Nafasi Mpya 18 Za Kazi Kutoka Halmashauri Ya Wilaya Ya Tunduru Agosti 2024
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kupitia kibali cha ajira mpya chenye kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 chenye Kada za Msaidizi wa kumbukumbu Daraja la II nafasi nne (4), Mtendaji wa kijiji Daraja la III nafasi kumi na moja (11) na Dereva Daraja la II nafasi tatu (3), kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tunduru anawatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa watanzania wote wenye sifa na kuleta maombi ya kazi kwa nafasi zilizoainishwa hapo chini.-
MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II – NAFASI 4
MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista
ii. Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi kwenye rejista
iii. Kusambaza majalada kwa watendaji Kupokea
iv. Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa watendaji.
v. Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji.
vi. Kurudisha majalada kwenye Shubaka/kabati la majalada au mahali pengine
yanapohifadhiwa
vii. Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi
SIFA ZA MWOMBAJI:
Awe na Elimu ya kidato cha Nne (IV) au cha Sita (VI) aliehitimu mafunzo ya
stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya Utunzaji wa kumbukumbu kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.
NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi ya Mshahara wa Serikali – TGS C1 kwa mwezi.
Download PDF HAPA
Mapendekezo ya mhariri:
1. Jinsi Ya Kuangalia Salio La NSSF Kwa Njia ya Simu
2. Jinsi Ya Kulipia King’amuzi Cha Azam Tv
3. Jinsi ya Kujiunga na Mfumo wa Maombi ya Ajira TAMISEMI