Mkurugenzi wa Mji Kasulu amepokea kibali cha ajira mpya kwa Ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora chenye Kumbu Na. FA.228/613/01/C/021 cha tarehe 25 Juni, 2024. Hivyo watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi
zifuatazo;
MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (NAFASI 2)
JIUNGE NA WHATSAPP CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA WHATSAPP GROUP LETU HAPA,
MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuchapa barua, taarifa au nyaraka za kawaida na za siri.
ii. Kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao na kuwaelekeza wanapoweza
kusaidiwa .
iii. Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miradi, tarehe za vikao, safari
za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine.
iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika Utekelezaji wa majukumu
ya kazi
v. Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika
Idara/Vitengo/Sehemu husika.
vi. Kukusanya, Kutunza na Kuyarejesha Majalada na nyaraka sehemu
zinazohusika.
vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali.
viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
SIFA ZA MWOMBAJI
- Kuajiriwa mhitimu wa Kidato cha IV au kidato cha VI wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powerpoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi ya Mishahara ya Serikali ni, TGS C.
Mapendekezo ya mhariri:
1. Jinsi Ya Kuangalia Salio La NSSF Kwa Njia ya Simu
2. Jinsi Ya Kulipia King’amuzi Cha Azam Tv
3. Jinsi ya Kujiunga na Mfumo wa Maombi ya Ajira TAMISEMI
4. Jinsi ya Kupata Namba ya NIDA Kwa Njia ya SMS
5. Jinsi Ya Kuangalia Deni La Gari 2024 (TMS Traffic Check)