, NTA level 5 na NTA level 6. Miongoni mwa kozi zinazotolewa katika chuo cha utalii Mwanza ni pamoja na
- Cheti cha Msingi cha Ufundi katika Usafiri na Utalii
- Cheti cha Ufundi katika Uongozaji wa Watalii
- Diploma ya Usimamizi wa Utalii
Ada za Chuo cha Utalii Mwanza katika Kozi Mbali Mbali
Hapa tunaenda kuangalia ada zinazotozwa kwa kozi zinazotolewa na chuo cha utalii Mwanza kama kozi ya cheti(NTA level 4), kozi ya cheti (NTA level 5) na kozi ya Diploma (NTA level 6)
Ada ya Kozi ya Cheti (NTA Level 4) Katika Chuo cha Utalii Mwanza
- Ada ya Masomo 1,200,000
- Ada ya Safari za Kitaaluma 100,000
- Ada ya Mitihani 50,000
- Fedha ya Tahadhari 50,000
- Michango ya Umoja wa Wanafunzi 10,000
- Vitambulisho vya Wanafunzi 5,000
- Bima ya Afya 50,400 TZS
Jumla 1,465,400 TZS
Ada ya Kozi ya Cheti (NTA Level 5) katika Chuo cha Utalii Mwanza
- Ada ya Masomo – TZS 1,200,000
- Ada ya Safari za Kitaaluma – 0
- Ada ya Mitihani – TZS 50,000
- Fedha ya Tahadhari – TZS 0
- Michango ya Umoja wa Wanafunzi – TZS 10,000
- Vitambulisho vya Wanafunzi – TZS 5,000
- Bima ya Afya – 50,400 TZS
Jumla =1,310,400 TZS
Ada ya Kozi ya Diploma (NTA Level 6) Katika Chuo Cha Utalii Mwanza
- Ada ya Masomo – TZS 1,250,000 TZS
- Ada ya Safari za Kitaaluma – 0
- Ada ya Mitihani – TZS 50,000
- Fedha ya Tahadhari – TZS 0
- Michango ya Umoja wa Wanafunzi – TZS 10,000 TZS
- Vitambulisho vya Wanafunzi – TZS 5,000
- Bima ya Afya – 50,400 TZS
Jumla= 1,365,400 TZS
Mgawanyo wa Malipo ya Ada kwa Awamu
Cheti cha Ufundi wa Msingi ada kamili ni Tsh 1,415,000
Malipo ya Awamu 1 Tsh-495,000
Malipo ya Awamu 2-354,000
Malipo ya Awamu 3-300,000
Malipo ya Awamu 4-266,000
Cheti cha Ufundi Ada kamili Tsh 1,515,400
Malipo ya Awamu 1 Tsh-495,000
Malipo ya Awamu 2 Tsh-261,000
Malipo ya Awamu 3 Tsh-300,000
Malipo ya Awamu 4 Tsh-204,000
Cheti cha Ufundi (NTA Level 4) Ada Kamili Tsh -1,310,400
Malipo ya Awamu 1 Tsh-495,000
Malipo ya Awamu 2 Tsh-384,000
Malipo ya Awamu 3 Tsh-300,000
Malipo ya Awamu 4 Tsh-286,000
Kozi ya Diploma Ada Kamili ni Tsh-1,365,400
Malipo ya Awamu 1 Tsh-495,000
Malipo ya Awamu 2 Tsh-291,000
Malipo ya Awamu 3 Tsh-300,000
Malipo ya Awamu 4 Tsh-224,000
Gharama za Ziada Kwa Wanafunzi
- Gharama za Sare ni Tsh -i 150,000
- Gharama za Hosteli kwa Muhula ni Tsh-200,000
Fomu ya Kujiunga Na Chuo Cha Utalii Kampasi ya Mwanza
Kuna njia mbili za kupata fomu ya kuomba kujiunga na chuo cha utalii kwenye kampasi ya Mwanza
1. Unaweza kupata fomu ya kujiunga na chuo cha utalii kupitia tovuti ya chuo – nct.ac.tz
2. Njia ya pili ni kwenda moja kwa moja kwenye ofisi za chuo cha utalii kampasi ya Mwanza.
Pindi mwanafunzi anapoludisha fomu ya maombi ya kujiunga katika chuo cha utalii kampasi ya Mwanza anakatakiwa pia kuambatanisha viambatanisho kama vile, Paspoti sizi moja, vyeti vya kilaaluma,Cheti cha kuzaliwa na risiti ya malipo ya ada.
Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Utalii Mwanza
Hapa chini tunaenda kukuelezea juu ya sifa za kujiunga na chuo cha utalii kampasi ya Mwanza.Ili kujiunga na chuo cha utalii kampasi ya mwanza kunasifa na vigezo ambavyo mwombaji anapaswa kua navyo. Miongoni mwa sifa ni pamoja na;
Sifa za Kujiunga na kozi za Cheti cha Msingi (NTA Level 4)
- ili kujiunga na kozi hii mwombaji inabidi awe na cheti cha kidato cha nne (CSEE) na angalau alama nne za kufaulu
Sifa za Kujiunga na kozi za Cheti cha Ufundi (NTA Level 5)
- Ili kujiunga na kozi hii mwombaji inabidi awe na cheti cha kidato cha nne pamoja na cheti cha NTA Level 4
Sifa za Kujiunga na kozi za Diploma (NTA Level 6)
- Ili kujiunga na kozi hii mwombaji inabidi awe na cheti cha kidato cha sita au cheti cha NTA Level 5
Hitimisho
Ili kujiunga na chuo cha utalii kampasi ya Mwanza lazima uwe na sifa na vigezo tulivyovitaja hapo juu, chuo cha utalii kwa kampasi ya mwanza kinapatikana katika mkoa wa Mwanza na kinauwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 500 kwa mwaka katika kozi mbali mbali kwa ngazi ya cheti na diploma kwa NTA level 4,5 na 6.
Kwa taarifa zaidi unaweza tembelea tovuti ya chuo cha utalii kampasi ya mwanza kupitia linki hii nct.ac.tz/mwanza
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Utalii Dar es Salaam
2. Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Utalii Temeke
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku