Jinsi Ya Kuangalia usajili wa kampuni BRELA
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Kuangalia usajiri wa kampuni Brela, Namna ya kuangalia usajili wa kampuni BRELA, Habari za wakati huu mwana Habarika24, Karibu tena katika makala hii ambayo itaenda kukuelezea kindani zaidi juu ya njinsi ya kuangalia usajili wa kampuni BRELA
Kama ulifanya ombi la usajiri wa kampuni BRELA na huna uhakika kama usajili wako umekamilika au la basi unaweza kutumia njia ya usajili wa mtandao (ORS) ili kuweza kutazama usajili wa kampuni yako.
BRELA imeweza kurahisisha huduma zake hasa katika kuangalia usajili wa kampuni kwa kuanzisha mfumo wa mtandao ambao unawapa nafuu wateja wke kuweza kuangalia taarifa muhimu za usajili wa kampuni zao kupiti mfumo wa ORS (Online Legislation System)
Hivyo basi katika makala hii tutaenda kukuonyesha hatua za kufuata ili uweze kuangalia usajili wa kampuni yako BRELA.

Jinsi Ya Kuangalia usajili wa kampuni BRELA
Hapa chini tunaenda kukuonyesha hatua za kufuata ili kuangalia usajili wa kampuni yako BRELA;
1. Jisajiri katika Mfumo wa ORS wa BRELA
Kwanza kabisa itakupasa kwenda kufungua akaunti yako katika mfumo wa BRELA wa Online legislation System
– Ili kufanya hivyo ingia kwenye internet kupitia kifaa chako kwa kutumia linki hii hapa ors.brela.go.tz
Mara baada ya mfumo kufunguka kama unavyonekana hapo juu nenda sehemu palipoandikwa tengeneza akaunti ya ORS na bonyeza hapo jaza taarifa zinazohitajika na utakua umesha fungua akaunti.
2. Ingia kwenye Akaunti yako ya ORS
Baadaya kutengeneza akaunti sasa ingia kwenye akaunti yako ya ORS ambayo umeitengeneza ili kuanza mchakato wa kuangalia usajili wa kampuni yako.
3. Tafuta Kampuni
Ukiwa ndani ya akaunti yako ya ORS nenda sehemu palipo andikwa utafutaji wa bure kisha na ubonyeze hapo , ukrasa wa taarifa muhimu za kujaza utafunguka. Igiza namaba ya usajil na jina la kampuni na sehemu ya aina ya kitu bonyeza kampuni kisha bonyeza kitufe cha tafuta.
4. Soma maelezo Ya Usajili
Mara baada ya kubonyeza kitufe cha kutafuta mfumo utatoa taarifa zote muhimu juu ya usajili wa kampuni taarifa kama vile
- Hari ya usajili
- Tarehe ya Usajili
- Jina la kampuni
- Wshirika katika kampuni na uongozi wake
5. Pakua Taarifa za usajiri
Baada ya kusoma na kuona hali ya usajili wa kampuni yako sasa unaweza kupakua taarifa hizo na kuzichapisha kwa mahitaji ya siku zijazo.
Hitimisho
ORS ni mfumo wa kimtandao uliochini ya usimamizi wa BRELA ukiwa na lengo la kuwawzesha wamiliki wa kampuni waliofanya usajili wa kampuni zao BRELA kuweza kuangalia hali ya usajili wa kampuni zao, Ikiwa umepata changamoto yoyote au unahitaji taarifa zaidi na maelezo ya ziada tafadhari unaweza tembelea ofisi yoyote ile ya BRELA iliyoko kari na wewe.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Nauli ya Boti Dar es Salaam Kwenda Zanzibar
2. Mshahara wa Usalama wa Taifa
3. Vifurushi vya Starrtimes Na Bei Zake
4. Mafunzo Ya Usalama Wa Taifa Tanzania
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku