Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Mweka
Ikiwa tayari umehitimu elimu ya sekondari ngazi ya kidati cha sita na kutunukiwa cheti cha ACSEE chenye ufauru na kuhitaji kujiunga na kozi yoyote ile kutoka chuo cha usimamizi wanyamapori Afrika cha KWEKA basi ni bora ukasoma nankufahamu sifa na vigezo vinavyohitajika ili kuweza kujiunga na chuo hicho cha KWEKA
Hapa chini tumekuwekea sifa za kujiunga na chuo cha kweka kwa kila ngazi ya kozi itolewayo na chuo hiki
Sifa za kujiunga na Kozi ya Usimamizi Wanyamapori Ngazi ya Digrii (Bachelor Degree in Wildlife Management)
– Mwombaji awe na Principle pass 2 kwenye masomo ya biolojia,kemia fizikia,jiografia,kilimo,lishe, Hisabati ya juu (advance mathematics), Zoolojia, Botonia au Mazingira
Sifa za Kujiunga na Kozi ya Utarii wa Wantamapori Ngazi ya Digrii ( Bachelor Degree in Wildlife Tourism)
– Mwombaji anapaswa kua na elimu ya kidato cha sita na kutunukiwa cheti cha ACSEE chenye ufaulu wa principle pass 2 kwenye masomo ya Biolojia, Kemia, Fizikia, Jiografia, Kilimo, Lishe, Hisabati ya Juu ( Advanced Mathematics), Biashara, Uchumi, Historia, Lugha ya Kiingereza, Mazingira, Utalii, Jiografia ya Utalii, Ujasiriamali wa Masoko au Masoko ya Utalii.
Sifa za kujiunga na Kozi ya Usimamizi Wanyamapori Ngazi ya Diploma ya Kawaida (Ordinary Diploma In Wildlife Management)
– Mwmbaji anapaswa kua na Cheti cha Fundi (NTA Level 5) katika Usimamizi wa Wanyamapori.
– Cheti cha Fundi (NTA Level 5) katika Utekelezaji wa Sheria ya Wanyamapori kutoka taasisi zinazotambuliwa na NACTE.
Sifa za Kujiunga na Kozi ya Utarii wa Wanyamapori Ngazi ya Diploma ya Kawaida (Ordinary Diploma In Wildlife Tourism)
– Mwombaji anapaswa kua na Cheti cha Fundi (NTA Level 5) katika Utalii wa Wanyamapori.
– Cheti cha Ufundi (NTA Level 5) katika Mwongozo wa Watalii kutoka taasisi zinazotambuliwa na NACTE.
Sifa za kujiunga na Kozi ya Usimamizi Wanyamapori Ngazi ya Cheti cha Msingi cha Ufundi (Basic Technician Certificate In Wildlife Management)
– Mwombaji inampasa awe na cheti cha sekondari chenye ufaulu usiopungua pass 4 katika masomo ya Biolojia, Kemia, Fizikia, Jiografia, Hisabati, Kilimo, Kiingereza, Lishe.
-Tuzo III katika Mafunzo ya Ufundi Stadi kwenye Mifugo, Uvuvi, Kilimo, Ufugaji Nyuki na Misitu kutoka taasisi zinazotambuliwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).
-Waombaji wanaoomba kutumia VTA III lazima wawe wamepata ufaulu wa pass 4 katika Cheti cha Elimu ya Sekondari kidato cha nne (CSEE).
Mapendekezo ya mhariri:
Sifa za Kujiunga Archbishop Mihayo University College of Tabora
Vigezo Na Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Ardhi Dar es Salaam
Sifa Za Kujiunga Na Arusha Technical College
Sifa Za Kujiunga Na Chuo cha ardhi Tabora ARITA 2024/2025