Jinsi ya Kukopa Salio La Nipige Tafu Vodacom Tanzinia
Jinsi ya Kupa salio la Nipigie Tafu, Karibu tena katika makala hii, leo tutaenda kukuelekeza namna ya kukopa salio la nipige tafu kwenye mtandao wa vodacom Tanzania. Kam wewe ni mtumiaji wa laini ya Vodacom na bado hujajua jinsi ya kukopa salio la nipige tafu vodacom.

Mtandao Wa Vodacom
Vodacom ni moja miongoni mwa makampuni yanayotoa huduma za mawasiliano ya simu inchini Tanzania. Kama wewe si mttumiaji wa mtandao wa vodacom katka nyanja ya mawasiliano basi tambua ya kua mtandao huu ni miongoni mwa makampuni boraz zaidi nchini Tanzania katika utoaji wa huduma za kimawasiliano. Mfano wqa huduma zitolewazo na kampuni ya Vodacom ni pamoja na;
- Huduma ya mawasiliano ya simu ( kupiga na kupokea simu)+Huduma ya Kutuma na kupokea pesa kupitia M Pesa
- Huduma ya kutuma mseji
- Huduma ya Internet
- Huduma ya kulipia bili na maripo ya serikali
Jinsi ya Kukopa Salio La Nipige Tafu Vodacom
Vodacom kama mtandao mkubwa zaidi Tanzania katika kutoa huduma za kimawasiliano basi pia inawajali wateja wake kwa kuhakikisha inatoa huduma bora na hata kuwasaidia kwa kuwapa mkopo wenye riba nafuu zaidi pale wanapokua na upugusu wa salio na mkopo huo unatambulika kama nipige tafu.Hivyo basi hapa tunaenda kukuelekeza jinsi ya kukopa salio la nipige tafu vodacom.
Vigezo na Masharti ya Kukopa Salio la Nipige Tafu Vodacom
Ili kupata mkopo huo lazima uweze kukidhi vigezo na masharti yafuatayo;
- Kwanza uwe mtumiaji wa Vodacom
- Laini yako iwe imesajiliwa kwa mfumo wa alama za vidole
- Uwe umetumia laini ya vodacom si chini ya mwezi mmoja na zaidi bila kuitoa kwenye simu
- Uwe mtumiaji au mnunuaji wa vifurushi vya vodacomu na utarati wa kuongeza salio mara kwa mara
- Uwe na utarati wa kurejesha malipo ya mkopo wako ndani ya muda husika
Baada ya kukidhi vigezo hapo juu sasa unaweza kua miongoni mwa wateja wa vodacom ambao wanaweza kupatiwa mkopo wa salio wa nipige tafu kupitia laini zao za vodacom, ili kupata mkopo huo tafadhari fuata hatua hizi hapa chini;
- Ingia kwenye simu yako na upige *149*01*99#
- Kisha chagua nipige tafu
- Chagua kiasi unachotaka kukopa kutoka kwenye orodha
- Baada ya hapo bonyeza thibitisha ombi lako
Baada ya kufuata hatua hizo hapo juu utapokea ujumbe ambao utaonyeza kua umepokea kiasi flani cha mkopo wa nipige tafu na kiasi cha jumla unachotakiwa kulipa kwa ujumla wake.
Jinsi ya Kuangalia Kiwango Chako cha Mkopo au Deni la Nipige Tafu
Kupitia vodacom nipige tafu mteja wa vodacom anaweza kuangalia ni kiasi gani anaweza kukopa kabla ya kukopa au ni deni kiasi gani analodaiwa. Kutazama kiwango cha mkopo wako au dani lako tafadhari fuata hatua hizi hapa chini;
- Ingia kwenye menu ya simu yako
- Bonyeza *149*01#
- Kisha chagua “Nipige Tafu”
- Kisha chagua salio la mkopo
Mapendekezo ya Mhariri
1. Jinsi ya Kukopa Salio Airtel
2. Jinsi ya Kukopa Salio Tigo Haraka na Rahisi