Jinsi Ya Kuhakiki Bima Ya Gari Lako Haraka Zaidi
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Jinsi Ya Kuhakiki Bima Ya Gari Lako Haraka Zaidi, Kama wewe ni mmiliki wa chombo cha moto aina ya gari basi nimuhimu kujua nakua na bima ya gari yako kwani ni kinga muhumu sana kwenye umiliki wa gari yako.TIRA ndio mamlaka yenye dhamana ya usimamizi wa Bina Tanzania ambayo inaendeshwa chini ya sheria ya bima Na. 10 ya mwaka 2009. Kazi ya TIRA ni kusimamia na kuhakiki uhalali wa bima za magari.
Wewe kama mliki wa gari kuwa na bima ya gari lako kwanza kabisa ni kutii sheria ya nchi lakini pia nimuhimu sana gari yako kua na bima kwani hukuepusha na hasara inayoweza kujitokeza pasipo ya wewe mmlikiwa Chombo hicho kutarajiakutokana na mbambo kadha wa kadha kama vile kuibiwa, ajiali au hata uharibifu wowote ule wa gari yako. Iweke akilini kua bima huwa na muda maalumu na ndani ya muda huo ndio uhalali na matumizi yake hufanyika, endapo muda wake ukaisha pia hata matumizi yake husitishwa hivyo basi kumbuka kuangalia uhalali wa bima yako kila baada yam da furani ili kukwepa hasara ya kimatumizi ya kifedha pindi changamoto yoyote ile inapo jitokeza.

TIRA kama mamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania ikishirikiana na makampuni yanayotoa bima wamejaribu kufanya mfumo wa uhakiki wa uhalali wa bima ya gari kua rahisi ili kuwapa wamiliki wa magari fursa ya kuhakiki uhalali wa bima wanazozimiliki kwa wepesi zaidi kuepuka usumbu wa aina mbali mbali pindi bima zao zitakapokwisha mda wake.
Jinsi Ya Kuhakiki Bima Ya Gari
Kama unahitaji kuhakiki uhaali wa bima yako basi tambua kua mamlaka zinazohusika zimeweka njia tofauti tofauti ambazo unaweza zitumia ili kuhakiki taarifa za uhalali wa bima ya gari yako. Miongoni mwa njia hizo ni pamaoja na;
- Wavuti za kampuni za bima
- Portal za serikali kama TANROADs na TIRA
- Pia kwa kufika ofisi za bima
Njia hizo hapo juu zinatofautiana kimatumizi au kanuni na miongozo yake katika kuzitumia ili kuhakiki bima yako, hivyo basi wewe kama mtumiaji wa bima ni jambo la muhimu kuweza kuzifahamu mwongozo na matumizi yake kimsingi.
Hivyo basi kama kichwa cha Makala hii kinavyoeleza, tutaenda kukuelekeza mambo mbali mbali kama vile kunaumuhimu gani kuwa na bima ya gari yako,ni njia gani rahisi unaweza kuitumia katika kuhakiki uhalali wa bima ya gari yako pia tutaenda kukuelekeza mambo ya msingi ya kufanya pale bima yako itakapokua imeisha uhalali wake.
Kwanini Unatakiwa kuhahiki uhalali wa Bima ya Gari? /Umuhimu wa Kuhakiki Uhalali wa Bima ya Gari
Kuhakiki uhalali wa bima ya gari ni jambo la msingi kwa wamiliki wa magari nchini Tanzania kutokana na sababu kadhaa muhimu:
Mapendekezo
Kama tulivyosema hapo awali, kwa mliki yoyote yule wa gari ni muhimu sana kwako kuwa na bima ya gari lako na kuhakikisha unafanya uhahakiki wa uhalali wa bima hiyo kutokana na sababu zifuatazo za kimsingi zaidi;
1. Sababu za Kisheria
Kuwa na bima ya gari si jambo la hiyali bali ni jambo la kisheria kwa maana sheria ya bima Na. 10 ya mnamo mwaka 2009 inaelekeza kua wamiliki wote wa magari wanapaswa kua na bima za magari yao tena zilizo halali. Kwani umiliki wa bima kwa milikiwa gari husaidia kuimalisha usalama kwenye Chombo chake na pia kwa watumiaji wa Barabara na mali zao, Hivyo basi licha ya mmiliki wa gari kuwa na bima ya gari yake lakini pia anapaswa kua anahakiki uhalali wa bima yake.
2. Kuepuka Hasara Za Kifedha Zinazoweza Jitokeza
Mmliki wa gari kua na bima ya gari lake inampa ulinzi wa matumizi ya fedha zake katika gari lake pindi linapopatwa na changamoto yoyote ile kama ajali,kuibiwa kwa gari au uharibifu wowote ule utakao tokea. Bali bima inatoa usalama kwani pindi tukio lolote lile litakapo toke abasi bima itatumika kulipa gharama zote na kumuach huru mmliki wa gari hilo pasipo kutumia hata senti moja ya fedha zake.
3.Kuepuka Adhabu na Faini
Bima ilianzishwa kisheria na pia ni miongoni mwa sheria kwa wamiliki wa magarikua na bima hiyo, hivyo basi mmliki yoyote yule wa gari anapaswa kua na bima ya gari lake kinyume cha hapo anaweza kukumbana na adhabu au faini kutoka kutoka kwnye mamlaka za barabarani hata kuwekewa kizuizi kwenye matumizi ya gari hilo. Tabi ya mara kwa mara ya mmliki wa gari kuweza kuhakiki uhalali wa bima ya gari lake unaweza kumfanya kuwa salama kutoka kwenye mikono ya sheria.
Jinsi Ya Kuhakiki Bima Ya Gari
Kama wewe ni mmiliki wa chombo cha moto Tanzania hususani gari na unatafuta njia ya kuhakiki uhalali wa bima ya gari lako, basi hapa tumekusanya taarifa zote unazohitaji kujua ili kuhakiki bima ya gari lako online.
Kutokana na maendeleo ya kiteknolojia mamlaka zinazohusika na usimamizi wa bima za magari zimeweza kumlahisishia mmliki wa bima ya gari kuweza kufanya uhakiki wa uhalali wa bima yake kwa njia ya kimtandao, kupitia kifaa chochote kile kinachoweza kuunganishwa na huduma ya intaneti kama vile simu aina ya smartphone, laptop au desktop kompyuta
Uhakiki wa Bima ya Gari Kwa Njia ya Mtandao
Ili Kuhakiki uhalali wa bima ya gari yako kwa njia ya mtandao tafadhari unaweza kufuata njia hizi hapa chi;
-Kupitia kifaa chako cha intaneti tafadhari fungua google
-Kiasha tembelea wavuti ya TIRA-MIS au bonyeza linki hii www.tiramis.tira.go.tz.
-Ukiwa kwenye ukrasa wa TIRA-MIS CHAGUA NJIA YA Uhakiki
Mara baada ya wavuti ya TIRA-MIS kufunguka kwenye bonyeza upande wa menyu na kisha njia mbali mbali za kufanya uhakiki wa bima ya gari yako zitafunguka na itakuhitaji kuchagua njia gani ambayo ungependa kuitumia kufanya uhakiki wa uhalali wa bima ya gari yako
Miongoni mwa Njia hizo za uhakiki ni;
- Namba ya Marejeo ya Cover Note (Cover Note Reference Number)
- Namba ya Usajili wa Gari (Registration Number)
- Namba ya Sticker (Sticker Number)
- Namba ya Chassis (Chassis Number)
Hivyo basi kutoka katika njia hizo hapo juu itaku[asa kuchagua njia moja wapo ili kukamilisha uhakiki wa bima ya gari lako.
Ingiza Taarifa Inayohitajika
Mara baada ya kufanya uchaguzi na kubonyeza maelekezo ya msingi yatafunguka na itakupasa kujaza taarifa zinazo hitajika kulingana na changuzi yako.
Thibitisha na Tafuta
Baada ya kujaza taarifa kwa usahihi sasa itakupasa kubonyeza kitufe kilicho andikwa “Tafuta” au “Search” na kisha mfumo utaanza kutafuta taaarifa za bima yako.
Soma Matokeo ya Utafutaji
Itakubidi usubili ndani ya sekunde kadhaa kisha mfumo utatoa taarifa zote juu ya bima yako, Kama bima yak oni halali basi itakupa taarifa juu ya kampuni iliyo toa hiyo bima n ani mda upi bima yako itaenda kuisha uhalali wake.
Ila kama bima si halali kimatumizi pia mfumo utakuonyesha siku bima yako ilipoisha matumizi yake na itakupasa uchukue hatua za haraka kuweza kukata/kupata bima mpya.
Mapendekezo ya mhariri:
1. Jinsi Ya Kuangalia Salio La NSSF Kwa Njia ya Simu
2. Jinsi Ya Kulipia King’amuzi Cha Azam Tv
3. Jinsi Ya Kupata Salary Slip Kwa Njia Ya Mtandao