Jinsi ya kujisajiri Na Baraza la Sanaa la Tiafa (BASATA)
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Jinsi ya kujisajiri Katika Baraza la Sanaa la Tiafa (BASATA), jinsi ya kujisajiri BASATA, Habari mwana habarika24, karibu tena katika makala hii fupi ambayo itaenda kukupa maelekezo ya msingi jinsi ya kujisajili Basata.
Kama wewe ni msanii basi makala hii ni ya muhimu sana kwa upande wako kwani kujisajiri BASATA ni swala la kisheria na linaumuhimu wa hali ya juu kwa msanii kama vile kulinda haki miliki ya kazi ya msanii.
Jinsi ya kujisajiri Na Baraza la Sanaa la Tiafa
Kuhusu Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ni Shirika la umma lililoundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 23 ya Mwaka 1984 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 5 ya Mwaka 2019. Historia inaonyesha kuwa, Sheria ya kuunda upya Baraza hili ilifanywa kwa kuunganishwa Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa ya Mwaka 1974 na Baraza la Muziki la Taifa (BAMUTA) ya Mwaka 1974. Baraza liliundwa ili lisimamie maendeleo ya sanaa nchini
Kazi za Baraza la Sanaa la Tiafa (BASATA)
Kwa mujibu wa Sheria Na. 23 ya mwaka 1984 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 5 ya Mwaka 2019, ambayo kwayo Baraza liliundwa, Majukumu ya Baraza ni pamoja na :
- Kufufua na kuhimiza maendeleo ya kazi za Sanaa
- Kufanya tafiti wa masuala mbalimbali ya Sanaa
- Kutoa ushauri na misaada ya kitaalamu kwa asasi au watu wanaojihusisha na shughuli za sanaa.
- Kuratibu shughuli za sanaa zinazofanywa na watu au Taasisi mbalimbali
- Kutoa na kuimarisha mipango ya mafunzo kwa Wadau wa Sanaa
- Kuishauri Serikali juu ya mambo yahusuyo maendeleo na uzalishaji wa kazi za Sanaa.
- Kuhamasisha maendeleo ya Sanaa kwa njia ya Maonyesho, Mashindano, Matamasha, Warsha na Semina.
- Kuanzisha, kukusanya na kuhifadhi torwi, ikiwa pamoja na zile zinazohusu watu, Asasi, Taasisi, vifaa na miundo mbinu inazohusiana na Sanaa
- Kusajili Wasanii na wale wote wanaojihusisha na shughuli za Sanaa
Jinsi ya kujisajiri Katika Baraza la Sanaa la Tiafa (BASATA)
Ili uweze kujisajili na balaza la sanaa la Taifa unapaswa kufuata baadhi ya hatua kwani hufanywa kwa kujaza fomu ya maombi ya kujiunga na baraza hilo
Kupata Fomu ya Maombi ya Usajili
Hatua ya kwanzani ni kuhakikisha unapata form ya mamombi ya usajili kutoka BASATA. Fomu ya maombi ya usajiri inaweza kupatikana kwa njia mbili tofauti
- Njia ya kwanza ni kupitia tovuti ya balaza la sanaa la Taifa BASATA, ingia kwenye tovuti ya BASATA kisha pakua fomu ya maombi kisha chapisha fomu hiyo tumia linki hii basata.go.tz
- Njia ya pili tembelea ofisi za basata zilizopo eneo lako na omba fomu ya maombi ya usaji
Jaza fomu ya Maombi ya Usaji
Ukisha kua na fomu ya maombi ya usajili sasa utatakiwa kujaza taarifa zinazo hitajika kulingana na maelezo ya bfomu. Hkikisha unajaza taarifa zote za msingi kwa usahihi na hupaswi kudanganya kwa njia yoyote ile.Jazaa taarifa kama vile
- Taarifa binafsi- jina, jinsia, mwaka wa kuzaliwa
- Jaza aina ya sanaa unayoifanya
Na utahitajika kujaza taarifa nyingine kulingana na maelekezo ya fomu.
Rudisha Fomu ya Maombi ya Usajiri Katika Ofisi za BASATA
Baada ya kuhakikisha umejaza fomu kwa umakini na taarifa zote za msingi sasa utatakiwa kuirudisha fomu hiyo kwenye ofisi za BASATA zilizopo karibu yako. Pindi utakapo rudisha fomu hiyo hakikisha unaambatanisha na nyaraka muhimu ambazo zitakuwa zimetajwa katikia fomu ya maombi
Subili Majibu ya Usajiri
Baada ya kurudisha fomu basi mchakato wa usajili utaanza mara moja, hivyo itakubidi kusubiri taarifa za zoezi lako la usajiri kutoka katika ofisi za BASATA. Kama kutakua na changamoto kwenye taarifa zako basi utapokea ujumbe kutoka BASATA ili kufanya marekebisho na kama hakuna changamoto basi Utasubili uthibitisho wa usajili wako.
Umuhimu wa Usajili BASATA
Kuna faida nyingi sana kwa msanii wa sanaa ya aina yoyote ile pindi anapojisajiri na Balaza la Sanaa laTaifa (BASATA), Hapa tumeweka baadhi ya faida za kujisajiri BASATA
1. Utambulisho wa Msanii
BASATA hutoa utamburisho kwa msanii mara baada ya kukamilisha usajiri wake. Usajiri wa msanii kwenye baraza la sanaa la Taifa humfanya msanii na kazi yake kutambulika kisheria.
2. Kupata Mafunzo.
Wasanii walioko chini ya usajili wa baraza la sanaa la Taifa BASATA huwa na nafasi za kujiunga na mafunzo mbali mbali yanayotolewa na baraza hilo la sanaa la Taifa
3. Ulinzi wa Kazi za Msanii
BASATA husaidia katika kutoa ulinzi kwa kazi zote za wasanii ambao tayari wameweza kujisajili katika mfumo wao, ikiwemo pamoj na kuzuia umiliki wa kazi kutok kwa wezi wa umiliki wa kazi hizo.
Hitimisho
Kama wewe ni msanii wa aina yoyote basi ili uwe huru katika kazi zako za kisanaa ni vyema ukahakikisha unajisajiri na baraza la Sanaa la Taifa kwa uhalali na ulinzi wa kazi zako.
Mapendekezo ya Mhariri;
2. Bei ya Tiketi ya Treni Kutoka Dar es Salaam kwenda Arusha
3. Mshahara Wa Mwalimu wa Shule Ya Msingi
4. Mshahara Wa Mwalimu Wa Diploma Ya Sekondari
5. Afisa Maendeleo ya Jamii na Majukumu Yake
7. Vigezo na Sifa za Kujiunga JKT Mujibu Wa Sheria
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku