Afisa Maendeleo ya Jamii na Majukumu Yake
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Afisa maendeleo ya Jamii, Huyu ni mtendaji katika jamii ambaye kazi yake kuu ni kusimamia na kuhakikisha utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo kakita jamii husika.
Afisa maendeleo ya jamii hufanya kazi kwa kuasidia na watu pamoja na jumuia nyingine ili kuhakikisha mipango yote ya maendeleo katika jamii inafanikiwa kwa uykarobu. Mfano afisa maendeleo ya jamii hushirikiana na
- Serikali
- Wanajamii
- Taasisi zisizo za kiserikali
Hivyo basi kwa Tanzania kila almashauli ya wilaya au mkoa huwa na afisa maendeleo yake akiwa na jukumu moja tu la kuhakikisha mipango ya maendeleo katika almashauri hiyo inafanikiwa.
Hapa tutaenda kutoa maelezo ya kina juu ya majukumu na umuhimu wa kuwa na afisa maendeleo ya jamii katika jamii zetu
Umuhimu wa Afisa Maendeleo ya Jamii
Afisa maendeleo ya jamii anaumuhimu mkubwa sana katika jamii zetu, na hapa ni miongoni mwa sababu za kuwa na afisa maendeleo ya jamii
1. Kuhimiza Ushirikiano katika Jamii
Maafisa jamii husaidi kwa kiasi kikubwa kuhimiza ushirikiano miongoni mwa mwanajamii kitu ambacho husaidia kwenye mipango ya kimaendeleo kuweza kunanikiwa
2. Kuchochea Uwelewa Kwa Wanajamii
Maafisa maendeleo ya jamii hutumia nasafi zao kuweza kuufahamisha uma/jamii kuweza kuwa na uwelewa juu ya rasilimali mabli mbali zilizpo katika jamii husika na jinsi ya kuzitumia ili kuhakikisha maendeleo maendeleo ya jamii hiyo yakikamilishwa.
3. Kuhakikisha kuwepo kwa maendeleo ya kweli katika Jamii.
Hii ndio kazi kuu ya maafisa maendeleo ya jamii, uwepo wao husaidia mipango ya kimaendeleo katika jamii inakamilishwa kwa ustawi wa jamii hiyo.
Majukumu ya Afisa Maendeleo ya Jamii
Hapa chini tutaenda kukuonyesha baadhi ya kazi amabzo afisa maendeleo ya jamii anazifanya katika jamii yake, kumbuka huyu ndio msimamizi mkuu wa mipango yote ya kimaendeleo katika jamii husika
Kuhamasisha Jamii
Baada ya kuwepo kwa mipango ya kimaendeleo swala la utekelezwaji hufanywa na wanajamii hivyo basi afisa maendeleo ya jamii jukumu lake ni kuhakikisha ana ushawishi umma na kuwahamasisha ili kushiriki katika utekerezaji wa mipango yote iliyowekwa ya kimaendeleo.
Kusimami Miradi ya Maendeleo
Maafisa maendeleo ya jamii ni kazi yao kuhakikisha miradi yote ya kiamendeleo iliyopo katika jamii inatekelezwa ipasavyo katika nyanja mbali mbali kama vile
- Kijamii
- Kiuchumi
- Kiutamaduni
Kutoa Elimu Kwa Jamii:
Ni jukumu la afisa maendeleo ya jamii kuhakikisha wanajamii wanaelimu ya kutosha juu ya matumizi ya rasilimali zilizopo katika jamii yao kwa leongo la kujiletea maendeleo, pia kuwapa elimu juu ya maswala mbali mbali kama vile
- Jinsia
- Elimu
- Afya
Ukusanyaji Wa Taarifa za Kimaendeleo
Ni wajibu wa afisa maendeleo kuhakikisha anakusanya taarifa mabli mbali katika jamii yake ili kuhakisha upandaji wa uboreshaji jamii hiyo. Taarifa hizo hutumika katika mipango ya maendeleo ya jamii
Usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
Shughuli ya usajili wa msahirika binafsi yasiyo ya kiserikali (NGos) husimamiwa moja kwa moja na afisa maendeleo wa jamii. Pia kuhakikisha ufanyaji kazi wake katika ustawi wa maendeleo ya jamii.
Hitimisho
Afisa Maendeleo ya jamii ni nafasi ya muhimu sana katika jamii na nchi kwa ujuma kwani hawa ndio watendaji wakuu katiuka ngazi ya jamii katika kuhakikisha sera na mipango ya kimaendeleo inayowekwa ma serikali kuu inasimamiwa na kutekelezwa kwa ukaribu zaidi katika ngazi ya jamii.
Ili maendeleo yaweze kutokea inahitaji watendakazi na wasimamizi ambao ni maafisa maendeleo ya jamii
Kwa maelezo zaidi unaweza tembelea Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum(WMJJWM )
Mapendekezo ya Mhariri;
2. Bei ya Tiketi ya Treni Kutoka Dar es Salaam kwenda Arusha
3. Mshahara Wa Mwalimu wa Shule Ya Msingi
4. Mshahara Wa Mwalimu Wa Diploma Ya Sekondari
5. Viwango Vipya Vya Mishahara ya Walimu Serikalini
7. Ratiba ya Treni Dar es Salaam Kwenda Arusha
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku