MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Karatu District Council September 2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu anapenda kuwataarifu Waombaji wote wa nafasi
za kazi zilizotangazwa kwenye Tangazo lenye Kumb Na. KDC/DED/S.1/58/VOL.I/211 la tarehe 13/06/2025
na kuomba kupitia Mfumo wa “ajira Portal” kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe
15/09/2025 hadi 18/09/2025 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi watakaofaulu usaili huo.Wasailiwa
wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo
usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
2. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi
3. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga
kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.
4. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI,
Astashahada na Stashahada kutegemeana na sifa za Mwombaji.
5. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza
matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA
HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
6. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
7. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
8. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na
Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
9. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi
vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya
tangazo husika.
10. Kwa kada ya Udereva na wenye Sifa za Daraja C au E wanapaswa kuwasilisha vyeti halisi vya
kujipatia Madaraja husika pamoja na Leseni ambazo hazijaisha muda wake.
11. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba
ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili
12. Wasailiwa wote mnajulishwa kuwa hali ya hewa ya Halmashauri ya Wilaya ya Karatu ni ya baridi kwa
kipindi hiki, hivyo mnashauriwa kuvaa nguo zinazohimili hali ya hewa ya ubaridi.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA MAJINA
Leave a Reply