Sifa za Kujiunga na Chuo Cha CC (University of Dar es salaam Computing Centre ), Je umehitimu elimu ya sekondari kidato cha nne au kidato cha sita na unalengo la kusoma kozi ya IT Sifa za Kujiunga na Chuo Cha CC (University of Dar es salaam Computing Centre ) ?,basi usiwe na hofu hapa katika makala hii tunaenda kukupa mwongozo wa sifa na vigezo vya kuweza kujiunga na chuo cha CC (University of Dar es Salaam Computing Centre)
Kuhusu UCC
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Computing Centre (UCC) ni chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kinachomilikiwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Kituo cha kompyuta cha UCC kilianzishwa mnamo mwaka 1999. Makao makuu ya UCC yapo UDSM ya Julius Kambarage Nyerere kampasi ya Mlimani . Ili kuweza kutoa huduma zake kwa watanzania walio wengi, UCC pia ina tawi mkoani Dodoma Tanzania.
JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Kozi Zitolewazo na Chuo Kikuu cha Dar es salaam Computing Center
Chuo kikuu cha Dare es Salaam Computing Center kinatoa kozi za muda mfupi na zile za muda mrefu
Kozi za Muda Mfupi
Hapa chini ni miongoni mwa kozi za muda mfupi zitolewazo na chuo kikuu cha Dar es Salaam Computing Center
- ICDL,
- Graphic design,
- Website development,
- Database administration
Kozi za Muda Mrefu
Chuo kikuu cha Dar es Salaam Computing Center kinatoa kozi mbali mbali katika ngazi ya cheti na Diploma kama vile
- Cheti na Diploma ya Kompyuta na Teknolojia ya Habari na Teknolojia ya Maendeleo ya Biashara.
Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha UCC (University of Dar es salaam Computing Centre )
Hapa chini tutaenda kukuonyesha sifa na vigezo ambavyo mwombaji anatakiwa kua navyo ili kuweza kujiunga nakituo cha kompyuta cha chuo kikuu cha Dar es Salaam UCC (University of Dar es salaam Computing Centre )
Sifa za Kujiunga na Kozi za Ngazi ya Diploma (Stashahada)
Ili kuweza kujiunga na kozi zitolewazo katika chuo cha UCC kwa ngazi ya diploma mwombaji anapaswa kua na sifa zifuatazo
- Mwombaji anapaswa awe na elimu ya sekondari kidato cha sita
- Mwombaji anapasw kua na Pass 1 na creadit 1 kwenye cheti cha ACSEE
- Au mwombaji awe na cheti cha msingi cha ufundi (NTA Level 4) katika sayansi ya kompyuta (CS), Teknolojia ya Habari (IT), Teknolojia ya Habari ya Biashara (BIT) au nyanja nyingine zinazohusiana kutoka kwa taasisi inayotambulika.
Sifa za Kujiunga na Kozi za Ngazi ya Cheti
Ili mwombaji aweze kukubaliwa kujiunga na kozi yoyote ile katika kituo cha kompyuta cha chuo kikuu cha Dar es Salaam lazima awe na sifa na vigezo vifuatavyo;
- Mwombaji anapaswa awe na elimu ya kidato cha nne
- Awe na cheti chenye ufaulu wa anagalu wa pass nne kwenye masomo yake ukitoa masomo ya dini
- Awe na tuzo ya Taifa ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Level III (Daraja la Mtihani wa Biashara). I) kutoka taasisi yoyote inayotambulika.
- Awe na Cheti cha Mtihani wa Kitaifa wa Biashara Hatua ya I na kufaulu wa pass 2.
Kwa msaada zaidi wa kujua juu ya sifa na vigezo vya kuweza kujiunga na kozi zitolewazo katika kituo cha kompyuta cha chuo kikuu cha Dar ws Salaam basi unaweza kuwasiliana nao kwa mawasiliano hapa chini
Anuani
- University of Dar es Salaam, Mlimani Road
- P.O. Box. 35062 Dar es Salaam, Tanzania
- Email: [email protected]
Mawasiliano ya Simu
- +255 22 2410641/5
- +255 22 2410690
- +255 754782120
Mapendekezo ya Mhariri:
1. Vigezo Na Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Mweka
2. Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Diplomasia
3. Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha DUCE Entry Requirements
4. Sifa za Kujiunga Archbishop Mihayo University College of Tabora
5. Vigezo Na Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Ardhi Dar es Salaam