NAFASI 300 za Sales Officers Kutoka Hope Holdings September 2025
Kampuni ya Hope Holdings, inayojihusisha na biashara mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwemo Mgahawa wa Papparoti, Supermarket ya kuuza mazulia iitwayo Amal Carpets (Mlimani City), pamoja na maduka ya FLO, Bottega Verde, Flormar, Skechers, Defacto na LC Waikiki, inatangaza nafasi za ajira kwa vijana 300 wa kiume watakaoajiriwa kama Maafisa Mauzo (Sales Officers) katika maduka ya AMAL CARPETS.
Vigezo vya Waombaji
-
Awe mhitimu wa chuo.
-
Awe na Diploma ya Utawala wa Biashara, Masoko na Mauzo au kozi yoyote ya biashara inayohusiana.
-
Awe na uzoefu wa angalau mwaka mmoja katika biashara ya rejareja (retail).
-
Awe mwanaume.
-
Awe na ujuzi mzuri wa mawasiliano pamoja na ujuzi wa mauzo.
Taarifa Muhimu
-
Usaili (interview) utafanyika kwa siku mbili: Septemba 16 na Septemba 17, kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana.
-
Waombaji wote wanatakiwa kufika Ofisi za Hope Holdings zilizopo Morocco Square Mall (jirani na taa za Morocco, Kinondoni – ghorofa ya pili) wakiwa na:
-
CV zao
-
Nakala za vyeti vyao
-
Nakala ya kitambulisho cha NIDA
-
Leave a Reply