Nafasi Mpya Za Kzi Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Newala Agosti 2024
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala kupitia kibali cha ajira mpya chenye kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024, chenye nafasi ya Mtendaji wa Kijiji Daraja La III (8) na Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II (5) kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Hivyo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Newala anatangaza nafasi za kazi na
anakaribisha maombi kwa watanzania wenye sifa za kujaza nafasi hizo kama ifuatavyo: –

MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III NAFASI 8
MAJUKUMU YA KAZI
i. Afisa Masuuli na Mtendaji mkuu wa Serikali ya Kijiji.
ii. Kuratibu na kusimamia Upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo
ya kijiji
iii. Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
iv. Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na taratibu
v. Kuandaa taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha Wananchi katika kuandaa na kutekeleza Mikakati ya kuondoa njaa, Umaskini na kuongeza Uzalishaji mali.
vi. Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaaluma katika kijiji
vii. Kusimamia ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika kijiji.
viii. Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijiji.
ix. Mwenyekiti wa kikao cha Wataalam waliopo katika kijiji.
x. Kupokea, kusikiliza na kutatua Malalamiko na Migogoro ya Wananchi.
xi. Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo za Kijiji na atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
xii. Kusimamia ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye elimu ya Kidato cha nne au sita, aliyehitimu Mafunzo ya Astashahada/ Cheti (NTA LEVEL 5) Katika mojawapo wa Fani zifuatazo, Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa Kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali- TGS B1
BONYEZA HAPA KUSOMA NAFASI ZOTE
MACHAGUZI YA MHARIRI;
1. Jinsi ya Kupata Namba ya NIDA Kwa Njia ya SMS
2. Jinsi Ya Kuangalia Deni La Gari 2024 (TMS Traffic Check)
3. Namna ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Kwa Mtu Mzima
4. Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mtendaji wa Kijiji na Mtaa
5. Ada za Airtel Money 2023/2024 Kwenye Kutoa na kuweka Pesa
6. Ratiba ya treni za SGR Dar es Salaam na Morogoro